Mara baada ya kutangaza TV yake ya kwanza ya Inch 55, kampuni ya Nokia hivi leo imetangaza simu yake mpya ya Nokia 2.3 toleo la maboresho kwa simu ya Nokia 2.2 iliyotoka mwezi wa sita mwaka huu 2019.
Simu hii mpya inakuja na maboresho machache ukilinganisha na toleo la awali la Nokia 2.2, Simu hii inakuja na kioo cha inch 6.2 kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya IPS LCD chenye resolution ya pixel 720 kwa 1520.
Mbali na hayo, Nokia 2.3 inakuja ikiwa inaendeshwa na Processor ya Mediatek Helio A22, inayosaidiwa na RAM ya GB 2 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 32 huku ikiwa na uwezo wa kuongezewa ukubwa huo kwa kutumia memory card hadi ya GB 512.
Kwa upande wa kamera , Nokia 2.3 inakuja na kamera mbili kwa nyuma, Kamera kuu inakuja na Megapixel 13 huku nyingine ikiwa na megapixel 2. Kamera zote hizo kwa pamoja zinaweza kuchukua video ya hadi 1080p@30fps. Kwa mbele Nokia 2.3 inakuja na kamera moja ya selfie yenye uwezo wa Megapixel 5, kamera hii inakuja na teknolojia ya kutambua uso ambayo ni sehemu ya ulinzi wa simu hii.
Nokia 2.3 inaendeshwa na mfumo wa Android 9 (Pie), mfumo ambao juu yake kuna mfumo wa muonekano wa Android One kutoka Google. Simu hii inapewa nguvu na battery isiyotoka ya Li-Ion (Lithium Ion) yenye uwezo wa 5000 mAh ambayo kwa mujibu wa Nokia inauwezo wa kudumu na chaji kwa siku mbili pale inapochajiwa na kujaa.
Bei ya Nokia 2.3
Kwa mujibu wa kampuni ya Nokia, Nokia 2.3 imeingia sokoni tokea siku ya jana na inauzwa kwa dollar za marekani $122 ambayo ni sawa na takribani shilingi za Tanzania TZS 280,000 bila kodi. Kumbuka kwa Tanzania bei hii inaweza kubadilika kutokana na kodi pamoja na kupanda na kushuka kwa viwango vya kubadilisha fedha.
nimelizika na bidhaa zenu nazipatajee