Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Huawei Yazindua Simu Mpya ya Huawei Y5 Prime (2018)

Ifahamu simu mpya ya Huawei Y5 Prime (2018)
Huawei Y5 Prime (2018) Huawei Y5 Prime (2018)
Simu Mpya ya Huawei Y5 Prime (2018)

Hivi karibuni imekuwa ni utaratibu wa kawaida kwa kampuni mbalimbali za simu kuzindua simu janja kimya kimya bila kutoa taarifa au kufanya event za uzinduzi wa simu husika. Hayo yametokea hivi karibuni ambapo kampuni ya Huawei imezindua simu mpya ya Huawei Y5 Prime (2018) kimya kimya bila kutoa taarifa kwa wateja wake.

Japokuwa hakuna kikubwa sana cha kuongelea kuhusu simu hii mpya ya Huawei Y5 Prime (2018), lakini kwa sababu Tanzania Tech hatutaki upitwe na habari yoyote ya teknolojia basi hizi hapa ndio sifa za Huawei Y5 Prime (2018).

Advertisement

Sifa za Huawei Y5 Prime (2018)

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 5.45 chenye teknolojia ya IPS LCD display, chenye uwezo wa kuonyesha rangi milioni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1440 pixels, 19:9 ratio (~295 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa core, 1.5 GHz, Cortex A53, MediaTek MT6739 Chipset.
  • Uwezo wa GPU – PowerVR GE8100
  • Ukubwa wa Ndani – GB 16 yenye uwezo wa kuongezewa na Memory card ya GB 128.
  • Ukubwa wa RAM – GB 2
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 5
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 13 yenye Continuous Shooting, High Dynamic Range mode (HDR), Autofocus, LED Flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-ion 3020 mAh.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP, LE, aptX HD pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS, MicroUSB 2.0
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Black, Blue na Gold.
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
  • Ulinzi – Face Unlock (Haina Fingerprint).

Bei ya Huawei Y5 Prime (2018)

Kuhusu bei bado kampuni ya Huawei haijatangaza bei rasmi ya simu hizi, kwa mujibu wa wa tovuti ya GSM Arena huenda simu hii ikauzwa bei rahisi kutokana na uwezo na sifa zake. endelea kutembelea Tanzania Tech tutakujulisha pindi tutakapo pata bei ya simu hii.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use