Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Kampuni ya Huawei Yazindua Simu Mpya ya Huawei Mate Xs

Simu hii inakuja na tofauti kidogo sana na simu ya mwaka jana 2019
Kampuni ya Huawei Yazindua Simu Mpya ya Huawei Mate Xs Kampuni ya Huawei Yazindua Simu Mpya ya Huawei Mate Xs

Kupitia mkutano wa MWC mwaka 2019, kampuni ya Huawei ilitangaza kwa mara ya kwanza simu yake mpya inayojikunja ya Huawei Mate X, kutokana na kuahirishwa kwa mkutano wa MWC mwaka huu 2020 kutokana na virusi vya corona, kampuni ya Huawei imetangaza leo imetangaza simu yako mpya ya Huawei Mate Xs bila kuwepo kwa mkutano maalum.

Simu hiyo mpya ya Huawei Mate Xs, inakuja na maboresho mapya huku ikiwa na muundo unao fanana na toleo la mwaka jana 2019 la Huawei Mate X. Tukianza na upande wa kioo, simu hii inakuja na kioo cha inch 8.0 ikiwa imefunuliwa huku ikiwa na kioo cha inch 6.6 ikiwa imefungwa, hata hivyo kioo hicho bado kinakuja kikiwa kimetengenezwa kwa teknolojia ya OLED.

Advertisement

Kampuni ya Huawei Yazindua Simu Mpya ya Huawei Mate Xs

Huawei Mate Xs inakuja na kamera nne huku kamera kuu ikiwa na Megapixel 40, huku kamera nyingine tatu zikiwa na Megapixel 8, Megapixel 16 na kamera ya mwisho ikiwa ni TOF 3D (depth). Kamera zote kwa pamoja zinakuja na uwezo wa kuchukua video za hadi 4K sawa na kusema simu hii inakuja na uwezo wa kuchukua video za hadi 2160p@30fps. Huawei Mate Xs haina kamera ya mbele kwani kamera inayotumika kwa nyuma ndio hiyo hiyo inayotumika kwa mbele.

Kwa upande wa sifa za ndani Huawei Mate Xs inakuja na processor ya HiSilicon Kirin 990 5G (7 nm+) yenye uwezo wa speed ya Octa-core (2×2.86 GHz Cortex-A76 & 2×2.36 GHz Cortex-A76 & 4×1.95 GHz Cortex-A55). Processor hiyo inasaidiwa na RAM ya GB 8 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 512, ukubwa huo unaweza kuongezwa na Memory Card ya Nano Memory card ya hadi GB 256GB. Sifa nyingine za Huawei Mate Xs ni kama zifuatazo.

Sifa za Huawei Mate Xs

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 8 ikiwa Tablet na Inch 6.6 ikiwa kama simu ya kawaida, kioo cha simu hii kina teknolojia ya OLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16, pamoja na resolution ya 2480 x 2200 pixels ikiwa tablet na 2480 x 892 ikiwa simu ya kawaida.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 10.0 yenye mfumo wa EMUI 10.0
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (2×2.86 GHz Cortex-A76 & 2×2.36 GHz Cortex-A76 & 4×1.95 GHz Cortex-A55).
  • Aina ya Processor (Chipset) – HiSilicon Kirin 990 5G (7 nm+).
  • Uwezo wa GPU – Mali-G76 MP16.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 512 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na NM card hadi ya GB 256.
  • Ukubwa wa RAM – GB 8.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Haina kamera ya mbele.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera nne moja ikiwa na Megapixel 40 (Wide Angle Lens), nyingine ina Megapixel 8 (Ultra Wide Angle Lens), Megapixel 16 (Telephoto) na ya mwisho ni TOF 3D, (depth). Kamera zote ni kamera za Leica.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 4500 mAh.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE na GPS ya A-GPS, GLONASS na USB 2.0, Type-C 1.0 reversible connector; USB Host.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi moja ya Interstellar Blue.
  • Mengineyo – Haina Radio FM, inatumia laini moja, Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Gravity Sensor, Ambient Light Sensor, Proximity Sensor, Gyroscope, Compass, Fingerprint Sensor, Hall sensor, Barometer, Infrared sensor, colour temperature sensor.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G, 4G na 5G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa pembeni).

Kampuni ya Huawei Yazindua Simu Mpya ya Huawei Mate Xs Kampuni ya Huawei Yazindua Simu Mpya ya Huawei Mate Xs

Bei ya Huawei Mate Xs

Kwa mujibu wa tovuti ya Huawei, Mate Xs inategemewa kuanza kupatikana kuanzia mwezi wa tatu mwaka huu 2020, huku ikitegemewa kwafikia wateja wote wa Huawei dunia nzima. Bei ya Mate Xs inategemewa kuanzia Euro €2,499 ambayo ni sawa na takribani Shilingi za Kitanzania TZS 6,265,000 bila kodi. Kumbuka kwa Tanzania bei hii inaweza kuongezeka.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use