Kampuni ya Inifnix hivi karibuni imezindua simu yake mpya ya Infinix Note 6 uko nchini Uganda, Simu hii ni toleo la Maboresho la simu ya Infinix Note 5 ambayo ilizinduliwa rasmi mwaka jana 2018.
Infinix Note 6 inakuja na muundo mpya tofauti na toleo lililopita huku ikiwa na sifa nzuri za kufanya watumiaji kufurahia simu hiyo mpya inayofanana kwa mbali na Galaxy Note 8.
Kama unavyoweza kuona Infinix Note 6 inakuja na kioo kikubwa cha Inch 6.01 kioo kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya FHD+ pamoja na Always-On AMOLED, kwenye kioo hicho kwa mbele kunakuja kamera ya Selfie ya Megapixel 16 yenye teknolojia AI.
Kwa nyuma Infinix Note 6 inakuja na kamera tatu zenye Megapixel 16, Megapixel 8 pamoja na kamera ya tatu ikiwa na Megapixel 2. Kamera zote zinakuja na teknolojia ya AI, HDR, Panorama pamoja na AR au Argument Realty ambayo inakupa uwezo wa kufanya mambo mbalimbali ikiwa pamoja na kuchukua vipimo mbalimbali vya urefu na upana kwa kutumia simu yako.
Mbali na hayo Infinix Note 6 inakuja na processor ya Mediatek MT6765 Helio P35 processor ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 4 pamoja na ukubwa wa ROM wa hadi GB 64, ukubwa huo unaweza kuongezwa kwa kutumia Memory card ya MicroSD Card ya hadi GB 500. Sifa nyingine za Infinix Note 6 ni kama zifuatazo.
TABLE OF CONTENTS
Sifa za Infinix Note 6
- Ukubwa wa Kioo – Inch 6.01 chenye teknolojia ya AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2340 pixels.
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie) yenye XOS V5.0
- Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.3 GHz Cortex-A53 & 4×1.8 GHz Cortex-A53)
- Aina ya Processor (Chipset) – Mediatek MT6765 Helio P35 (12 nm).
- Uwezo wa GPU – PowerVR GE8320.
- Ukubwa wa Ndani – GB 64 ikiwa na uwezo wa kuongezwa na memory card ya microSD ya hadi GB 500.
- Ukubwa wa RAM – GB 4.
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 16.
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 16, PDAF na kamera nyingine ikiwa na Megapixel 8 na kamera ya mwisho ikiwa na Megapixel 2, depth sensor. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya LED.
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 4000 mAh battery.
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, 4.2, A2DP, HD, LE
na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya micro USB 2.0, USB On-The-Go. - Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Midnight Black, Mocha Brown, Aqua Blue.
- Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Hybrid Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
- Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass.
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
- Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).
Bei ya Infinix Note 6
Kwa mujibu wa Infinix, Infinix Note 6 inapatikana sasa huko nchini Uganda kwa takribani shilingi ya uganda USh 740,000 ambayo ni sawa na takribani Shilingi za Tanzania Tsh 460,000 bila kodi. Kumbuka bei inaweza kubadilika pale simu hii itakapo zinduliwa hapa nchini Tanzania.