Hadi kufikia leo tarehe 27 mwezi August, Simu mpya kutoka kampuni ya Huawei, Huawei Mate 20 Lite bado haijazinduliwa rasmi. Hata hivyo japo kuwa simu hii haijazinduliwa lakini tayari simu hii imeshafikia kwenye masoko mbalimbali ya mtandaoni na unaweza kutoa oda ya simu hii kupitia masoko hayo.
Kupitia masoko hayo ya nchini poland na ujerumani, Tanzania Tech tumefanikiwa kupata sifa kamili za Huawei Mate 20 Lite pamoja na bei yake halisi kwa nchini humo. Hadi sasa tunafahamu kwamba Huawei Mate 20 Lite inakuja na kioo cha inch 6.3 kilicho tengenezwa kwa IPS LCD ambacho pia kinakuja na resolution ya 1080 x 2340 pixel. Simu hii inakuja na processor ya Kirin 710 chipset ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 6.
Huawei Mate 20 Lite inakuja na kamera nne kwa ujumla huku kamera mbili zikiwepo kwa mbele zenye uwezo wa Megapixel 24 na Megapixel 2, Vilevile kwa nyuma pia Mate 20 Lite inakuja na kamera mbili ambazo moja inakuja na uwezo wa Megapixel 20 na nyingine inakuja na uwezo wa Megapixel 2. Simu nzima inaendeshwa na battery yenye uwezo wa 3650mAh ambayo inaweza kuchajiwa kwa haraka kupitia teknolojia ya fast charging. Sifa nyingine za Huawei Mate 20 Lite ni kama zifuatazo.
Sifa za Huawei Mate 20 Lite
- Ukubwa wa Kioo – Inch 6.3 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2340 pixels, na uwiano wa 19.5:9 ratio (~409 ppi density).
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo).
- Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.2 GHz Cortex-A73 & 4×1.7 GHz Cortex-A53).
- Aina ya Processor (Chipset) – Hisilicon Kirin 710 Chipset.
- Uwezo wa GPU – Mali-G51 MP4.
- Ukubwa wa Ndani – GB 64 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card ya hadi GB 256.
- Ukubwa wa RAM – RAM ya GB 6
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Ziko kamera mbili moja inakuja na Megapixel 24 na nyingine inakuja na Megapixel 2 yenye depth sensor.
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili moja inakuja na Megapixel 24 yenye f/1.8, PDAF na nyingine inakuja na Megapixel 2 yenye depth sensor, huku zote zikisaidiwa na Flash ya LED flash.
- Uwezo wa Battery – Battery Inayotoka ya Li-Ion 3750 mAh battery yenye teknolojia ya Fast battery charging.
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 b/g/n, Wi-Fi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB 2.0, Type-C 1.0 reversible connector.
- Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Black, Gold na Blue
- Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Hybrid Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
- Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, proximity, compass.
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
- Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa nyuma).
Bei ya Huawei Mate 20 Lite
Kwa upande wa bei kama nilivyo kwambia simu hii bado haijatoka rasmi ila kwa upande wa nchini poland simu hii imewekwa kwenye tovuti ya X Kom ikiwa na bei ya złot ya poland 1599,00 zł ambayo ni sawa na Shilingi za Tanzania Tsh 996,000 bila kodi. Kwa hapa Tanzania bei hiyo inaweza kuongezeka kutokana na kodi pamoja na viwango vya kimataifa vya kubadilisha fedha.
Na hizo ndio sifa na bei ya Huawei Mate 20 Lite, endelea kutembelea Tanzania Tech tutakupa habari pindi simu hii itakapo zinduliwa rasmi na kutangaza tarehe ya upatikanaji kwa hapa Tanzania. Simu zote za Huawei Mate 20, Mate 20 Pro na Huawei Mate 20 Lite zinatarajiwa kuzinduliwa rasmi hivi karibuni.