Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Sifa na Bei ya Samsung Galaxy S10 na Galaxy S10 Plus

Baada ya tetesi za muda mrefu hizi hapa ndio sifa kamili za S10 na S10 Plus
Sifa na bei ya Samsung Galaxy S10 na Galaxy S10 Plus pic 2 Sifa na bei ya Samsung Galaxy S10 na Galaxy S10 Plus pic 2

Baada ya kampuni ya Samsung kuzindua simu mpya za Samsung Galaxy S10 na Galaxy S10 Plus hapo jana siku ya tarehe 20 february, Sasa kwetu ni wakati wa kuangalia sifa kamili pamoja na bei za simu hizi mpya.

Kama wewe ni mmoja wa watu waliofanikiwa kuangalia mubashara uzinduzi huu, basi unaweza kuwa tayari umeshajua sifa za simu hizi, ila kama hii ni mara yako ya kwanza hapa basi haya ndio mambo ya muhimu kuhusu simu hizi mpya za Galaxy S10 na Galaxy S10 Plus.

Advertisement

Samsung Galaxy S10

Kama ilivyotajwa kwenye tetesi mbalimbali za simu hizi, Galaxy S10 inakuja na teknolojia mpya pamoja na muonekano mpya kabisa. Kwa mbele simu hii inakuja na kioo cha inch 6.1 chenye resolution ya 1440 x 3040 pixels pamoja na teknolojia ya Dynamic AMOLED. Kioo hicho kwa juu kimekatwa ili kuweza kufit kamera ya Selfie ya Megapixel 10 yenye uwezo wa kuchukua video hadi za 2160p@30fps.

Mbali na hayo, sehemu muhimu kwenye simu hii ni pamoja na sehemu ya kamera za nyuma. Galaxy S10 inakuja na kamera tatu za nyuma, mbili zikiwa na Megapixel 12 na moja ikiwa na Megapixel 16 ambayo hii ni Ultra Wide.

Mbali na kamera, Simu hii ya Galaxy S10 inaendeshwa na processor ya Exynos 9820 Octa (8 nm) – EMEA au Qualcomm SDM855 Snapdragon 855 (7 nm) kwa simu zitakazo kuwa zinapatikana nchini China pamoja na Marekani. Processor hizi zinasaidiwa RAM ya GB 8 pamoja na ukubwa wa ndani au ROM ya GB 512 au GB 128, ukubwa unaweza kuongezwa kwa kutumia memory card hadi ya GB 512.

Vilevile Galaxy S10 inakuja na teknolojia mpya ya fingerprint iliyopo chini ya kioo pamoja na teknolojia mpya ya Wireless PowerShare, Teknolojia inayo ruhusu simu hiyo kuchaji simu au vifaa vingine kwa kutumia teknolojia ya wireless kwa kuweka kifaa unachotaka kuchaji nyuma ya simu hiyo.

Wireless PowerShare Galaxy S10

Kwenye upande wa battery, Galaxy S10 inakuja na battery ya Li-Ion yenye uwezo wa 3400 mAh yenye uwezo wa kudumu na chaji kwa masaa 24 kutokana na matumizi yako. Vilevile battery hii inawezeshwa na teknolojia ya Fast battery charging 15W, yenye uwezo wa kuchaji simu hii hadi asilimia 50 kwa muda wa nusu saa. Sifa nyingine za Samsung Galaxy S10 ni kama zifuatazo.

