Huawei Yazindua Simu Mpya ya Huawei Y7 Pro (2019)

Toleo la bei rahisi la simu ya Huawei P Smart (2019)
hizi hapa sifa na bei ya Huawei Y7 Pro (2019) hizi hapa sifa na bei ya Huawei Y7 Pro (2019)

Kampuni ya Huawei bado inaendelea na harakati za kuwa kampuni kubwa zaidi kwa kuuza simu nyingi zaidi kwa mwaka 2018 – 2019. Kwa mujibu wa ripoti za hivi karibuni, kampuni ya Huawei imeipita kampuni ya Apple kwa mauzo ya Smartphone kwa mwaka 2018 kwa zaidi ya Asilimia 10.

Mpaka sasa ni wazi juhidi hizi za Huawei haziji bure bali ni kwa kutoa simu mpya kila siku kwani siku tatu zilizo pita kampuni ya Huawei ilizindua simu mpya ya Huawei P Smart (2019), na hivi leo kampuni hiyo imerudi tena na simu mpya nyingine ya Huawei Y7 Pro (2019). Simu hizi zinaonekana kufanana kwa sura lakini utofauti upo zaidi kwenye upande wa sifa.

Advertisement

Huawei Yazindua Simu Mpya ya Huawei Y7 Pro (2019)

Huawei Y7 Pro inakuja na kioo cha inch 6.26, kioo ambacho kina uwiano wa 19:9. Simu hii inaonekana kuendeshwa na processor ya Qualcomm Snapdragon 450 ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 3 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 32, ukubwa unaoweza kuongezewa na memory card ya hadi GB 512. Sifa nyingine za Huawei Y7 Pro (2019) ni kama zifuatazo.

Sifa za Huawei Y7 Pro (2019)

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.26 chenye teknolojia ya IPS LCD, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resoluti ya 1080 x 2340 pixels (~415 ppi density)
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
  • Uwezo wa Processor – 1.8GHz Octa Core.
  • Aina ya Processor – Snapdragon 450 14nm.
  • Uwezo wa GPU – Adreno 506.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 32 yenye uwezo wa kuongezewa na memory card hadi GB 512.
  • Ukubwa wa RAM – GB 3.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 16 yenye (HDR, 1080p) pamoja na teknolojia ya autofocus.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko mbili moja ikiwa na Megapixel 13 (f/1.8) na Kamera nyingine inayo Megapixel 2 ambayo hii ni depth sensor. Kamera zote zinasaidiwa na Flash ya LED Flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Non-removable Li-Po 4000 mAh.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, microUSB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Blue na Black.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Accelerometer, proximity na compass
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
  • Ulinzi – Haina Fingerprint.

hizi hapa sifa na bei ya Huawei Y7 Pro (2019)

Bei ya Huawei Y7 Pro (2019)

Kwa upande wa bei Huawei Y7 Pro (2019), inatarajiwa kuuzwa kwa dollar za marekani $170 ambayo ni sawa na Shilingi za Tanzania Tsh 392,000 bila kodi ambayo ni sawa na takribani shilingi za Kenya Ksh 17,400 bila kodi. Simu hii inasemekana kuuzwa mtandaoni na inatarajiwa kuingia sokoni rasmi kuanzia tarehe 5 ya mwezi wa kwanza 2019.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use