Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya Huawei Mate 30 na Mate 30 Pro

Kampuni ya Huawei imezindua simu mpya za Huawei zisizo na Apps za Google
Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya Huawei Mate 30 na Mate 30 Pro Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya Huawei Mate 30 na Mate 30 Pro

Baada ya tetesi na subira ya muda mrefu hatimaye hivi leo kampuni ya Huawei imatangaza ujio wa simu zake mpya za Huawei Mate 30 na Huawei Mate 30 Pro. Kama ilivyo tarajiwa, simu hizi zote zinakuja bila huduma yoyote ya Google ikiwa pamoja na soko la Play Store pamoja na huduma nyigine ambazo zimezoeleka kutoka Google.

Huawei Mate 30

Tukianza na upande wa sifa, Huawei Mate 30 inakuja na kioo cha inch 6.62 kioo ambacho kime tengenezwa kwa teknolojia ya OLED pamoja na uwezo wa resolution hadi pixel 1080 kwa 2340. Chini ya kioo hicho kuna sensor ya Fingerprint ambayo inasaidia simu hii kufunguka kwa haraka kwa kutumia alama za vidole.

Advertisement

Mbali na hayo, kwa mbele simu hii inakuja na kamera ya Megapixel 24 yenye uwezo wa kuchukua video za hadi 1080p@30, huku ikisaidiwa na teknolojia ya HDR kwa ajili ya kufanya picha zako za selfie kuwa na rangi nzuri na mwanga bora zaidi.

Kwa nyuma Huawei Mate 30 inakuja na kamera tatu, kamera kuu ikiwa inakuja na Megapixel 40 na nyingine mbili zikiwa AQZwna Megapixel 8 pamoja na Megapixel 16. Kamera zote kwa pamoja zinakuja na uwezo wa kuchukua video za hadi 4k, hii ikiwa ni sawa na kusema kamera hizo zinakuja na uwezo wa 2160p@30/60fps, 1080p@30/60/120fps, pamoja na 720p@960fps, gyro-EIS.

Mbali na hayo, Huawei Mate 30 inakuja ikiwa inaendeshwa na processor ya HiSilicon Kirin 990 (7 nm+), processor ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 6 au GB 8 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 128. Simu hii inaweza kuongezewa ukubwa wa ndani kwa kutumia Nano Memory card ya hadi GB 256. Sifa nyingine za Huawei Mate 30 ni kama zifuatazo.

Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya Huawei Mate 30 na Mate 30 Pro

Sifa za Huawei Mate 30

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.62 chenye teknolojia ya OLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2340 pixels, na uwiano wa 18.7:9 ratio (~389 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 10 yenye mfumo wa Huawei EMUI 10
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (2×2.86 GHz Cortex-A76 & 2×2.09 GHz Cortex-A76 & 4×1.86 GHz Cortex-A55)
  • Aina ya Processor (Chipset) – HiSilicon Kirin 990 (7 nm+) Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Mali-G76 MP16.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 128 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na nano card hadi ya GB 256.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko simu za aina mbili moja inakuja na RAM ya GB 6 na nyingine inakuja na RAM ya GB 8.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 24 yenye HDR na uwezo wa 4K
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 40 yenye f/1.8, 27mm, 1/2.3″ na nyingine ikiwa na Megapixel 16 yenye f/2.2, 17mm (wide lens), na nyingine inakuja na Megapixel 8 yenye f/2.4, 52mm (telephoto lens). Huku zote zikiwa zinasadiwa na Leica optics, panorama, HDR, 4K pamoja na flash ya dual-LED dual-tone flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 4200mAh battery yenye teknolojia ya Fast battery charging yenye uwezo wa kuchaji asilimia 58 kwa nusu saa.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS. USB 3.1, Type-C 1.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi nne za Black, Space Silver, Cosmic Purple, Emerald Green.
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack. Inakuja na teknolojia ya kuzia maji na vumbi.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Face ID, fingerprint (under display, optical), accelerometer, gyro, proximity, barometer, compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G, 4G na 5G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Chini ya Kioo).

Bei ya Huawei Mate 30

Kwa upande wa bei, Huawei Mate 30 Pro inategemea kuanza kuuzwa hivi leo huko nchini china, na baadaye mwezi October simu hii inategemea kupatikana kwa Euro €800, ambayo ni sawa na shilingi za Tanzania TZS 2,031,000 bila kodi.

