Huawei Yazindua Simu Mpya ya Nova 4 Yenye Kamera ya 48 MP

Hizi hapa ndio sifa pamoja na bei ya Huawei Nova 4 (2018)
Sifa na bei ya Huawei Nova 4 Sifa na bei ya Huawei Nova 4

Kampuni ya Huawei hivi leo imetangaza ujio wa simu yake mpya ya Huawei Nova 4. Simu hii mpya inakuja na sifa nzuri sana huku ikiwa na kamera ya selfie ya Megapixel 25 na kwa nyuma ikiwa na kamera tatu kwa nyuma huku kamera hizo zikiwa na Megapixel 48, Megapixel 16 na nyingine ikiwa ni Megapixel 2.

Lipo toleo lingine la Huawei nova 4 ambalo linakuja na kamera ya nyuma ya Megapixel 20 na sifa nyingine zikiwa kama matoleo yote ya simu hiyo.

Advertisement

Kioo cha Huawei nova 4 kinakuja na ukubwa wa inch 6.4 huku kwa pembeni kikiwa kime tobolewa kwa ajili ya kamera ya mbele Kama ilivyo simu mpya ya Galaxy A8s. Kioo hicho kimetengenezwa kwa teknolojia ya IPS LCD ambacho pia kina resolution ya 2310×1080 pixel. Simu hii inaendeshwa na processor ya Kirin 970 chipset ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 4 pamoja na ukubwa wa ndani hadi GB 128. Sifa nyingine za Huawei nova 4 ni kama zifuatazo.

Sifa za Huawei Nova 4

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.4 chenye teknolojia ya IPS LCD, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resoluti ya 1080 x 2310 pixels (~398 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.4 GHz Cortex-A73 & 4×1.8 GHz Cortex-A53)
  • Aina ya Processor – Hisilicon Kirin 970 (10 nm)
  • Uwezo wa GPU – Mali-G72 MP12
  • Ukubwa wa Ndani – GB 128 yenye uwezo wa kuongezewa na memory card hadi GB 512.
  • Ukubwa wa RAM – RAM ya GB 8
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 25 yenye (f/2.0, 1080p) pamoja na teknolojia ya autofocus.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko tatu moja ikiwa na Megapixel 48 (f/1.8 PDAF), Nyingine ikiwa na Megapixel 16 yenye f/2.2, PDAF na Kamera nyingine ikiwa na Megapixel 2 ambayo hii ni depth sensor. Kamera zote zinasaidiwa na Flash ya LED Flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Non-removable Li-Ion 3750 mAh yenye teknolojia ya Fast battery charging 9V/2A 18W.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, microUSB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi nne za Aurora Blue, Red, White na Black.
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Fingerprint, accelerometer, proximity, compass
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa nyuma).

Bei ya Huawei Nova 4

Kwa upande wa bei, Nova 4 yenye kamera ya Megapixel 43 inatarajiwa kuzinduliwa huko nchini China na kuuzwa kwa Yuan ya China CNY 3,400  ambayo ni sawa na Shilingi za Tanzania Tsh 1,134,000 bila kodi, sawa na Shilingi za Kenya Ksh 50,600 bila kodi.

Kwa mujibu wa Huawei, Toleo lingine lenye kamera ya Megapixel 20 litauzwa kwa Yuan CNY 3,100 ambayo ni sawa na Tsh 1,034,000 bila kodi ambayo ni sawa na Shilingi za Kenya Ksh 47,000 bila kodi. Kumbuka bei zinaweza kubadilika kutokana na kodi pamoja na kupanda au kushuka kwa viwango vya kubadilisha fedha.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use