Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

LG Yazindua Simu Mpya ya LG V40 ThinQ Yenye Kamera 5

Zifahamu hizi hapa ndio sifa na bei ya simu mpya ya LG V40 ThinQ
LG Yazindua Simu Mpya ya LG V40 ThinQ Yenye Kamera 5 LG Yazindua Simu Mpya ya LG V40 ThinQ Yenye Kamera 5

Kampuni ya LG kama ilivyo kampuni ya Samsung, kila mwaka inazindua simu mbili ambazo ni flashship, flagship ni Simu zinazobeba Jina la kampuni au ni simu ambazo ndio muhimu sana kwa kampuni husika. Kwa mwaka huu simu ya LG G7 ThinQ na simu hii mpya ya LG V40 ThinQ ndio simu ambazo ni flagship kutoka kampuni ya LG na kwa sababu ya hilo sifa nyingi za simu hizi zinafanana.

Sasa tukiangalia simu hii mpya ya LG V40 ThinQ, simu hii inakuja na mabadiliko mengi mbalimbali lakini mabadiliko makubwa kwenye simu hii ni pamoja na simu hii kuwa na uwezo wa kamera 5. Kwa mbele simu hii inakuja na kamera mbili ambazo moja ya kamera hizo ni kwaajili ya kupiga picha za kawaida za selfie, ambayo inakuja na Megapixel 8 na nyingine ni kwaajili ya kupiga picha za Group Selfie (wide lens) ambayo inakuja na uwezo wa Megapixel 5.

Advertisement

Kwa nyuma simu hii ya LG V40 ThinQ inakuja na kamera tatu, ambazo kamera moja ni kamera ya kawaida na nyingine ni super wide angle lens na nyingine ni telephoto lens. Kamera ya kawaida iliyoko upande wa kulia inakuja na uwezo wa Megapixel 12 yenye f1.5 lens, Kamera ya pili iliyoko katikati ambayo hii ni super wide angle lens inakuja na uwezo wa Megapixel 16 yenye f1.9 lens na kamera ya mwisho ambayo ipo upande wa kushoto ambayo hii ni telephoto lens yenyewe inakuja na uwezo wa Megapixel 12 yenye f2.4 lens.

LG V40 ThinQ inakuja na uwezo mzuri sana na wa kipekee kwenye kamera hizi kwani utakuwa na uwezo wa kuweza kuona (preview) vidokezo vya picha za kamera hizo zote tatu moja baada ya nyingine kwenye kioo cha simu yako hata kabla ya kupiga picha, kitu ambacho hakipo kwenye simu zote zilizowahi kutoka zenye uwezo wa kamera tatu au zaidi. Maana yake ni kuwa unaweza kupiga picha tatu tofauti kwa kutumia kamera moja baada ya nyingine ndani ya kamera hizo tatu zilizopo kwa nyuma ya simu hizo.

Tukiachana na kamera kwa upande wa sifa LG V40 ThinQ inakuja na sifa za kawaida na kama vile kioo cha inch 6.4 chenye ukingo wa juu maarufu kama notch, processor ya Qualcomm SDM845 Snapdragon 845 ambayo ipo sambamba na RAM ya GB 6 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 6, Sifa nyingine za LG V40 ThinQ ni kama zifuatazo.

Sifa za LG V40 ThinQ

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.4 chenye teknolojia ya P-OLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1440 x 3120 pixels, na uwiano wa 18:9 ratio (~537 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.7 GHz Kryo 385 Gold & 4×1.7 GHz Kryo 385 Silver)
  • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM845 Snapdragon 845 Chipset
  • Uwezo wa GPU – Adreno 630.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 64 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 512.
  • Ukubwa wa RAM – RAM ya GB 6.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Ziko kamera mbili kwa mbele, kamera moja inakuja na uwezo wa Megapixel 8 yenye f/1.9, 1.4µm na nyingine inakuja na uwezo wa Megapixel 5 yenye f/2.2, 1.4µm.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 12 yenye f/1.5, 1.4µm, 3-axis OIS, PDAF & laser A na nyingine ikiwa na Megapixel 16 yenye f/1.9, 1.0µm, no AF na nyingine ikiwa na Megapixel 12 yenye f/2.4, 1.0µm, 2x optical zoom, OIS, PDAF. Huku zote zikiwa zinasadiwa na Flash ya LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 3300 mAh battery yenye uwezo wa fast charging  yenye uwezo wa kujaza asilimia 50% kwa dakika 36 (Quick Charge 3.0).
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 A2DP, LE, aptX HD na GPS ya A-GPS, GLONASS. USB ya 3.1, Type-C 1.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za New Aurora Black na New Moroccan Blue.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line ya Nano-SIM, Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack. Inayo uwezo wa kuzuia maji na vumbi IP68.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass, barometer na color spectrum
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).

Bei ya LG V40 ThinQ

Simu hii mpya inatarajiwa kupatikana kuanzia siku ya October 18 huko nchini marekani na bei yake itakuwa inatofautiana kutokana na kuwa simu hii itapatana kupitia kampuni mbalimbali za simu nchini marekani. US Cellular itakuwa inauzwa simu hii kwa dollar $900, na kupitia T-Mobile itakuwa inauzwa dollar $920, Sprint itapatikana kwa dollar $960 na kuptia Verizon simu hiyo itapatina kwa dollar $980. Kwa Tanzania simu hii inawezekana ikauzwa kwa bei zaidi kuanzia dollar za marekani $1000 bila kodi sawa na Tsh 2,290,000 bila kodi. Kumbuka bei inaweza kubadilika.

1 comments
  1. Habari ndugu nauliza aweza pata wapi kiii cha hii simu LG V40 , mimi nipo dar es salaam namba yangu ya simu 0714935771

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use