Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Sifa na Bei ya Infinix Hot 6, Hot 6 Pro Pamoja na Hot 6 Lite

Zifahamu hizi hapa simu mpya za Infinix Hot 6
Sifa na Bei za Infinix-Hot-6 Sifa na Bei za Infinix-Hot-6

Simu mpya za Infinix Hot 6 na Hot 6 lite ni simu mpya ambazo ni maboresho ya simu za Infinix Hot 5 pamoja na Infinix Hot 5 Lite simu ambazo zilitoka rasmi mwezi wa nane mwaka jana 2017, Lakini tofauti na matoleo hayo ya Infinix Hot 5, Infinix Hot 6 inakuja na toleo jipya la tatu ambalo ni Infinix Hot 6 Pro. Kwa upande wa muundo simu hizi za Infinix Hot 6, Infinix Hot 6 Pro na Hot 6 lite zinakuja na muundo wa tofauti kidogo na matoleo ya mwaka jana ya infinix Hot 5.

Tukianza na Simu ya Infinix Hot 6 Pro simu hii inakuja na kioo cha TFT HD+ infinity display chenye resolution ya 1440 x 720 pixels. Hot 6 Pro inakuja na kamera mbili kwa nyuma kamera moja ikiwa na uwezo wa megapixel 13 na nyingine inayo megapixel 2.

Advertisement

Mbali na hayo kitu kikubwa zaidi kwenye simu hii ya infinix hot 6 pro ni pamoja na kuwa na processor ya Qualcomm Snapdragon 425 Octa-core CPU, pamoja na GPU ya Adreno 308, hii ni hatua kubwa sana kwa simu za infinix kuanza kutumia processor za Qualcomm Snapdragon kwani tunajua mara zote simu za Infinix na Tecno zimekuwa zikitegemea processor za Mediatek. Anyway.. sifa nyingine za Infinix Hot 6 Pro ni kama zifuatazo.

Sifa za Infinix Hot 6 Pro

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6 chenye teknolojia ya TFT HD+ infinity display, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1720 x 1440 pixels (~272 ppi pixel density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Quad-core 1.4GHz Cortex-A53, Qualcomm Snapdragon 425 Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Adreno 308
  • Ukubwa wa Ndani – GB 32 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 128.
  • Ukubwa wa RAM – GB 3
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele –  Megapixel 5, yenye f/2.0, LED Flash.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko mbili moja ikiwa na Megapixel 13 na nyingine ikiwa na Megapixel 2 huku zote zikiwa na uwezo wa phase detection autofocus, LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 4000 mAh Battery.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, 3.1, microUSB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi nne za Black, Blue, Gold na Red.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint  (Kwa Nyuma), Inayo ulinzi wa Face Unlock.

Kwa upande wa Infinix Hot 6 yenye inakuja na kioo cha inch 6, processor ya Octa-core 1.4 GHz Cortex-A53 Qualcomm Snapdragon 425 pamoja na GPU ya Adreno 308. Sifa nyingine za Infinix Hot 6 ni kama zifuatazo.

Sifa za Infinix Hot 6

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6 chenye teknolojia ya TFT HD+ infinity display, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1440 pixels (~272 ppi pixel density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core 1.4 GHz Cortex-A53, Qualcomm Snapdragon 425 Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Adreno 308
  • Ukubwa wa Ndani – GB 16 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 128.
  • Ukubwa wa RAM – GB 2
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele –  Megapixel 5, yenye f/2.0, LED Flash.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko mbili moja ikiwa na Megapixel 13 na nyingine ikiwa na Megapixel 2 huku zote zikiwa na uwezo wa phase detection autofocus, LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 4000 mAh Battery.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, 3.1, microUSB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi nne za Black, Blue, Gold na Red.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint  (Kwa Nyuma), Inayo ulinzi wa Face Unlock.

Simu ya Infinix Hot 6 Lite ni toleo la bei nafuu la simu za Infinix Hot 6, simu hii inakuja na sifa sawa na Infinix Hot 6 lakini tofauti kubwa iko kwenye RAM, kwani simu hii ya Infinix Hot 6 Lite inakuja na RAM ya GB 1 na bila shaka simu hii inakuja na mfumo wa Android GO. Sifa nyingine za Hot 6 Lite ni kama zifuatazo.

Sifa za Infinix Hot 6 Lite

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6 chenye teknolojia ya TFT HD+ infinity display, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1440 pixels (~272 ppi pixel density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android GO 8.1 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core 1.4 GHz Cortex-A53, Qualcomm Snapdragon 425 Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Adreno 308
  • Ukubwa wa Ndani – GB 16 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 128.
  • Ukubwa wa RAM – GB 1
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele –  Megapixel 5, yenye f/2.0, LED Flash.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko mbili moja ikiwa na Megapixel 13 na nyingine ikiwa na Megapixel 2 huku zote zikiwa na uwezo wa phase detection autofocus, LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 4000 mAh Battery.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, 3.1, microUSB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi nne za Black, Blue, Gold na Red.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint  (Kwa Nyuma), Inayo ulinzi wa Face Unlock.

Bei ya Infinix Hot 6 Pro, Infinix Hot 6 na Infinix Hot 6 Lite

Kwa upande wa bei ya simu hizi, Infinix Hot 6 Pro inakadiriwa kuja kwa bei ya Tsh 360,000 huku Infinix Hot 6 inakadiriwa kuja kwa bei ya Tsh 310,000. Wakati simu ya Infinix Hot 6 Lite yenyewe inakadiriwa kuja kwa bei ya Tsh 240,000. Kumbuka bei inaweza kubadilika kwa Tanzania.

Je wewe unaonaje kuhusu simu hizi mpya za Infinix Hot 6 Pro, Infinix Hot 6 na Infinix Hot 6 Lite, je ni simu gani ungependa kuwa nayo mwaka huu, tuambie kwenye maoni hapo chini.

9 comments
  1. Nahitaji hiyo infix hot 6 nipo hapa Iringa Je! Nita ipataje??? Na Bei ya mwisho ni shilingi ngapi??

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *