Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya iPhone 11, 11 Pro na 11 Pro Max

Kampuni ya Apple imezindua simu mpya ambazo wengi walikuwa wakizingoja
Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya iPhone 11, 11 Pro na 11 Pro Max Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya iPhone 11, 11 Pro na 11 Pro Max

Hapo siku ya jana kampuni ya Apple ilizindua simu zake mpya za iPhone 11, simu ambazo zimekuwa ni simu za tofauti sana hasa kwa muundo wake wa nyuma kutokana na kamera mpya zinazopatikana kwenye simu hiyo.

Kupitia makala hii tutaenda kuangalia muundo, sifa pamoja na bei za simu hizi mpya za iPhone 11, iPhone 11 Pro, pamoja na iPhone 11 Pro Max. Basi bila kuendelea kupoteza muda zaidi twende tuangalie simu hizi.

Advertisement

iPhone 11

iPhone 11 mwaka huu inakuja na kioo cha inch 6.1 kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya IPS LCD, kioo hicho kina uwezo wa kuonyesha picha na video zenye resolution ya hadi pixels 1620 x 2160. Mbali na hayo kioo hicho kime tengenezwa kwa teknolojia ya kuzuia kioo hicho kuharibika kwa kuchubuka kwa urahisi au Scratch-resistant glass, na oleophobic coating.

Kwa juu simu hii inakuja na ukingo wa juu maarufu kama topnotch, ukingo ambao unatumika kuhifadhi spika na kamera ya mbele ya Megapixel 12 ambayo inauwezo wa kuchukua video za hadi 4K, hii ni sawa na kusema simu hii ina uwezo wa kuchukua video za pixels 2160p@24/30/60fps, 1080p@30/60/120fps, na gyro-EIS.

Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya iPhone 11, 11 Pro na 11 Pro Max

Kwa nyuma simu hii inakuja na kamera mbili kubwa, kamera ambazo zote zinakuja na uwezo wa Megapixel 12 (wide) pamoja na Megapixel 12 (ultrawide) ambayo hutumika kupiga picha za umbali zaidi. Kamera zote kwa pamoja zina uwezo wa kuchukua video za hadi 4K ambayo ni sawa na kusema simu hii inauwezo wa kuchukua video za hadi pixels 2160p@24/30/60fps, 1080p@30/60/120/240fps. Mbali na hayo, kamera zote za iPhone 11 zina saidiwa na teknolojia za HDR (photo/panorama) pamoja na Flash ya Quad-LED dual-tone flash.

Kwa upande wa sifa za ndani, iPhone 11 inakuja na processor ya A13 Bionic (7 nm+) processor ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 4 pamoja na ukubwa wa ndani au ROM ya kuchagua kati ya GB 64, GB 128 na GB 256. Kama zilivyo simu nyingine za iPhone simu hii pia haina sehemu ya kuweka memory card. Sifa nyingine za iPhone 11 ni kama zifuatazo.

Sifa za iPhone 11

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.1 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 828 x 1792 pixels, na uwiano wa 19.5:9 ratio (~326 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – iOS 13
  • Uwezo wa Processor – Hexa-core.
  • Aina ya Processor (Chipset) – Apple A13 Bionic Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Apple GPU (4-core graphics).
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina tatu moja inakuja na ukubwa wa ndani wa GB 64 nyingine GB 128, na nyingine GB 256 zote zikiwa hazina uwezo wa memory card.
  • Ukubwa wa RAM – RAM ya GB 4.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8 yenye f/2.2, 32mm pamoja na uwezo wa kuchukua video za 2160p@24/30/60fps, 1080p@30/60/120fps, gyro-EIS.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Zipo kamera mbili moja ikiwa na Megapixel 12 yenye f/1.8, 26mm (wide), 1/2.55″, 1.4µm, PDAF, OIS na kamera ya pili inakuja na Megapixel 12 yenye f/2.4, 13mm (ultrawide). Kamera zote zina saidiwa na Quad-LED dual-tone flash, HDR (photo/panorama).
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3110 mAh battery yenye teknolojia ya Fast battery charging.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS, GALILEO, QZSS. USB ya Type-C 2.0, proprietary reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi sita za Black, Green, Yellow, Purple, Red, na White
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack. Inakuja na uwezo wa kuzuia maji na vumbi (IP67 dust/water proof (maji ya urefu wa 1m kwa dakika 30), pia Inakuja na Apple Pay.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Face ID, accelerometer, gyro, proximity, compass na barometer.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Haina Fingerprint, inakuja na Ulinzi wa kutambua uso na macho (Face ID).

