Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Hatimaye Nokia Yazindua Simu Mpya ya Nokia 9 Pureview

Zifahamu kwa undani hizi hapa ndio sifa na bei za Nokia 9 Pureview
Sifa na bei ya Nokia 9 Pureview Sifa na bei ya Nokia 9 Pureview

Baada ya kusubiri kwa muda mrefu hatimaye hivi laeo mkutano wa MWC 2019 umeanza rasmi na kampuni mbalimbali ikiwemo Nokia imezindua simu zake mpya. Moja kati ya simu zilizo zinduliwa leo ni simu mpya ya Nokia 9 Pureview, simu ya kwanza kutoka kampuni ya Nokia kuwa na kamera 5 kwa nyuma.

Kwa kuanza Tukiangalia muundo wa simu hii mpya, Nokia 9 Pureview inakuja ikiwa imetengenezwa kwa Glass mbele na nyuma huku ikiwa na fremu ya chuma ambayo ndio imeshikilia simu hiyo. Chuma hiyo imeshikilia simu hiyo kwa umakini kiasi cha simu hiyo kupewa alama za IP67, maana yake ikiwa simu hiyo inauwezo wa kuzuia maji na vumbi.

Advertisement

Nokia 9 pureview body

Kwenye upande wa kioo, Nokia 9 inakuja na kioo cha inch 5.99, chenye resolution ya 2,880 x 1,440 pixels pamoja na teknolojia ya P-OLED pamoja na HDR10. Kioo hichi kinakuja na ulinzi wa Gorilla Glass 5 ambayo hii inazuia kioo hicho kisipate mikwaruzo kwa haraka. Kwenye kioo hicho pia kuna sehemu ya Fingerprint ambayo ipo chini ya kioo ambayo itakusaidia kufungua simu yako kwa haraka zaidi.

https://www.tanzaniatech.one/finder/specs/nokia-9-pureview/

Mbali na ulinzi wa kutumia alama za vidole (Fingerprint), pia Nokia 9 pureview inakuja na ulinzi wa kutambua uso (Face Unlock) ambao unaendeshwa na mfumo wa AI au Artificial Intelligence. Mbali na hayo yote, Nokia 9 inakuja na processor ya Snapdragon 845 yenye kusaidiwa na RAM ya GB 6 pamoja na ukubwa wa ndani au ROM ya GB 128.

Kwa upande wa kamera Pureview inakuja na kamera tano kwa nyuma ambazo zote zinakuja na uwezo wa Megapixel 12, hata hivyo kunayo kamera ya sita kwa nyuma ambayo hii ni TOF au (Time-of-flight camera) ambayo hii kazi yale kubwa ni kupima kiasi cha mwanga kati ya kamera ilipo na kitu kinachopigwa picha, hii husaidia picha kuwa angavu zaidi hata wakati wa usiku.

Nokia 9 Pureview back

Kwa mujibu wa Nokia, Jinsi kamera hizo zinavyofanya kazi ni kuwa kamera zote 5 zinachukua picha moja na kufanya picha hiyo kuwa na muonekano mzuri zaidi na wenye mwanga. Japokuwa Nokia 9 pureview siyo simu bora yenye kamera nzuri zaidi, lakini inajitahidi kutoa picha zenye mwanga zaidi.

Kwenye uzinduzi wa simu hii HMD Global ilisema kuwa simu hii inaweza kuzalisha picha za Raw image format, ambazo unaweza kuzitumia kwenye programu ya Adobe moja kwa moja hasa Adobe Lightroom ambayo inapatikana kwenye simu za Android.

Kwa mbele simu hii inakuja na kamera ya Selfie yenye uwezo wa Megapixel 20 yenye uwezo wa HDR pamoja na uwezo wa kuchukua video za 1080p@30. Sifa nyingine za Nokia 9 Pureview ni kama zifuatazo.

Sifa za Nokia 9 Pureview

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 5.99 chenye teknolojia ya P-OLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16, pamoja na resolution ya 1440 x 2880 pixels.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie) yenye mfumo wa Android One.
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.8 GHz Kryo 385 Gold & 4×1.7 GHz Kryo 385 Silver).
  • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM845 Snapdragon 845 (10 nm).
  • Uwezo wa GPU – Adreno 630.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 128 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 512.
  • Ukubwa wa RAM – GB 6.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 20 yenye,1.0µm na HDR.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tano zote zina Megapixel 12, zenye uwezo wa f/1.8, 1/2.9″, 1.25µm, kamera nyingine ya sita ni TOF. Kamera zote zina uwezo wa kurekodi video za 2160p@30fps, 1080p@30fps, Kamera zote zinasaidiwa na Zeiss optics, dual-LED dual-tone flash, HDR pamoja na panorama.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po 3320 mAh yenye teknolojia ya Fast Charging na Wireless charging.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE
    na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS, GALILEO na USB ya 3.1, Type-C 1.0 reversible connector; magnetic connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi moja ya Midnight Blue
  • Mengineyo – Haina Radio FM, inatumia laini mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama headphone jack. Inayo teknolojia ya kuzuia maji na vumbi, IP67 dust/water proof (up to 1.5m for 30 mins).
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass, barometer.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Chini ya kioo).

Bei ya Nokia 9 Pureview

Kwa upande wa bei Nokia 9 Pureview, Simu hii inatarajiwa kuingia sokoni rasmi siku za karibuni na inategemewa kupatikana kwa kiwango kidogo (Limited edition), simu hii inatarajiwa kuuzwa kuanzia dollar za marekani $699 ambayo hii ni sawa na Shilingi za Tanzania Tsh 1,636,000 bila kodi. Kumbuka bei hii inaweza kuongezeka kutokana na kubadilika kwa viwango vya kubadilisha fedha pamoja na kodi.

Hizi ndio sifa na bei ya Nokia 9 Pureview, kujua zaidi kuhusu simu nyingine ambazo kampuni ya Nokia imezindua kwenye mkutano wa MWC 2019, hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use