Huawei Mate 30 Pro

Kwa upande wa Mate 30 Pro, simu hii inakuja na kioo cha kisasa cha inch 6.53 kioo ambacho kime tengenezwa kwa teknolojia ya OLED pamoja na uwezo wa resolution hadi ya 1176 x 2400. Kioo hicho pia kinakuja na ukingo wa kushoto na kulia zilizo jikunja kwa nyuzi 88°.

Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya Huawei Mate 30 na Mate 30 Pro

Kioo hicho pia kinakuja na ulinzi wa Corning Gorilla Glass 6, ulinzi ambao unazuia kioo hicho kuchubuka au kupasuka kwa urahisi. Vilevile kama ilivyo Mate 30 simu hii pia inakuja na sehemu ya ulinzi ya Fingerprint chini ya kioo.

Kwa mbele juu simu hii inakuja na kamera mbili za Selfie zenye uwezo wa Megapixel 32 pamoja na 3D TOF camera, mbali na hayo simu hii inakuja na senser maalum ambazo zinaweza kutambua uso na macho yako na kubadilisha mwelekeo wa picha kulingana na muelekeo wa macho na uso wako. Ikiwa pamoja na uwezo wa kuendelesha simu bila kuigusa.

Kwa nyuma simu hii inakuja na kamera nne, ambapo kamera kuu inakuja na Megapixel 40 na nyingine zinakuja na Megapixel 8, Megapixel 40 na nyingine ikiwa ni 3D TOF camera. Kamera zote kwa pamoja zinakuja na uwezo wa kuchukua video za hadi 4K ikiwa ni sawa na kusema simu hii ina uwezo wa 2160p@30/60fps, 1080p@30/60/120fps, 1080p@960fps, 720p@7680fps, gyro-EIS.

Kwa upande wa sifa, Mate 30 Pro inaendeshwa na processor ya HiSilicon Kirin 990 (7 nm+), processor inayo saidiwa na RAM ya GB 8 na ukubwa wa ROM wa GB 128 au GB 256. Simu hii inasaidiwa na nano memory card yenye uwezo wa hadi GB 256, Sifa nyingine za Huawei Mate 30 Pro ni kama zifuatazo.

Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya Huawei Mate 30 na Mate 30 Pro

Sifa za Huawei Mate 30 Pro

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.53 chenye teknolojia ya OLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2400 pixels, na uwiano wa 18.7:9 ratio (~389 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 10 yenye mfumo wa Huawei EMUI 10
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (2×2.86 GHz Cortex-A76 & 2×2.36 GHz Cortex-A76 & 4×1.95 GHz Cortex-A55).
  • Aina ya Processor (Chipset) – HiSilicon Kirin 990 (7 nm+) Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Mali-G76 MP16.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 128 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na nano card hadi ya GB 256.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko simu za aina mbili moja inakuja na RAM ya GB 6 na nyingine inakuja na RAM ya GB 8.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 32 yenye HDR
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera nne kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 40 yenye f/1.8, 27mm, 1/2.3″ na nyingine ikiwa na Megapixel 8 yenye f/2.2, 17mm (wide lens), na nyingine inakuja na Megapixel 40 yenye f/2.4, 52mm (telephoto lens) na kamera ya mwisho ni 3D TOF camera. Huku zote zikiwa zinasadiwa na Leica optics, panorama, HDR, 4K pamoja na flash ya dual-LED dual-tone flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 4500mAh battery yenye teknolojia ya Fast battery charging yenye uwezo wa kuchaji asilimia 58 kwa nusu saa.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS. USB 3.1, Type-C 1.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi nne za Black, Space Silver, Cosmic Purple, Emerald Green.
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack. Inakuja na teknolojia ya kuzuia maji na vumbi.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Face ID, fingerprint (under display, optical), accelerometer, gyro, proximity, barometer, compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G, 4G na 5G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Chini ya Kioo).

Kwa upande wa bei, Huawei Mate 30 Pro inategemea kuanza kuuzwa hivi leo huko nchini china, na baadaye mwezi October simu hii inategemea kupatikana kote duniani kwa Euro €1,100, ambayo ni sawa na shilingi za Tanzania TZS 2,792,000 bila kodi kwa toleo la 4G. Toleo la 5G itauzwa kwa Euro €1,200 ambayo ni sawa na TZS 3,045,000 bila kodi.

Soko Jipya la AppGallery

Simu hizi kwa kua hazina huduma za Google, Huawei imeanisha kuwa watumiaji wa simu hizi wataweza kupakua app kupitia soko la Huawei la App Gallery ambapo sasa linasemekana kuwa na watumiaji zaidi ya milioni 100 hadi sasa.

Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya Huawei Mate 30 na Mate 30 Pro

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use