Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Zifahamu kwa Undani Simu Mpya za Infinix Smart 3 na Smart 3 Plus

Hizi hapa ndio sifa pamoja na bei ya simu mpya za Infinix Smart 3 na Smart 3 Plus
Zifahamu kwa Undani Simu Mpya za Infinix Smart 3 na Smart 3 Plus Zifahamu kwa Undani Simu Mpya za Infinix Smart 3 na Smart 3 Plus

Kampuni ya Infinix ni moja kati ya kampuni zinazo zalisha simu nzuri na ambazo zinapatikana kwa bei rahisi, simu hizi nyingi zina sifa ambazo pengine unaweza kudhani kwamba simu hiyo ingeuzwa kwa bei ghali, lakini unakuta simu simu hiyo ni ya bei nafuu sana.

Infinix Smart 3 na Smart 3 Plus ni mfano wa simu hizo ambazo ni nzuri sana kwa muonekano na pia ni simu nzuri sana kwa sifa. Simu hizi zinakuja na sifa ambazo zinaweza kumtosha mtu yoyote mwenye mahitaji ya kuwa na smartphone bora, kama uniamini endelea kusoma makala hii.

Advertisement

Tukianza na Infinix Smart 3 Plus, simu hii inakuja na kioo chenye ukubwa wa inch 6.2 , kioo ambacho kimetengenzwa kwa teknolojia ya IPS LCD pamoja na resolution ya hadi pixel 720 x 1520. Kwenye kioo hicho kwa juu kuna ukingo wa juu ambao unajulikana kama water drop notch.

Zifahamu kwa Undani Simu Mpya za Infinix Smart 3 na Smart 3 Plus

Kama unavyoweza kuona kwenye picha hapo juu, ukingo huo maarufu kama water drop notch kuna kamera ya mbele yenye uwezo wa Megapixel 8, kamera ambayo inakuja na teknolojia ya AI ambayo inasaidia kufanya picha hizo kuonekana vizuri hasa kwenye mwanga mdogo.

Kwa nyuma Infinix Smart 3 Plus inakuja na kamera tatu ambazo zina Megapixel 13, Megapixel 2 pamoja na kamera nyingine ambayo ni QVGA. Kamera zote zinasaidiwa na teknolojia ya AI pamoja na flash mbili za LED ambazo kwa ujumla zinafanya simu hii kuwa bora kwenye upande wa picha.

Zifahamu kwa Undani Simu Mpya za Infinix Smart 3 na Smart 3 Plus

Smart 3 Plus inaendeshwa kwa processor ya Mediatek MT6761 Helio A22 ambayo inasaidiwa na RAM GB 2 au GB 3 pamoja na ukubwa wa ndani wa ROM wa kuchagua kati ya GB 16 au GB 32. Ukubwa huo unaweza kuongezwa kwa kutumia Memory card ya hadi GB 128. Sifa nyingine za Infinix Smart 3 Plus ni kama zifuatazo.

Sifa za Infinix Smart 3 Plus

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.21 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1560 pixels.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie) yenye mfumo wa OSX V5.0
  • Uwezo wa Processor – Quad-core 2.0 GHz Cortex-A53.
  • Aina ya Processor (Chipset) – Mediatek MT6761 Helio A22 (12 nm)
  • Uwezo wa GPU – PowerVR GE8320.
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu mbili moja inakuja na GB 16  na nyingine inakuja na GB 32, simu zote mbili zinakuja zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 128.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko simu mbili moja ina RAM ya GB 2 na nyingine inakuja na GB 3.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 13 yenye f/1.8, PDAF nyingine ikiwa na Megapixel 2 huku kamera ya mwisho ikiwa ni kamera ya QVGA. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya Dual-LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 3500 mAh.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2 na GPS ya A-GPS. USB ya micro USB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi nne za Midnight Black, Aqua Blue, Cosmic Purple na Bordeaux Red.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, proximity, compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G, 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).

Bei ya Infinix Smart 3 Plus

Kwa upande wa bei Infinix Smart 3 Plus inasemekana kuuzwa kwa kati ya Tsh 350,000 hadi Tsh 370,000 pamoja na kodi. Simu hii kwa sasa bado haipatikani nchini Tanzania.

Kwa upande wa Infinix Smart 3, yenyewe ni tofauti kidogo na Infinix Smart 3 Plus kwani inakuja na kioo ambacho ni kidogo zaidi na chenye ukingo mkubwa wa juu.

Zifahamu kwa Undani Simu Mpya za Infinix Smart 3 na Smart 3 Plus

Infinix Smart 3 inakuja na kioo cha inch 5.5 kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya IPS LCD, kama ilivyo Infinix Smart 3 Plus, Smart 3 inakuja na resolution ya hadi pixel 720 x 1520. Simu hii pia inakuja na kamera ya mbele ya Megapixel 8 huku ikiwa na flash ya LED.

Mbali na hayo Smart 3 inakuja na kamera mbili kwa nyuma, kamera moja ikiwa na Megapixel 13 na nyingine ikiwa na Megapixel 2, simu hii inasaidiwa na teknolojia ya AI kuweza kufanya picha ziwe na muonekano mzuri hasa wakati wa usiku.

Zifahamu kwa Undani Simu Mpya za Infinix Smart 3 na Smart 3 Plus

Sifa nyingine za ndani ni sawa na toleo la Plus, ila utofauti upo kwenye upande wa ukubwa wa ROM ambapo kwenye simu hii ni GB 16 na ukubwa wa RAM ambapo kwenye simu hii ni GB 2. Vilevile simu hii inakuja na mfumo mpya wa Android 9.0 (Pie) Go Edition. Sifa kamili za Infinix Smart 3 ni kama zifuatazo.

Sifa za Infinix Smart 3

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 5.5 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1560 pixels.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie) Go Edition yenye mfumo wa OSX V5.0
  • Uwezo wa Processor – Quad-core 2.0 GHz Cortex-A53.
  • Aina ya Processor (Chipset) – Mediatek MT6761 Helio A22 (12 nm)
  • Uwezo wa GPU – PowerVR GE8320.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 16 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 128.
  • Ukubwa wa RAM – GB 2.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 13 yenye f/1.8, PDAF nyingine ikiwa na Megapixel 2. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya Dual-LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 3050 mAh.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2 na GPS ya A-GPS. USB ya micro USB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi nne za Midnight Black, Aqua Blue, Cosmic Purple na Bordeaux Red.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, proximity, compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G, 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).

Bei ya Infinix Smart 3

Kwa mujibu wa infinix, simu ya Infinix Smart 3 tayari inapatikana hapa nchini Tanzania na unaweza kuipata kwa bei ya makadirio kuanzia shilingi za kitanzania 250,000 hadi Tsh 270,000 pamoja na kodi. Kumbuka bei hii inaweza kubadilika kati ya duka na duka.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use