Zijue kwa Undani Hizi Hapa Ndio Sifa na Bei ya Nokia 7.1

Kampuni ya Nokia Kupitia HMD Global imerudi tena na Nokia 7.1
Zijue kwa Undani Hizi Hapa Ndio Sifa na Bei ya Nokia 7.1 Zijue kwa Undani Hizi Hapa Ndio Sifa na Bei ya Nokia 7.1

Kampuni ya Nokia kupitia HMD Global hivi leo imefanya tamasha lake la uzinduzi rasmi wa simu yake mpya ya Nokia 7.1, Simu hii ni toleo jipya la simu ya Nokia 7 ambayo ilizinduliwa rasmi mwezi october mwaka jana 2017. Simu hii mpya ya Nokia 7.1 inakuja na maboresho na muonekano bora zaidi huku ikiwa na kioo kikubwa zaidi kuliko Nokia 7 ya mwaka jana.

Simu hii ya Nokia 7.1 inakuja na kioo cha inch 5.84 chenye resolution ya 1080 x 2280 pixel pamoja na uwiano wa 16:9, kioo hicho pia kimetengenezwa kwa teknolojia ya IPS LCD na pia kinakuja na ukingo wa juu maarufu kama notch.

Advertisement

Nokia 7.1 inaendeshwa na processor ya Qualcomm Snapdragon 636 SoC ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 3 au GB 4 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 64 au GB 32. Kwa upande wa kamera simu hii inakuja na kamera ya mbele yenye Megapixel 8 huku kamera za nyuma ambazo ziko mbili zenyewe zinakuja na uwezo wa Megapixel 12 na Megapixel 5 ambazo zote zimetengenezwa na Zeiss optics. Kamera hizo za nyuma zinakuja na sehemu mpya ya “bothie” ambayo in akupa uwezo wa kupiga picha kwa kutumia kamera zote za mbele na nyuma kwa wakati mmoja.

Simu hii mpya ya Nokia inapewa nguvu na battery yenye uwezo wa 3,060 mAh ambayo pia inakuja na uwezo wa Fast Charging yenye uwezo wa kuchaji simu hii kwa haraka. Sifa nyingine za Nokia 7.1 ni kama zifuatazo.

Sifa za Nokia 7.1

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 5.84 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2280 pixels, na uwiano wa 16:9 ratio (~432 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo) inaweza ku-update hadi Android 9 Pie (Android One)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core 1.8 GHz Kryo 260.
  • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM636 Snapdragon 636 Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Adreno 509.
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili simu moja inakuja na GB 32 na nyingine inakuja na GB 64 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 400.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko simu tatu moja ikiwa na RAM ya GB 3 na nyingine ikiwa na GB 4 na ya mwisho ikiwa na GB 6.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8 yenye f/2.0, 24mm.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 16 yenye f/1.8, 1.28µm, Dual Pixel PDAF na nyingine ikiwa na Megapixel 5 yenye f/2.4, 1.12µm, depth sensor. Huku zote zikiwa zinasadiwa na Zeiss optics, dual-LED dual-tone flash, panorama, na HDR.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3060 mAh battery battery yenye teknolojia ya Fast battery charging 9V/2A 18W.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya Type-C 2.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa mbili za Gloss midnight blue, na gloss steel.
  • Mengineyo – Bado haijajulikana kama inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Hybrid Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, na compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa nyuma).

Bei ya Nokia 7.1

Kwa upande wa bei simu hii inatarajiwa kuanza kuagizwa kuanzia October 5 huku tarehe ya kufikiwa na simu hizo kama uliagiza itakua kuanzia tarehe 28 ya mwezi huu October. Kwa upande wa Nokia 7.1 yenye GB 32 na RAM ya GB 3 itauzwa kwa dollar za marekani $349 sawa na Tsh 797,000 bila kodi. Toleo lenye ukubwa wa ndani wa GB 64 na RAM ya GB 4 lenyewe litauzwa kwa dollar $401 ambayo ni sawa na Tsh 913,000 bila kodi. Kumbuka bei inaweza kubadilika kwa Tanzania.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use