Kampuni ya Huawei bado inaendelea na mpango wake wa kuzindua simu zake mpya za Android japo kuwa inapitia wakati mgumu kibiashara. Siku za karibuni kampuni ya Huawei ili tangaza kupungua kwa mauzo ya simu zake kwa baadhi ya nchi kwa asilimia 40 hadi 60.
Japo kuwa Huawei inapitia wakati mgumu bado hii haija zuia kampuni hiyo kutangaza ujio wa simu zake mpya za Huawei Nova 5, Nova 5 Pro pamoja na Nova 5i. Kwa mwaka huu kitu kikubwa kwenye simu hizi ni pamoja na processor ya Kirin 980 kutoka Huawei, processor ambayo kwa mara ya kwanza ilitumika kwenye simu mpya za Huawei P30 na P30 Pro.
Mbali na processor kitu kingine kikubwa kwenye simu hizi ni pamoja na kamera ambapo kwa mbele simu hizi zote zinakuja na kamera ya Megapixel 32, huku kwa nyuma simu hizi zikiwa zinakuja na kamera nne kila moja.
Tukianza na Huawei Nova 5, yenyewe inakuja na kamera nne kwa nyuma huku kamera kubwa ikiwa na Megapixel 48, nyingine ikiwa na Megapixel 12 na nyingine mbili za mwisho zote zikiwa na Megapixel 2 kila moja. Nova 5 Pro nayo inakuja na kamera zinazo fanana na Huawei Nova 5.
Kama ilivyo kwenye kamera, Huawei Nova 5 na Nova 5 Pro zote zinakuja na sifa zinazo karibia kufanana, kama vile zote zinakuja na kioo cha OLED chenye inch 6.39 kioo ambacho kinakuja na resolution ya hadi pixel 1080 x 2340. Simu zote pia zinakuja na uzito sawa pamoja na muundo unaofanana. Kitu kikubwa cha tofauti kwenye simu hizi ni processor kwani Huawei Nova 5 Pro inakuja na processor ya Kirin 980, wakati Nova 5 yenyewe inakuja na processor ya Kirin 810.
Kwa upande wa Nova 5i yenyewe ndio simu ya bei nafuu zaidi kwenye simu hizi hivyo inakuja na sifa za chini kidogo. Simu hii inakuja na kamera nne kwenye nyuma ambazo zinakuja na uwezo wa Megapixel 24, Megapixel 8 huku kamera mbili za mwisho zikiwa na Megapixel 2 kila moja.
Kwa upande wa muundo Nova 5i inakuja na kioo cha inch 6.4 chenye resolution ya hadi pixel 1080 x 2310, kioo ambacho pia kimetengenezwa kwa teknolojia ya IPS LCD. Mbali na kioo simu hii inakuja na kamera ya mbele ya Megapixel 24 ambayo iko kwa pembeni, tofauti na simu za Huawei Nova 5 na Nova 5 Pro, Sifa nyingine za simu hizi ni kama zifuatazo.
TABLE OF CONTENTS
Sifa za Huawei Nova 5
- Ukubwa wa Kioo – Inch 6.39 chenye teknolojia ya OLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2340 pixels.
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
- Uwezo wa Processor – Octa-core (2×2.6 GHz Cortex-A76 & 2×1.92 GHz Cortex-A76 & 4×1.8 GHz Cortex-A55).
- Aina ya Processor (Chipset) – HiSilicon Kirin 810 (7 nm).
- Uwezo wa GPU – Mali-G52 MP6.
- Ukubwa wa Ndani – GB 128 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card ya NM (Nano Memory), ya hadi GB 256.
- Ukubwa wa RAM – GB 8.
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 32 yenye f/2.0, HDR pamoja na uwezo wa kuchukua video za 1080p@30.
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera nne kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 48 yenye f/1.8, 27mm (wide), 1/1.7″, PDAF/Laser AF na nyingine ikiwa na Megapixel 16 yenye f/2.2, 17mm (ultrawide), na kamera za mwisho zikiwa na Megapixel 2 ambayo ni f/2.4, 27mm (wide) dedicated macro camera, na nyingine ikiwa Megapixel 2 ambayo ni f/2.4, depth sensor. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya LED.
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 3500 mAh battery yenye teknolojia ya Fast Charging.
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, 5.0, A2DP, aptX HD, LE
na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya 3.1, Type-C 1.0 reversible connector. - Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Black, Purple na Green.
- Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Hybrid Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
- Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass.
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
- Ulinzi – Inayo Fingerprint (Chini ya Kioo).
