Wakati tukiwa tunasubiri mkutano wa MWC 2019, kampuni ya Samsung siku chache zilizopita ilizindua tablet mpya ya Galaxy Tab S5e, Tablet hiyo inasemekana kuwa ni tablet nyembamba kuliko tablet zote zilizowahi kuzinduliwa na kampuni ya Samsung miaka ya karibuni.
https://www.tanzaniatech.one/finder/specs/samsung-galaxy-tab-s5e/
Kwa mujibu wa Samsung, Galaxy Tab S5e pia inakuja na kioo kikubwa zaidi huku ikiwa na pembe ndogo zaidi kuliko tablet iliyopita ya Samsung Galaxy Tab S4. Mbali na hayo, tablet hiyo mpya inakuja na kioo cha inch 10.5 chenye resolution ya 1600 x 2560 pixels, kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya Super AMOLED.
Kwa mbele Galaxy Tab S5e inakuja na kamera ya Selfie ya Megapixel 8, huku ikiwa na teknolojia ya face recognition. Kwa nyuma tablet hii inakuja na kamera ya Megapixel 13 yenye teknolojia ya HDR pamoja na panorama. Pia tablet hii inakuja na sehemu nyingine kama vile sehemu ya fingerprint iliyoko pembeni kwenye sehemu ya kuwashia, pamoja na mfumo wa Samsung DeX ambao unakuwezesha kutumia tablet hii kwenye kompyuta. Sifa nyingine za Galaxy Tab S5e ni kama zifuatazo.
TABLE OF CONTENTS
Sifa za Samsung Galaxy Tab S5e
- Ukubwa wa Kioo – Inch 10.5 chenye teknolojia ya Super AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16, pamoja na resolution ya 1600 x 2560 pixels.
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie) yenye mfumo wa OneUI
- Uwezo wa Processor – Octa-core (2×2.0 GHz 360 Gold & 6×1.7 GHz Kryo 360 Silver).
- Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM670 Snapdragon 670 (10 nm).
- Uwezo wa GPU – Adreno 615.
- Ukubwa wa Ndani – Ziko simu Tablet za aina mbili moja ikiwa na GB 64 na nyingine ikiwa na GB 128 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 512.
- Ukubwa wa RAM – Ziko tablet za aina mbili moja ikiwa na RAM GB 4 na nyingine ikiwa na RAM ya GB 6.
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8 yenye f/2.0, 26mm, 1/4.0″, 1.12µm uwezo wa kurekodi video za 1080p@30fps.
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 13 yenye f/2.0, 26mm, 1/3.4″, 1.0µm, AF. Huku ikisaidiwa na HDR, Panorama pamoja na flash ya LED flash.
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po 7040 mAh yenye teknolojia ya Fast Charging.
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE
na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS, GALILEO na USB ya 3.1, Type-C 1.0 reversible connector; magnetic connector. - Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Black, Gold, Silver.
- Mengineyo – Haina Radio FM, inatumia laini mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama headphone jack.
- Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass.
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
- Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Pembeni).
Bei ya Samsung Galaxy Tab S5e
Kwa upande wa bei Galaxy Tab S5e inakuja ikiwa inauzwa bei rahisi ya dollar za marekani $400 sawa na Shilingi za Tanzania Tsh 933,000 bila kodi. Hata hivyo, toleo lenye LTE litauzwa kwa bei ya ziada ya dollar za marekani $460 ambayo ni sawa na Shilingi za Tanzania Tsh 1,100,000 bila kodi.