Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Meizu Zero Simu ya Kwanza Isiyokuwa na Kibonyezo Chochote

Simu ya kwanza duniani isiyokuwa na kibonyezo chochote
Sifa na bei ya Meizu zero Sifa na bei ya Meizu zero

Kampuni zinazo tengeneza simu bado zinaendelea kuleta teknolojia mpya kwenye simu za mkononi kila siku, hivi karibuni tumesikia simu zinazo jikunja na pengine hivi karibuni zinakuja simu zisizo na kibonyezo chochote pamoja na sehemu za kuweka laini pamoja na sehemu ya kuchomeka chaji.

Meizu Zero ni simu mpya kutoka kampuni ya Meizu, simu hii imekuja na teknolojia ya kipekee kwani simu hii inakuja bila kibonyesho chochote ikiwa pamoja na sehemu ya kuweka laini, sehemu ya kuchomeka chaji na spika.

Advertisement

Kama ulikuwa unajiuliza simu hii inafanyaje kazi, basi nikwambie simu hii mpya ya Meizu Zero inakuja na sehemu za kugusa kama simu ya HTC U12 Plus, ambapo utagusa kwenye pembe ya simu hiyo kwa ajili ya kuongeza sauti, na kwa upande wa spika simu hii inatumia teknolojia mpya ambapo spika za simu hii zipo chini ya kioo cha simu hiyo.

Meizu zero

Kwa upande wa sehemu ya laini, simu hii inatumia mfumo mpya wa laini za eSIM pamoja na teknolojia ya wireless network huku chaji ya simu hii ikiwa haitumii waya au (Wireless charge).

Meizu zero pic 2

Kwa upande wa sifa za kawaida simu hii inasemekana kuja na kioo cha inch 5.5 chenye teknolojia ya AMOLED. Meizu zero inaendeshwa na processor ya Qualcomm SDM845 Snapdragon 845 (10 nm) yenye uwezo wa Octa-core (4×2.8 GHz Kryo 385 Gold & 4×1.8 GHz Kryo 385 Silver) pamoja na GPU ya Adreno 630. Sifa nyingine za simu hii ni kama zifuatazo.

Sifa za Meizu Zero

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 5.99 chenye teknolojia ya AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.8 GHz Kryo 385 Gold & 4×1.8 GHz Kryo 385 Silver).
  • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM845 Snapdragon 845 (10 nm) Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Adreno 630.
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili simu moja inakuja na GB 64 na nyingine inakuja na GB 128 zote zikiwa Hazina uwezo wa kuongezewa na memory card.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko simu mbili moja ina RAM GB 4 na nyingine ina RAM ya GB 6.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 20 yenye uwezo wa kurekodi video za 1080p@30fps.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko mbili moja ikiwa na Megapixel 12 yenye f/1.8, 27mm (wide), 1/2.3″, 1.55µm, PDAF. Nyingine ikiwa na Megapixel 20 yenye PDAF. Kamera zote mbili zinasaidiwa na Auto HDR, Panorama pamoja na flash ya Dual-LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion (ukubwa wa battery hauja julikana)
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. Haina USB.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi Black, White za White na Black.
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Haina sehemu ya laini lakini pia unaweza kutumia eSim (laini ya simu inayo unganishwa moja kwa moja na kampuni ya simu na sio ile ya kadi), Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Juu ya Kioo).

Bei ya Meizu Zero

Kwa upande wa bei Meizu Zero bado haija julikana itauzwa kwa shilingi ngapi za Tanzania hivyo endelea kutembelea Tanzania Tech tutakujuza zaidi kuhusu bei ya simu hii.

Kwa sasa taarifa kama hii ikufikie ya ujio wa simu kama hii kutoka kampuni ya Vivo, ambayo kwa mujibu wa GSMArena simu hiyo nayo inategemea kuwa simu isiyokuwa na kitufe chochote. Kupata  taarifa zaidi kuhusu sifa pamoja na bei za simu hiyo mpya ya Vivo hakikisha unatembelea Tanzania Tech hapo siku ya kesho.

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use