Bei ya Huawei Nova 5
Kwa upande wa bei Nova 5 inategemea kuingia sokoni hivi karibuni na itakuwa inapatikana kwanza kwa nchini China kwa yuan ya china CNY2,999 ambayo ni sawa na takribani shilingi za kitanzania Tsh 1,005,000 bila kodi.
Sifa za Huawei Nova 5 Pro
- Ukubwa wa Kioo – Inch 6.39 chenye teknolojia ya OLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2340 pixels.
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
- Uwezo wa Processor – Octa-core (2×2.6 GHz Cortex-A76 & 2×1.92 GHz Cortex-A76 & 4×1.8 GHz Cortex-A55).
- Aina ya Processor (Chipset) – HiSilicon Kirin 980 (7 nm).
- Uwezo wa GPU – Mali-G76 MP10.
- Ukubwa wa Ndani – Ziko simu mbili moja ikiwa na GB 128 na nyingine ikiwa na GB 256 zote zikiwa na uwezo wa kuongezwa na memory card ya NM (Nano Memory), ya hadi GB 256.
- Ukubwa wa RAM – GB 8.
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 32 yenye f/2.0, HDR pamoja na uwezo wa kuchukua video za 1080p@30.
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera nne kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 48 yenye f/1.8, 27mm (wide), 1/1.7″, PDAF/Laser AF na nyingine ikiwa na Megapixel 16 yenye f/2.2, 17mm (ultrawide), na kamera za mwisho zikiwa na Megapixel 2 ambayo ni f/2.4, 27mm (wide) dedicated macro camera, na nyingine ikiwa Megapixel 2 ambayo ni f/2.4, depth sensor. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya LED.
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 3500 mAh battery yenye teknolojia ya Fast Charging.
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, 5.0, A2DP, aptX HD, LE
na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya 3.1, Type-C 1.0 reversible connector. - Rangi – Inakuja kwa rangi nne za Black, Purple, Green na Orange.
- Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Hybrid Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
- Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass.
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
- Ulinzi – Inayo Fingerprint (Chini ya Kioo).
Bei ya Huawei Nova 5 Pro
Kwa upande wa bei kama ilivyo Nova 5, Nova 5 Pro inatajiwa kutoka siku za karibuni kwa nchini china, huku bei yake ikitarajiwa kuanzia Yuan ya China CNY2,999 ambayo ni sawa na Tsh 1,005,000 bila kodi kwa toleo lenye GB 128. Huku toleo lenye GB 256 likiuzwa kwa Yuan CNY3,399 ambayo ni sawa na takribani Tsh 1,139,000 bila kodi.
Sifa za Huawei Nova 5i
- Ukubwa wa Kioo – Inch 6.4 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2310 pixels.
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
- Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.2 GHz Cortex-A73 & 4×1.7 GHz Cortex-A53).
- Aina ya Processor (Chipset) – Hisilicon Kirin 710F (12 nm).
- Uwezo wa GPU – Mali-G51 MP4.
- Ukubwa wa Ndani – GB 128 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card ya MicroSD Card ya hadi GB 256.
- Ukubwa wa RAM – Ziko simu mbili moja ikiwa na GB 6 na nyingine ikiwa na GB 8.
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 24 yenye f/1.8, 27mm (wide), PDAF pamoja na uwezo wa kuchukua video za 1080p@30.
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera nne kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 24 yenye f/1.8, 27mm (wide), 1/1.7″, PDAF/Laser AF na nyingine ikiwa na Megapixel 8 yenye f/2.2, 17mm (ultrawide), na kamera za mwisho zikiwa na Megapixel 2 ambayo ni f/2.4, 27mm (wide), na nyingine ikiwa Megapixel 2 ambayo ni f/2.4, depth sensor. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya LED.
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 4000 mAh battery yenye teknolojia ya Fast Charging.
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, 5.0, A2DP, aptX HD, LE
na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya 3.1, Type-C 1.0 reversible connector. - Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Black, Gradient Blue na Red.
- Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Hybrid Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
- Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass.
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
- Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).
Bei ya Huawei Nova 5i
Kwa upande wa Bei Nova 5i inatarajiwa kuingia sokoni hivi karibuni kwa nchini china, huku bei yake ikiwa inatarajiwa kuwa takribani Yuan CNY2,199 ambayo ni sawa na Tsh za kitanzania 737,000 bila kodi. Kumbuka bei za simu hizi zinaweza kubadilika kutoka na viwango vya kubadilisha fedha pamoja na kodi.
mega pix 2 unapigaje picha si uwezo wake mdogo au inatumika kwa picha zipi
Hizo zinasaidiana na hiyo kamera kubwa na zote kwa pamoja zinaweza kutoa picha bora zaidi.