Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Hizi Hapa Sifa na Bei ya iPad Pro 11 na iPad Pro 12.9 (2018)

….inaendelea baada ya kuzindua laptop mpya ya MacBook Air (2018)
Hizi Hapa Sifa na Bei ya iPad Pro 11 na iPad Pro 12.9 (2018) Hizi Hapa Sifa na Bei ya iPad Pro 11 na iPad Pro 12.9 (2018)

Hapo jana kampuni ya Apple ilizindua bidhaa zake mpya ikiwa ni pamoja na MacBook Air 2018 pamoja na tablet mpya za iPad Pro 11 na iPad Pro 12.9. Kwa sababu jana tulisha angalia kuhusu laptop hiyo mpya ya MacBook Air 2018, sasa leo ni wakati wa kuangalia yaliyomo kwenye tablet hizi mpya za iPad Pro 11 na iPad Pro 12.9.

Kwa kuanza tuangalie vioo vya tablet hizi, kama majina yanavyosema kuna iPad Pro yenye kioo cha inch 11 na vilevile kunayo iPad Pro yenye kioo cha inch 12.9. iPad zote hizi zinakuja na kioo cha super-sharp Liquid Retina display ambacho pia kinakuja na kingo ndogo zenye round kwenye pembeni, hata hivyo kutokana na kuwa na kingo ndogo iPad hizi zimeondolewa sehemu ya kitufe cha katikati ambacho kilikuwa na sehemu ya ulinzi ya fingerprint na sasa iPad hizi zinatumia ulinzi wa kutambua uso maarufu kama Face ID.

Advertisement

Mbali na hayo sasa iPad Pro hizi mpya zinakuja na kalamu iliyo boreshwa zaidi na kalamu hii sasa inachajiwa bila waya kwa kunatishwa pembeni ya iPad hizo. Vilevile iPad hizi zinakuja na USB-C port ambayo unaweza kuitumia kwenye vitu mbalimbali kama vile kioo cha kompyuta na kamera na vitu vingine kama hivyo.

Kwa upande wa processor iPad hizi zinakuja na processor ya Apple A12X Bionic chipset yenye uwezo wa Octa-core (4x Vortex + 4x Tempest) na GPU ya Apple GPU (7-core graphics) yenye uwezo wa kucheza game zenye uwezo mkubwa kama vile game ya Assassin’s Creed Rebellion ambayo sasa inapatikana maalum kwa ajili ya iPad. Sifa nyingine za iPad Hizi ni kama zifuatazo.

Sifa za iPad Pro 11 (2018)

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 11.00 chenye teknolojia ya LED-backlit IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1668 x 2388 pixels, na uwiano wa (~265 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – iOS 12.
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4x Vortex + 4x Tempest).
  • Aina ya Processor (Chipset) – Apple A12X Bionic (7 nm) Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Apple GPU (7-core graphics).
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko iPad za aina tatu simu moja inakuja na GB 64, nyingine GB 256 pamoja na nyingine inakuja na GB 512 zote zikiwa hazina uwezo wa Memory Card.
  • Ukubwa wa RAM – Bado haijajulikana
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 7 yenye f/2.2, 32mm pamoja na uwezo wa Face detection, HDR na panorama.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 12 yenye f/1.8, 1/3″, PDAF, huku ikiwa inasadiwa na HDR, pamoja na Quad-LED dual-tone flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po battery (29.37 Wh) yenye teknolojia ya kuweza kuchaji simu nyingine.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya Type-C 1.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Silver na Space Gray
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Nano-SIM / Electronic SIM card (Apple e-SIM), haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Face ID, accelerometer, gyro, proximity, barometer
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Ulinzi wa Face ID

Bei ya iPad Pro 11 (2018)

Kwa upande wa bei, iPad Pro ya Inch 11 itauzwa kuanzia dollar za marekani $800 ambayo ni sawa na Tsh 1,833,000 hadi dollar $1,550 ambayo ni sawa na Tsh 3,550,000 kwa iPad Pro ya inch 11 yenye ukubwa wa ndani wa Terabyte (TB) 1.

Sifa za iPad Pro 12.9 (2018)

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 11.00 chenye teknolojia ya LED-backlit IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 2048 x 2732 pixels, na uwiano wa 4:3 ratio (~265 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – iOS 12.
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4x Vortex + 4x Tempest).
  • Aina ya Processor (Chipset) – Apple A12X Bionic (7 nm) Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Apple GPU (7-core graphics).
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko iPad za aina nne iPad moja inakuja na GB 64, nyingine GB 256 na nyingine GB 512 pamoja na ya mwisho ambayo inakuja na TB 1 zote zikiwa hazina uwezo wa Memory Card.
  • Ukubwa wa RAM – Bado haijajulikana
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 7 yenye f/2.2, 32mm pamoja na uwezo wa Face detection, HDR na panorama.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 12 yenye f/1.8, 1/3″, PDAF, huku ikiwa inasadiwa na HDR, pamoja na Quad-LED dual-tone flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po battery (36.71 Wh) yenye teknolojia ya kuweza kuchaji simu nyingine.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya Type-C 1.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Silver na Space Gray
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Nano-SIM / Electronic SIM card (Apple e-SIM), haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Face ID, accelerometer, gyro, proximity, barometer
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Ulinzi wa Face ID

Bei ya iPad Pro 12.9 (2018)

Kwa upande wa bei ya iPad Pro 12.9, yenyewe itaanzia dollar za marekani $1000 ambayo ni sawa na Tsh 2,300,000 hadi dollar za marekani $1,750 ambayo ni sawa na Tsh 4,100,000 kwa iPad Pro ya Inch 12.9 yenye ukubwa wa ndani wa TB 1.

Tablet zote hizi zitakuwa zinapatikana rasmi kuanzia November 7 lakini Kumbuka bei hizo zote ni kwa mujibu wa viwango vya kubadilisha fedha vya siku ya leo hivyo bei inaweza kuongezeka kutokana na kodi au kubadilika kwa viwango vya kubadilisha fedha. That’s it..guys hizi ndio sifa za iPad Pro 11 (2018) na iPad Pro 12.9 (2018) ambazo zimezinduliwa hapo siku ya jana.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use