Samsung Galaxy S10 Pic Sifa na Bei ya Samsung Galaxy S10 na Galaxy S10 Plus Samsung Galaxy S10 Pic Sifa na Bei ya Samsung Galaxy S10 na Galaxy S10 Plus

Sifa za Samsung Galaxy S10

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.1 chenye teknolojia ya Dynamic AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16, pamoja na resolution ya 1440 x 3040 pixels.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie) yenye mfumo wa OneUI
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (2×2.7 GHz Mongoose M4 & 2×2.3 GHz Cortex-A75 & 4×1.9 GHz Cortex-A55) – EMEA au Octa-core (1×2.8 GHz Kryo 485 & 3×2.4 GHz Kryo 485 & 4×1.7 GHz Kryo 485) – USA/LATAM, China.
  • Aina ya Processor (Chipset) – Exynos 9820 Octa (8 nm) – EMEA au Qualcomm SDM855 Snapdragon 855 (7 nm) – USA/LATAM, China.
  • Uwezo wa GPU – Mali-G76 MP12 – EMEA.
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili moja ikiwa na GB 128 na nyingine ikiwa na GB 512 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 512.
  • Ukubwa wa RAM – RAM GB 8.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 10 yenye, f/1.9, Dual Pixel PDAF. Huku ikisaidiwa na Dual video call, Auto-HDR.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu moja inakuja na Megapixel 12, yenye uwezo wa f/1.5-2.4, 26mm (wide), 1/2.55″, 1.4µm, Dual Pixel PDAF, OIS, nyingine inakuja na Megapixel 12 yenye f/2.4, 52mm (telephoto), 1/3.6″, 1.0µm, AF, OIS, 2x optical zoom na kamera nyingine inakuja na Megapixel 16 yenye f/2.2, 12mm (ultrawide). Huku zote zikiwa na uwezo wa kurekodi video za 2160p@60fps, 1080p@240fps, 720p@960fps, HDR, dual-video rec.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3400 mAh yenye teknolojia ya Fast Charging.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE
    na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS, GALILEO na USB ya 3.1, Type-C 1.0 reversible connector; magnetic connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi sita za Prism White, Prism Black, Prism Green, Prism Blue, Canary Yellow, Flamingo Pink.
  • Mengineyo – Haina Radio FM (Radio ipo kwa simu za USA na China), inatumia laini mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama headphone jack. Inayo teknolojia ya kuzuia maji na vumbi, IP68 dust/water proof (up to 1.5m for 30 mins), Inayo teknolojia ya kuchaji vifaa vingine kwa kutumia Wireless.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass, barometer, heart rate, SpO2.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Chini ya kioo).

Bei ya Samsung Galaxy S10

Kwa upande wa bei Galaxy S10 inatarajiwa kuanza kuuzwa kuanzia mwezi wa tatu mwaka huu, kwa kuanzia dollar za marekani $899 ambayo ni sawa na Shilingi za Tanzania Tsh 2,97,000 bila kodi. Kumbuka bei hii inawezekana kupanda kutokana na kodi.

Samsung Galaxy S10 Plus

Kwa upande wa Samsung Galaxy S10 Plus, simu hii inakuja na uwezo wa hali ya juu kuliko simu zote za S10 zilizo zinduliwa hapo jana. Simu hii inakuja na mara mbili ya kila kitu ambacho kipo kwenye simu mpya ya Galaxy S10.

Kama nilivyo kwambia Samsung Galaxy S10 Plus inakuja na mara mbili ya kila kitu kilichopo kwenye Galaxy S10. Kwa kuanza na kamera Galaxy S10 Plus inakuja na kamera mbili kwa mbele huku kamera hizo zikiwa na Megapixel 10 na nyingine ikiwa na Megapixel 8. Kamera hizo ziko chini ya kioo cha inch 6.4 chenye resolution ya 1440 x 3040 pixels pamoja na teknolojia ya Dynamic AMOLED.

https://www.tanzaniatech.one/finder/specs/samsung-galaxy-s10-plus/

Kwa nyuma Galaxy S10 Plus inakuja na kamera tatu za Megapixel 12 zikiwa mbili pamoja na moja ya Megapixel 16 kama ilivyo Galaxy S10.

Mbali na kamera Galaxy S10 Plus inakuja na processor ya Exynos 9820 Octa (8 nm) – EMEA au Qualcomm SDM855 Snapdragon 855 (7 nm) kwa nchi za China na Marekani. Processor hizi zinasaidiwa na RAM ya GB 12 au GB 8, pamoja na ukubwa wa ndani au ROM ya TB 1 au GB 512. Vilevile unaweza kuongeza ukubwa huo kwa kutumia memory card hadi ya GB 512.

