Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Kampuni ya HTC Yazindua Simu Mpya ya HTC U12 Life

Zifahamu hizi hapa ndio sifa kamili na bei ya HTC U12 life
Sifa na Bei ya HTC U12 Life Sifa na Bei ya HTC U12 Life

Japokuwa kampuni ya HTC imekuwa na mwaka mbaya kwenye mauzo ya simu zake, lakini bado kampuni hiyo haijakata tamaa na sasa iko tayari kurudi sokoni na simu yake mpya ya HTC U12 Life.

Simu hiyo mpya ya HTC U12 Life inakuja na kioo cha Inch 6.0 chenye uwiano wa 18:9 pamoja na resolutiona ya 1080 x 2160 pixel, simu hii inatumia kioo kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya Super LCD ambacho kina uwezo wa kuonyesha rangi hadi milioni 16.

Advertisement

Simu hii haina ukingo wa juu maarufu kama notch na tofauti na simu ya HTC 12+, HTC U12 Life inakuja na sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama headphone jack. Simu hii pia inakuja na battery kubwa yenye uwezo wa 3600mAh ambayo haina teknolojia ya Fast charging.

Kwa upande wa kamera simu hii inakuja na kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na uwezo wa megapixel 16 na nyingine ikiwa na uwezo wa Megapixel 5, kwa mbele inakuja na kamera ya Selfie ambayo inauwezo wa megapixel 12 ambayo pia inasaidia na flash ya LED flash kwaajili ya kupiga picha nzuri za Selfie hata wakati wa usiku. Sifa nyingine za HTC U12 Life ni kama zifuatazo.

Sifa na Bei ya HTC U12 Life

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.0 chenye teknolojia ya Super LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2160 pixels, na uwiano wa 18:9 ratio (~402 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo).
  • Uwezo wa Processor – Octa-core 1.8 GHz Kryo 260.
  • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM636 Snapdragon 636 Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Adreno 509 au Adreno 512.
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu mbili moja ikiwa na GB 128 na nyingine ikiwa na GB 64 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card ya hadi GB 512.
  • Ukubwa wa RAM –  Ziko simu mbili moja ikiwa na RAM ya GB 6 na nyingine ikiwa na GB 4.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 13 yenye f/2.0, HDR, panorama pamoja na LED flash, .
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili moja inakuja na Megapixel 16 yenye f/2.0, PDAF na nyingine inakuja na Megapixel 5 yenye depth sensor, huku zote zikisaidiwa na HDR, panorama pamoja na Flash ya LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery Inayotoka ya Li-Ion 3600 mAh battery.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 b/g/n, Wi-Fi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS. USB 2.0, Type-C 1.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Moonlight Blue na Twilight Purple.
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa nyuma).

Bei ya HTC U12 Life

Kwa upande wa bei simu hii inatarajiwa kuingia sokoni kuanzia mwezi ujao na inatarajiwa kupatikana kuanzia Euro £300 ambayo hii ni sawa na Shilingi za Tanzania Tsh 893,000 bila kodi. Kumbuka bei hiyo inaweza kubadilika kwa Tanzania kutokana na kodi pamoja na viwango vya kubadilisha fedha vya siku husika.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use