Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Kampuni ya Lenovo Yazindua Simu Mpya ya Lenovo Z5s

Hizi hapa sifa kamili pamoja na bei ya Lenovo Z5s
Kampuni ya Lenovo Yazindua Simu Mpya ya Lenovo Z5s Kampuni ya Lenovo Yazindua Simu Mpya ya Lenovo Z5s

Wakati tukikaribia mwishoni mwa mwaka 2018, bado kampuni mbalimbali za simu zinapambana kutoa simu zake mpya zitakazo malizia mwaka. Moja ya kampuni hizo ni kampuni ya lenovo ambayo hivi leo imatangaza toleo jipya la simu yake ya Lenovo Z5s.

Lenovo Z5s ni toleo la maboresho la simu ya Lenovo Z5 Pro ambayo ilizinduliwa mwezi wa 11 mwaka huu. Hata hivyo simu hii mpya ya Lenovo Z5s anaingia kwenye historia kwa kuwa simu ya kwanza kutoka kampuni ya Lenovo kuwa na ukingo wa juu maarufu kama Top notch.

Advertisement

Kioo chenye ukingo huo wa juu kinakuja na ukubwa wa inch 6.3 ambacho pia kimetengenezwa kwa teknolojia ya LTPS LCD huku kikiwa na resolution ya 1080 x 2340 pixels pamoja na uwiano wa 19.5:9. Tukiwa bado tuko mbele ya simu hii kuna kamera moja ya Selfie ambayo inakuja na uwezo wa MP 16.

Kwa nyuma simu hii inakuja na kamera tatu huku kamera kuu ikiwa na uwezo wa Megapixel 16 ambayo hii ni wide-angle lens, na secondary kamera hii ni telephoto lens yenye uwezo wa Megapixel 8 huku pia ikiwa na uwezo wa optical zoom 2x na kamera ya mwisho ikiwa ina uwezo wa Megapixel 5 ambayo hii ni depth-sensor.

Lenovo Z5s ina endeshwa na processor ya Snapdragon 710 ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 4 na ukubwa wa ndani wa GB 64, nyingine ikiwa na RAM ya GB 6 na ukubwa wa ndani wa GB 64 na RAM ya GB 6 na ukubwa wa ndani wa GB 128. Sifa nyingine za Lenovo Z5s ni kama zifuatazo.

Sifa za Lenovo Z5s

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.3 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2340 pixels, na uwiano wa 19.5:9 ratio (~403 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core 2.2 GHz Kryo 260.
  • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM710 Snapdragon 710 (14 nm) Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Adreno 616.
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili moja ikiwa na ukubwa wa ndani wa GB 64 na nyingine ikiwa na ukubwa wa ndani wa GB 128 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi GB 256.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko za aina mbili moja ikiwa na RAM ya GB 6 na nyingine ikiwa na RAM ya GB 4.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele –  Megapixel 16 yenye uwezo f/2.0 huku ikiwa na uwezo wa kuchukua video za 1080p@30fps.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu moja ikiwa na Megapixel 16 /1.8, 26mm (wide), PDAF na nyingine inakuja na Megapixel 8 yenye f/2.4, (telephoto), PDAF, 2x optical zoom huku kamera nyingine ikiwa na Megapixel 5 yenye f/2.4, depth sensor. Kamera zote zinasaidiwa na Flash ya Dual-LED dual-tone flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3300 mAh yenye uwezo wa Fast battery charging 15W
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS. 2.0, Type-C 1.0 reversible connector, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Starry Night Grey, Love Orange na Titanium Blue
  • Mengineyo – Bado haija julikana kama inakuja na Radio FM, Inatumia Line Mbili za Hybrid Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by). Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa nyuma).

Bei ya Lenovo Z5s

Kwa upande wa bei, Lenovo Z5s itakuja ikiwa inauzwa kwa nchini china kwa Yuan CNY1,398 sawa na Tsh 467,000 sawa na Shilingi za Kenya Ksh 21,000 kwa toleo lenye RAM ya GB 4 na ukubwa wa ndani wa GB 64. Kwa toleo lenye ukubwa wa ndani wa GB 128 na RAM ya GB 6 litauzwa kwa Yuan CNY1,998 ambayo ni sawa na Tsh 667,000 bila kodi ambayo ni sawa na Shilingi za Kenya Ksh 29,700 bila kodi. Kwa mujibu wa tovuti ya Lenovo, simu hii itaanza kuuzwa kuanzia mwezi huu tarehe 24.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use