Huawei Y3 ni moja kati ya simu zilizo tumika sana hapa Tanzania na Afrika kwa ujumla, Sasa kuliona hilo kampuni ya Huawei imetangaza kurudi na toleo jipya la simu hiyo ya Huawei Y3 (2018) ambayo sasa itakuja ikiwa inatumia mfumo wa uendeshaji wa Android Go.
Kama tunavyojua, mfumo wa Android Go ni maalum kwaajili ya simu za bei nafuu zenye uwezo mdogo wa RAM kuanzia GB 1 na kutoka na uwezo wake simu hizi mara nyingi huwa zinauzwa kwa bei nafuu zaidi kuliko zile zenye mfumo wa Android wa Kawaida.
Sasa katika kuhakikisha kuwa simu hizi zinawafikia watu wa kipato cha chini, Huawei Y3 (2018) imelenga zaidi soko la Afrika na kwa mujibu wa tovuti ya gizmochina, simu hii ita-anza kupatikana kwanza huko nchini Zambia.
Kwa mujibu wa tovuti hiyo, simu hiyo imeonekana kwenye tovuti ya Huawei ya nchini Zambia huku ikionyesha sifa za simu hiyo pamoja na picha halisi za simu hiyo Kama zinavyo onekana hapao chini.
Sifa za Huawei Y3 (2018)
- Ukubwa wa Kioo – Inch 5 chenye teknolojia ya IPS display, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 854 x 480 pixels, 16:9 ratio
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.0 (Oreo Go)
- Uwezo wa Processor – Quad-core Quad-core 1.1 GHz Cortex-A53, MediaTek MT6737 Chipest.
- Uwezo wa GPU – Mali-T720MP2
- Ukubwa wa Ndani – GB 8 yenye uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 256.
- Ukubwa wa RAM – GB 1
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 2 yenye Fix Focus.
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 8 yenye Auto Focus pamoja na single LED Flash.
- Uwezo wa Battery – Battery ya Li-Ion 2,280 mAh battery
- Viunganishi – Wi-Fi 802.1, hotspot, Bletuooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS.
- Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za White, Grey na Gold
- Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM
, inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack. - Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
- Ulinzi – Haina Fingerprint
Kuhusu bei bado kampuni ya Huawei hawaja tangaza bei ya simu hii lakini tegemea kuipata simu hii kwa makadirio ya shilingi za kitanzania Tsh 350,000 hadi Tsh 250,000. Endelea kutembelea Tanzania Tech tutakujuza zaidi kuhusu simu hii pamoja na bei yake halisi itakapo tangazwa.