Kampuni ya Huawei Yazindua Simu Mpya ya Honor Note 10

Huawei yaja na simu yake mpya ya Honor Note 10 Zijue sifa na bei ya simu hii
Sifa na Bei ya Honor Note 10 Sifa na Bei ya Honor Note 10

Baada ya kuwepo kwa tetesi nyingi juu ya ujio wa simu mpya kutoka kampuni ya Huawei, Hatimaye sasa leo Kampuni ya Huawei kupitia kampuni yake ya Honor leo imezindua simu yake mpya ya Honor Note 10 yenye uwezo mzuri na sifa bora.

Advertisement

Simu hii ya Honor Note 10 inakuja na kioo cha inch 6.95 chenye teknolojia ya Full HD+ AMOLED display pamoja na resolution ya 1080 x 2220 pixels. Simu hii pia inakuja na teknolojia zingine kwenye kioo chake kama vile HDR10 Standard pamoja na NTSC 115% color gamut.

Vilevile simu hii ya Honor Note 10 inakuja na processor kutoka kampuni ya Huawei ya Kirin 970 ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 6 au GB 8. Ukubwa wa ndani wa simu hii umegawanyika kwa simu za aina mbili huku simu yenye RAM ya GB 6 yenye ikiwa na ukubwa wa ndani wa GB 64 na simu yenye RAM yagb 8 yenyewe ikiwa na ukubwa wa ndani wa GB 128.

Simu hii pia imetengenezewa mkanda maalum ndani ya simu hiyo ambao unafanya kazi ya kupooza simu hiyo na kufanya uweze kuitumia simu hiyo kwa mda mrefu pale unapo angalia video au hata pale unapoitumia kucheza Game. Kwenye upande huo wa Game, simu hii inakuja na sehemu mpya ya GPU na CPU Turbo ambayo inafanya simu hiyo kufanya kazi kwa haraka zaidi hasa pale unapo itumia kucheza Game au kazi zingine kama hizo. Sehemu hii imewekewa kitufe maalum ambacho ndio kinatumika kuwasha sehemu hizo.

Simu hii ya Honor Note 10 inakuja na kamera mbili za nyuma moja ikiwa na Megapixel 24 na nyingine Megapixel 16, huku kwa mbele simu hiyo ikiwa na kamera ya selfie yenye Megapixel 13 huku kamera zote zikiwa zinakuja na teknolojia ya A.I au Artificial Intelligence. Sifa nyingine za Honor Note 10 ni kama zifuatazo.

Sifa za Honor Note 10

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.95 chenye teknolojia ya AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2220 pixels, 18.5:9 ratio (~355 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo) yenye mfumo wa EMUI 8.2
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.4 GHz Cortex-A73 & 4×1.8 GHz Cortex-A53), Hisilicon Kirin 970 Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Mali-G72 MP12
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu mbili moja ikiwa na GB 64 na nyingine ikiwa na GB 128 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa ukubwa na memory card hadi ya GB 256.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko simu mbili simu yenye GB 6 na nyingine GB 8.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele –  Megapixel 13.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili moja ikiwa na Megapixel 16 yenye (f/1.8) na nyingine ikiwa na Megapixel 24 yenye B/W (f/1.8), gyro-EIS (1080p), na PDAF. Kamera zote mbili zinasaidiwa na flash ya LED Flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po 5000 mAh battery yenye teknolojia ya Fast battery charging 4.5V/5A.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, USB 3.1, Type-C 1.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Midnight Black na Phantom Blue.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Hybrid Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Ulinzi kwa Fingerprint (Kwa Nyuma).

Bei ya Honor Note 10

Kwa upande wa bei simu hii ya Huawei Note 10 itakuja kwa bei tofauti kulingana na ukubwa wa ndani. Toleo la Honor Note 10 la ukubwa wa ndani wa GB 64 na RAM ya GB 6 litauzwa kwa Yuan ya China CNY 2,799 sawa na Tsh 935,000 huku Toleo la GB 128 na RAM ya GB 6 litauzwa kwa Yuan CNY 3,199 sawa na Tsh 1,068,000 na Honor Note 10 ya GB 128 na RAM ya GB 8 yenyewe itasimamia Yuan CNY 3,599 sawa na Tsh 1,202,000.

Simu zote ziko tayari kwa kutoa Oda kupitia tovuti ya Honor na simu hizo zitaanza kuwafikia wateja walio agiza kuanzia Tarehe 31 ya mwezi unaokuja.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use