Kitu kingine ambachi ni tofauti kwenye simu hizi ni pamoja na battery, Galaxy S10 Plus inakuja na battery kubwa ya Li-Ion yenye uwezo wa 4100 mAh ikiwa na uwezo wa kudumu siku mbili kulingana na matumizi yako. Sifa nyingine za simu hii zinafanana kabisa na Galaxy S10 hivyo soma hapo chini kujua zaidi.

Samsung Galaxy S10 Pic

Sifa za Samsung Galaxy S10 Plus

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.4 chenye teknolojia ya Dynamic AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16, pamoja na resolution ya 1440 x 3040 pixels.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie) yenye mfumo wa One UI
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (2×2.7 GHz Mongoose M4 & 2×2.3 GHz Cortex-A75 & 4×1.9 GHz Cortex-A55) – EMEA au Octa-core (1×2.8 GHz Kryo 485 & 3×2.4 GHz Kryo 485 & 4×1.7 GHz Kryo 485) kwa nchini China pamoja na Marekani.
  • Aina ya Processor (Chipset) – Exynos 9820 Octa (8 nm) – EMEA au Qualcomm SDM855 Snapdragon 855 (7 nm) – USA/LATAM, China.
  • Uwezo wa GPU – Mali-G76 MP12 – EMEA.
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili moja ikiwa na TB 1 na nyingine ikiwa na GB 512 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 512.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko za aina mbili GB 12 au GB 8.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Ziko kamera mbili moja ikiwa na Megapixel 10 yenye, f/1.9, Dual Pixel PDAF na nyingine ikiwa na Megapixel 8 yenye f/2.2, depth sensor. Huku ikisaidiwa na Dual video call, Auto-HDR.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu moja inakuja na Megapixel 12, yenye uwezo wa f/1.5-2.4, 26mm (wide), 1/2.55″, 1.4µm, Dual Pixel PDAF, OIS, nyingine inakuja na Megapixel 12 yenye f/2.4, 52mm (telephoto), 1/3.6″, 1.0µm, AF, OIS, 2x optical zoom na kamera nyingine inakuja na Megapixel 16 yenye f/2.2, 12mm (ultrawide). Huku zote zikiwa na uwezo wa kurekodi video za 2160p@60fps, 1080p@240fps, 720p@960fps, HDR, dual-video rec.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 4100 mAh yenye teknolojia ya Fast Charging.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE
    na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS, GALILEO na USB ya 3.1, Type-C 1.0 reversible connector; magnetic connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi sita za Prism White, Prism Black, Prism Green, Prism Blue, Canary Yellow, Flamingo Pink.
  • Mengineyo – Haina Radio FM (Radio ipo kwa simu za USA na China), inatumia laini mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama headphone jack. Inayo teknolojia ya kuzuia maji na vumbi, IP68 dust/water proof (up to 1.5m for 30 mins), Inayo teknolojia ya kuchaji vifaa vingine kwa kutumia Wireless.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass, barometer, heart rate, SpO2.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Chini ya kioo).

Bei ya Samsung Galaxy S10 Plus

Kwa upande wa bei Galaxy S10 Plus inatarajiwa kupatikana mwezi wa tatu kama ilivyo Galaxy S10, Lakini Galaxy S10 Plus itakuwa inapatika kwa bei ghali zaidi ya dollar za marekani $999 sawa na shilingi za Tanzania Tsh 1,330,000 bila kodi. Kumbuka bei inaweza kubadilika kulingana na viwango vya kubadilisha fedha pamoja na kodi.

Na hizo ndio bei pamoja na sifa za Samsung Galaxy S10 pamoja na S10 Plus zilizo zinduliwa rasmi hapo siku ya jana. Kujua zaidi kuhusu lini simu hizi zitafika hapa Tanzania endelea kutembelea Tanzania Tech.

6 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use