Bei ya iPhone 11

Kwa upande wa bei, Apple imetangaza kuwa simu hii inategemewa kupatikana kuanzia mwezi huu na oda zimeanza kupokelewa kuanzia siku ya jana kwa dollar za marekani $699 ambayo ni sawa na takribani shilingi za Tanzania TZS 1,607,000 bila kodi. Kumbuka bei ya simu hii inaweza kubadilika kulingana na ukubwa wa ROM ya simu, kodi pamoja na viwango vya kubadilisha fedha

iPhone 11 Pro

Kwa upande wa simu mpya ya iPhone 11 Pro, simu hii inakuja na kioo cha inch 5.8 ambacho kime tengenezwa kwa teknolojia ya OLED huku kikiwa na resolution ya hadi pixels 1125 x 2436. Kama ilivyo iPhone 11, simu hii pia inakuja na kioo kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya kuzuia kioo hicho kuharibika kwa kuchubuka kwa urahisi au Scratch-resistant glass, na oleophobic coating.

iPhone 11 Pro kama ilivyo iPhone 11, Simu hii pia inakuja na ukingo wa juu ambao unatumika kuhifadhi kamera ya selfie ya hadi Megapixel 12. Kamera hii inakuja na uwezo wa kuchukua video za hadi 4K sawa na kusema simu hii inauwezo wa kuchukua video za pixels 2160p@24/30/60fps, 1080p@30/60/120fps, gyro-EIS.

Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya iPhone 11, 11 Pro na 11 Pro Max

Kwa nyuma simu hii inakuja na kamera tatu, kamera zote zikiwa zinakuja na uwezo sawa wa Pixel huku kamera kuu ikiwa na Megapixel 12 ambayo ni (wide lens), na nyingine ikiwa na Megapixel 12 ambayo ni (telephoto lens) na kamera ya mwisho ikiwa na Megapixel 12 ambayo ni (ultrawide lens). Kamera zote hizi kwa pamoja zina uwezo wa kuchuku video za hadi 4K ambayo ni sawa na kusema simu hizi zina uwezo wa kuchua video hadi za pixels 2160p@24/30/60fps, pamoja na pixels 1080p@30/60/120/240fps.

Kwa upande wa sifa za ndani, iPhone 11 Pro inakuja ikiwa inaendeshwa na processor ya Apple ya A13 Bionic (7 nm+) ambayo inasidiwa na RAM ya GB 4 pamoja na ukubwa wa ndani au ROM ya GB 64, GB 256, pamoja na GB 512. Simu hii pia haina sehemu ya kuweka memory card. Sifa nyingine za iPhone 11 Pro ni kama zifuatazo.

Sifa za iPhone 11 Pro

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 5.8 chenye teknolojia ya OLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1125 x 2436 pixels, na uwiano wa 19.5:9 ratio (~458 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – iOS 13
  • Uwezo wa Processor – Hexa-core.
  • Aina ya Processor (Chipset) – Apple A13 Bionic Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Apple GPU (4-core graphics).
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina tatu moja inakuja na ukubwa wa ndani wa GB 64 nyingine GB 256, na nyingine GB 512 zote zikiwa hazina uwezo wa memory card.
  • Ukubwa wa RAM – RAM ya GB 4.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 12 yenye f/2.2, 32mm pamoja na uwezo wa kuchukua video za 2160p@24/30/60fps, 1080p@30/60/120fps, gyro-EIS.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Zipo kamera mbili moja ikiwa na Megapixel 12 yenye f/1.8, 26mm (wide), 1/2.55″, 1.4µm, PDAF, OIS na kamera ya pili inakuja na Megapixel 12 yenye f/2.4, 13mm (ultrawide). Kamera zote zina saidiwa na Quad-LED dual-tone flash, HDR (photo/panorama). Na uwezo wa kuchukua video za 2160p@24/30/60fps, pamoja na 1080p@30/60/120/240fps.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3190 mAh battery yenye teknolojia ya Fast battery charging.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS, GALILEO, QZSS. USB ya Type-C 2.0, proprietary reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi nne za Space Gray, Silver, Gold, na Midnight Green
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack. Inakuja na uwezo wa kuzuia maji na vumbi (IP67 dust/water proof (maji ya urefu wa 1m kwa dakika 30), pia Inakuja na Apple Pay.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Face ID, accelerometer, gyro, proximity, compass na barometer.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Haina Fingerprint, inakuja na Ulinzi wa kutambua uso na macho (Face ID).

