Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya iPhone Xs na iPhone Xs Max

Hizi hapa sifa kamili pamoja na bei ya iPhone Xs na iPhone Xs Max
sifa na bei ya iPhone Xs na iPhone Xs Max sifa na bei ya iPhone Xs na iPhone Xs Max

Hayawi hayawi sasa yamekuwa, baada ya tetesi za muda mrefu kampuni ya Apple usiku huu imefanya uzinduzi wa bidhaa zake mbalimbali ikiwemo simu mpya za iPhone Xs pamoja na iPhone Xs Max. Simu hizi ni picha halisi ya simu mpya za Apple zitakazo endelea kuwepo kuanzia mwaka huu, hii inamaanisha kuanzia sasa inawezekana kabisa simu zenye muundo wa zamani hazitokwepo tena sokoni na badala yake sasa tegemea kuona simu za iPhone zenye muundo wa iPhone X.

Anyway.. tukija kwenye uzinduzi wa siku ya leo, kampuni ya Apple imeweza kuzindua simu hizi ambazo zinakuja na maboresho kadhaa ikiwa pamoja na kioo kikubwa cha inch 6.5 kwa simu ya iPhone Xs Max ambayo pia inakuja na kioo chenye teknolojia ya “Super Retina” display chenye resolution ya 1242 x 2688 pixel pamoja na teknolojia zingine kama vile HDR10 pamoja na Dolby Vision.

Advertisement

Kwa upande wa iPhone Xs yenyewe inakuja na teknolojia hizo hizo lakini inakuja na kioo kidogo cha cha Inch 5.8 chenye resolution ya 1125 x 2436 pixels. Simu zote mbili za iPhone Xs na iPhone Xs Max zinakuja na kamera mbili kwa nyuma zenye uwezo wa Megapixel 12 kwa kila kamera huku pia simu hizi kwa mbele zote zikiwa na kamera za Megapixel  7. Sifa nyingine za iPhone Xs na iPhone Xs Max.

Sifa za iPhone Xs

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 5.8 chenye teknolojia ya Super AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1125 x 2436 pixels, na uwiano wa 19.5:9 ratio (~458 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – iOS 12
  • Uwezo wa Processor – Hexa-core.
  • Aina ya Processor (Chipset) – Apple A12 Bionic Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Apple GPU (4-core graphics).
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina tatu moja inakuja na ukubwa wa ndani wa GB 64 nyingine GB 256, na nyingine GB 512 zote zikiwa hazina uwezo wa memory card.
  • Ukubwa wa RAM – RAM ya GB 4.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 7 yenye f/2.2, 32mm pamoja na uwezo wa kuchukua video za 1080p@60fps.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili moja ikiwa na Megapixel 12 yenye f/1.8, 28mm, 1.4µm, OIS, PDAF , na kamera nyingine pia inakuja na Megapixel 12 yenye f/2.4, 52mm, 1µm, AF, OIS, 2x optical zoom.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion (ukubwa wa battery haujajulikana) battery yenye teknolojia ya Fast battery charging.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS, GALILEO, QZSS. USB ya Type-C 2.0, proprietary reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Space Gray na Silver, Gold
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack. Inakuja na uwezo wa kuzuia maji na vumbi (IP68 dust/water proof (maji ya urefu wa 2m kwa dakika 30), pia Inakuja na Apple Pay.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Face ID, accelerometer, gyro, proximity, compass na barometer.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Haina Fingerprint, inakuja na Ulinzi wa kutambua uso na macho (Face ID).

Kwa upande wa simu ya iPhone Xs Max hakuna tofauti sana kwani tofauti kubwa iliyoko kati ya iPhone Xs na iPhone Xs Max ni ukubwa wa kioo pekee.

Sifa za iPhone Xs Max

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.5 chenye teknolojia ya Super AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1242 x 2688 pixels, na uwiano wa 19.5:9 ratio (~458 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – iOS 12
  • Uwezo wa Processor – Hexa-core.
  • Aina ya Processor (Chipset) – Apple A12 Bionic Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Apple GPU (4-core graphics).
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina tatu moja inakuja na ukubwa wa ndani wa GB 64 nyingine GB 256, na nyingine GB 512 zote zikiwa hazina uwezo wa memory card.
  • Ukubwa wa RAM – RAM ya GB 4.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 7 yenye f/2.2, 32mm pamoja na uwezo wa kuchukua video za 1080p@60fps.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili moja ikiwa na Megapixel 12 yenye f/1.8, 28mm, 1.4µm, OIS, PDAF , na kamera nyingine pia inakuja na Megapixel 12 yenye f/2.4, 52mm, 1µm, AF, OIS, 2x optical zoom.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion (ukubwa wa battery haujajulikana) battery yenye teknolojia ya Fast battery charging.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS, GALILEO, QZSS. USB ya Type-C 2.0, proprietary reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Space Gray na Silver, Gold
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack. Inakuja na uwezo wa kuzuia maji na vumbi (IP68 dust/water proof (maji ya urefu wa 2m kwa dakika 30), pia Inakuja na Apple Pay.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Face ID, accelerometer, gyro, proximity, compass na barometer.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Haina Fingerprint, inakuja na Ulinzi wa kutambua uso na macho (Face ID).

Bei ya iPhone Xs na iPhone Xs Max

Kwa upande wa bei simu hizi mpya za iPhone Xs na Xs Max zinakuja kwa bei ya dollar $999 mbayo ni sawa na Tsh 2,284,000 kwa iPhone Xs yenye GB 64, huku iPhone Xs ya GB 256 itauzwa kwa dollar $1,149 ambayo ni sawa na Tsh 2,627,000, na iPhone Xs ya GB 512 itauzwa kwa dollar za marekani $1,349 sawa na Tsh 3,084,000. Kwa sasa bado bei ya iPhone Xs ya GB 128 haijajulikana rasmi.

Kwa upande wa iPhone Xs Max yenye ukubwa wa GB 64 itakuja kwa dollar za marekani $1,099 ambayo ni sawa na Tsh 2,512,000, huku kwa iPhone Xs Max ya GB 128 yenyewe itauzwa kwa dollar za marekani $1,249 ambayo ni sawa na Tsh 2,855,000, huku iPhone Xs Max ya GB 512 yenyewe itauzwa kwa dollar za $1,449 sawa na Tsh 3,312,000 bila kodi.

Na hizo ndio sifa pamoja na bei ya iPhone Xs pamoja na iPhone Xs Max ambazo zimezinduliwa hivi karibuni, simu hizi zitaanza kupatikana rasmi kuanzia mwezi ujao tarehe 19.

1 comments
  1. hello mi naomba msaada nimeibiwa sim yangu na alie iiba nimefanikiwa kupata mawasiloano yake je nawezaje kumpata kupitia namba yake ya sim kwa kutumia app yoyote inayo directions moja kwa moja alipo

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use