Kampuni ya Xiaomi kupitia chapa yeke ya Redmi imezindua laptop mbili mpya za Redmi Book 14 na Redmi Book 16 (2025), zote zikiwa zinakuja na vipengele vya kisasa vya utendaji na muundo wa kuvutia.
TABLE OF CONTENTS
Skrini
Redmi Book 14 (2025): Ina skrini nzuri yenye uwiano wa 16:10 na azimio la 2,880 x 1,800 pikseli. Paneli inasaidia kiwango cha kuburudisha cha 120 Hz, ambayo inamaanisha kuwa picha na video zitakuwa smooth na zenye uhalisia zaidi.
Mwangaza wa skrini unafikia 400 nits, hivyo unaweza kuitumia kwa urahisi hata katika mazingira yenye mwanga mkali. Zaidi ya hayo, skrini inachukua asilimia 100% ya wigo wa rangi ya sRGB, ambayo inahakikisha kuwa rangi zinaonekana kwa usahihi.
Redmi Book 16 (2025): Ina sifa sawa na Book 14, lakini tofauti yake ikiwa ni uwiano wa 2,560 x 1,600 pikseli.
Utendaji
- Zote zina vifaa vya kisasa vya utendaji, ikiwa ni pamoja na RAM hadi 32 GB ya aina ya LPDDR5X, ambayo inaruhusu kompyuta kufanya kazi kwa kasi na haraka. Hifadhi ya ndani ni ya aina ya SSD ya PCIe 4.0 yenye uwezo wa hadi 1 TB.
- Zote zinaendesha mfumo wa uendeshaji wa Windows 11
- Kwa ajili ya kuhakikisha kuwa kompyuta hazipati joto kupita uwezo wake, laptop hizi zina mfumo wa kupooza joto la kuwa la kawaida wakati wa matumizi makali.
Betri na Kuchaji
- Book 14 (2025): Ina betri ya 56 Wh, wakati Book 16 ina betri kubwa zaidi ya 72 Wh. Hii inamaanisha kuwa unaweza kutumia kompyuta kwa muda mrefu zaidi bila kuichaji tena.
- Zote zinakuja na uwezo wa Fast Charging hadi 100W kwa kutumia adapta ya GaN, ambayo ni ndogo na nyepesi lakini yenye uwezo mkubwa wa kuchaji.
Viunganisho
Kompyuta zote zina viunganisho ikiwa ni pamoja na:
- USB-C 3.2 Gen 2 kwa kuunganisha vifaa na kuchaji.
- HDMI 2.1 kwa kuunganisha kwenye skrini za nje.
- Sehemu mbili za USB-A 3.2 Gen 1.
- Sehemu moja ya USB-A 2.0.
- Sehemu moja ya Headphone Jack ya 3.5 mm.
Laptop zote zina teknolojia ya Wi-Fi 6, Bluetooth 5.2 ikiwa pamoja na teknolojia ya Dolby Vision na Dolby Atmos, ambayo inaboresha ubora wa picha na sauti. Kamera ya mbele iliyojengwa kwenye ukingo ikiwa na uwezo wa hadi 1080p
Bei na Upatikanaji
Bei za Redmi Book 14 na Redmi Book 16 zinatofautiana kulingana na uwezo wa RAM na hifadhi.
Redmi Book 14 (2025)
- 16 GB + 512 GB: CNY 4,599, USD $630 – TZS 1,499,400 (approx.)
- 16 GB + 1 TB: CNY 4,899, USD $670 – TZS 1,594,600 (approx.)
- 32 GB + 1 TB: CNY 5,199, USD $715 – TZS 1,701,700 (approx.)
Redmi Book 16 (2025)
- 16 GB + 512 GB: CNY 4,799, USD $655 – TZS 1,558,900 (approx.)
- 16 GB + 1 TB: CNY 5,099, USD $700 – TZS 1,666,000 (approx.)
- 32 GB + 1 TB:, CNY 5,399, USD $740 – TZS 1,761,200 (approx.)
Laptops hizi zinaweza kununuliwa katika duka la kampuni na wauzaji wengine waliochaguliwa nchini China.
Uzinduzi wa Kimataifa
Kwa sasa, bado hakuna uhakika wa upatikanaji wa laptop hizi nchin Tanzania kwani, mara ya mwisho kuona Redmi Book zikiuzwa kimataifa ilikuwa mwanzoni mwa mwaka 2023.
Hata hivyo, huenda hatua hii ikabadilika kwa siku za usoni. Kwa taarifa juu ya sehemu ya kununua laptop hizi endelea kutembelea Tanzania Tech