Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Zifahamu Hizi Hapa Sifa Pamoja na Bei ya Infinix Hot 8

Kampuni ya Infinix imezindua simu mpya ya Infinix Hot 7
Zifahamu Hizi Hapa Sifa Pamoja na Bei ya Infinix Hot 8 Zifahamu Hizi Hapa Sifa Pamoja na Bei ya Infinix Hot 8

Baada ya tetesi za muda kidogo, hatimaye hapo jana kampuni ya Infinix imetambulisha simu mpya ya Infinix Hot 8 huko nchini India. Simu hii ni toleo la maboresho ya simu ya Infinix Hot 7 ambayo ilizinduliwa mapema mwezi January mwaka huu 2019.

Simu hii mpya ya Infinix Hot 8 inakuja na sifa bora pamoja na muonekano mzuri tofauti kidogo na Hot 7. Kwa kuanza labda tuanze kwa kuangalia sifa za nje za simu hii, Infinix Hot 8 inakuja na kioo cha inch 6.52 kioo ambacho kimetengenezwa kwa teknolojia ya IPS LCD.

Advertisement

Zifahamu Hizi Hapa Sifa Pamoja na Bei ya Infinix Hot 8

Kioo hicho kwa juu kinakuja na kamera moja ya selfie yenye Megapixel 8 ambayo inakuja na teknolojia kama Face ID, HDR, AI Beauty huku ikiwa inasaidiwa na Flash ya LED Flash. Kwa nyuma simu hii inakuja na kamera tatu huku kamera kuu ikiwa na Megapixel 13 na nyingine mbili zikiwa na Megapixel 2 kwa kila moja.

Zifahamu Hizi Hapa Sifa Pamoja na Bei ya Infinix Hot 8

Kwa upande wa sifa za ndani Infinix Hot 8 inakuja ikiwa inaendeshwa na processor ya Mediatek MT6762 Helio P22, processor ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 4 pamoja na ukubwa wa ROM wa GB 64, ukubwa ambao unaweza kuongezwa kwa kutumia Memory Card ya hadi GB 256. Sifa nyingine za Infinix Hot 8 ni kama zifuatazo.

Zifahamu Hizi Hapa Sifa Pamoja na Bei ya Infinix Hot 8

Sifa za Infinix Hot 8

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.52 chenye teknolojia ya IPS LCD HD+ infinity display, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1520 pixels.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
  • Aina ya Processor (Chipset) – Mediatek MT6762 Helio P22 (12 nm).
  • Uwezo wa Processor (CPU) – Octa-core CPU (4×2.0 GHz Cortex-A53 and 4×1.5 GHz Cortex-A53).
  • Uwezo wa GPU – PowerVR GE8320
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili moja ikiwa na GB 32 na nyingine ikiwa na GB 64 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 256.
  • Ukubwa wa RAM – GB 3 au GB 4
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele –  Megapixel 8, yenye LED Flash.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko tatu moja ikiwa na Megapixel 13 na nyingine ikiwa na Megapixel 2 na nyingine pia ikiwa na Megapixel 2, zote zikiwa na uwezo wa phase detection autofocus, LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 5000 mAh Battery.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, 3.1, microUSB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Midnight Black, Cosmic Purple na Quetzal Cyan.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM2, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Aina za Sensor – Fingerprint scanner; Face recognition; Gyroscope; Proximity; e-Compass; Light; G-sensor.
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint  (Kwa Nyuma), Inayo ulinzi wa Face Unlock.

Bei ya Infinix Hot 8

Kwa mujibu wa tovuti ya Infinix, simu mpya ya Infinix Hot 8 inasemekana kuanza kupatikana kwa nchini India kuanzia tarehe 12 mwezi wa nane na inasemekana itakuwa inapatikana kwa bei ya rupee ya india INR 6,999 ambayo ni sawa na shilingi za Tanzania Tsh 225,000 bila kodi. Hata hivyo simu hii inategemea kuongezwa bei kuanzia mwezi wa kumi na kuuzwa ka rupee ya india INR 7,999 ambayo ni sawa na shilingi za Tanzania Tsh 256,000 bila kodi. Kwa Tanzania bei hii inaweza kupanda.

16 comments
  1. Hot 8 yangu ina mwezi nanusu ina 32gb lakini ina tatizo la kustack alaf inajichora mistari alafu inajizima na kujiwasha inafanya hivyo kwa muda inakaa sawa.Tatizo lilianza simu ilipo timiza mwezi.Hapo tatizo litakua nikitu gani.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use