Bei ya iPhone 11 Pro

Kwa upande wa bei, Apple imetangaza kuwa iPhone 11 Pro inategemewa kupatikana kuanzia mwezi huu na oda zimeanza kupokelewa kuanzia siku ya jana kwa dollar za marekani $999 ambayo ni sawa na takribani shilingi za Tanzania TZS 2,297,000 bila kodi. Kumbuka bei ya simu hii inaweza kubadilika kulingana na ukubwa wa ROM ya simu, kodi pamoja na viwango vya kubadilisha fedha

iPhone 11 Pro Max

Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya iPhone 11, 11 Pro na 11 Pro Max

Kwa upande wa iPhone 11 Pro Max simu hii inakuja na muonekano wa tofauti kidogo na muonekano wa simu nyingine za Apple zilizo zinduliwa jana. Simu hii inakuja na kioo kikubwa cha inch 6.5 kioo ambacho kime tengenezwa kwa teknolojia ya Super Retina XDR OLED, kioo ambacho kinaweza kuonyesha video au picha zenye resolution hadi ya pixels 1242 x 2688.

iPhone 11 Pro Max inakuja na ukingo wa juu ambao unatumika kuhifadhi kamera ya selfie ya hadi Megapixel 12. Kamera hii inakuja na uwezo wa kuchukua video za hadi 4K sawa na kusema simu hii inauwezo wa kuchukua video za pixels 2160p@24/30/60fps, pamoja na 1080p@30/60/120fps, gyro-EIS. Kamera hii inasaidiwa na teknolojia za TOF 3D camera pamoja na HDR.

Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya iPhone 11, 11 Pro na 11 Pro Max

Kwa nyuma simu hii inakuja na kamera tatu, kamera zote zikiwa zinakuja na uwezo sawa wa Pixel huku kamera kuu ikiwa na Megapixel 12 ambayo ni (wide lens), na nyingine ikiwa na Megapixel 12 ambayo ni (telephoto lens) na kamera ya mwisho ikiwa na Megapixel 12 ambayo ni (ultrawide lens). Kamera zote hizi kwa pamoja zina uwezo wa kuchuku video za hadi 4K ambayo ni sawa na kusema simu hizi zina uwezo wa kuchua video hadi za pixels 2160p@24/30/60fps, pamoja na pixels 1080p@30/60/120/240fps.

Kwa upande wa sifa za ndani, iPhone 11 Pro Max inakuja ikiwa inaendeshwa na processor ya Apple ya A13 Bionic (7 nm+) ambayo inasidiwa na RAM ya GB 4 pamoja na ukubwa wa ndani au ROM ya GB 64, GB 256, pamoja na GB 512. iPhone 11 Pro Max pia haina sehemu ya kuweka memory card. Sifa nyingine za iPhone 11 Pro Max ni kama zifuatazo.

Sifa za iPhone 11 Pro Max

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.5 chenye teknolojia ya Super Retina XDR OLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1242 x 2688 pixels, na uwiano wa 19.5:9 ratio (~458 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – iOS 13
  • Uwezo wa Processor – Hexa-core.
  • Aina ya Processor (Chipset) – Apple A13 Bionic Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Apple GPU (4-core graphics).
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina tatu moja inakuja na ukubwa wa ndani wa GB 64 nyingine GB 256, na nyingine GB 512 zote zikiwa hazina uwezo wa memory card.
  • Ukubwa wa RAM – RAM ya GB 4.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 12 yenye f/2.2, 32mm pamoja na uwezo wa kuchukua video za 2160p@24/30/60fps, 1080p@30/60/120fps, gyro-EIS.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Zipo kamera mbili moja ikiwa na Megapixel 12 yenye f/1.8, 26mm (wide), 1/2.55″, 1.4µm, PDAF, OIS na kamera ya pili inakuja na Megapixel 12 yenye f/2.4, 13mm (ultrawide). Kamera zote zina saidiwa na Quad-LED dual-tone flash, HDR (photo/panorama). Na uwezo wa kuchukua video za 2160p@24/30/60fps, pamoja na 1080p@30/60/120/240fps.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3500 mAh battery yenye teknolojia ya Fast battery charging.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS, GALILEO, QZSS. USB ya Type-C 2.0, proprietary reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi nne za Space Gray, Silver, Gold, na Midnight Green
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack. Inakuja na uwezo wa kuzuia maji na vumbi (IP67 dust/water proof (maji ya urefu wa 1m kwa dakika 30), pia Inakuja na Apple Pay.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Face ID, accelerometer, gyro, proximity, compass na barometer.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Haina Fingerprint, inakuja na Ulinzi wa kutambua uso na macho (Face ID).

Bei ya iPhone 11 Pro Max

iPhone 11 Pro Max inategemewa kupatikana kuanzia mwezi huu na oda zimeanza kupokelewa kuanzia siku ya jana kwa dollar za marekani $1,099 ambayo ni sawa na takribani shilingi za Tanzania TZS 2,527,000 bila kodi. Kumbuka bei ya simu hii inaweza kubadilika kulingana na ukubwa wa ROM ya simu, kodi pamoja na viwango vya kubadilisha fedha.

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use