Kampuni ya LG hivi leo imatangaza kuja na simu yake mpya ya LG Candy, simu hiyo ni simu ya bei nafuu kwa wapenzi wa simu za LG na inakuja na sifa za kawaida kama vile kioo cha inch 5.0-inch ambacho kimetengenezwa kwa IPS display. processor ya 1.3GHz quad-core ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 2 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 16. Sifa nyingine za LG Candy ni kama zifuatazo
Sifa za LG Candy
- Ukubwa wa Kioo – Inch 5.0 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1280 pixels, na uwiano wa 16:9 ratio (~294 ppi density).
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 7.1.2 (Nougat).
- Uwezo wa Processor – Quad-core 1.3 GHz Cortex-A53.
- Aina ya Processor (Chipset) – Hisilicon Kirin 710 Chipset.
- Uwezo wa GPU – Bado Haijajulikana.
- Ukubwa wa Ndani – GB 18 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card ya hadi GB 512.
- Ukubwa wa RAM – RAM ya GB 2
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 5
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 8 yenye Flash ya LED flash.
- Uwezo wa Battery – Battery Inayotoka ya Li-Ion Li-Ion 2500 mAh battery.
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 b/g/n, Wi-Fi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP pamoja na GPS ya A-GPS. USB 2.0, Type-C 1.0 reversible connector.
- Rangi – Inakuja kwa rangi nne za Black, Gold, Blue na Silver
- Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
- Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, proximity.
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
- Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa nyuma).
Bei ya LG Candy
Kwa upande wa bei LG Candu itauzwa kwanza kwa nchini india kuanzia tarehe 3 ya mwezi september kwa rupee ya india INR 6999 ambayo ni sawa na Tsh 226,000. Kumbuka bei hii ni bila kodi hivyo bei inaweza kubadilika kwa Tanzania.
serdw
nice sanaaa