Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Samsung Yazindua Simu Mpya za Galaxy M10 na Galaxy M20

Hizi hapa ndio sifa kamili na bei ya Samsung Galaxy M10 na Galaxy M20
Samsung Yazindua Simu Mpya za Galaxy M10 na Galaxy M20 Samsung Yazindua Simu Mpya za Galaxy M10 na Galaxy M20

Baada ya tetesi za muda mrefu hatimaye hivi leo kampuni ya Samsung imezindua simu mpya za Samsung Galaxy M10 pamoja na Samsung Galaxy M20. Kama unavyoweza kuona majina ya simu hizi ni mapya kabisa hii ikiwa na maana kuwa Galaxy M ni aina mpya ya simu kutoka kampuni ya Samsung.

Samsung Galaxy M10

Tukianza kuangalia Samsung Galaxy M10, yenyewe inakuja na kioo cha inch 6.0 chenye resolution ya 1520 x 720px, kioo ambacho kimetengenezwa kwa teknolojia ya PLS TFT Display. Simu hii inakuja na ukingo wa juu maarufu kama Infinity-V notch, ukingo ambao unatumika kuhifadhi kamera ya mbele ya Megapixel 5.

Advertisement

Kwa nyuma simu hii inakuja na kamera mbili, kamera moja ikiwa na Megapixel 13 na nyingine ikiwa na Megapixel 5 ambayo hii ni Ultra wide. Simu hii inaendeshwa na processor ya Exynos 7870 (14nm 8x Cortex-A53 @ 1.6GHz) ambayo inasaidiwa na RAM kati ya GB 2 au GB 3. Sifa nyingine za Samsung Galaxy M10 ni kama zifuatazo.

Sifa za Samsung Galaxy M10

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.2 chenye teknolojia ya PLS TFT capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1520 pixels, pamoja na uwiano wa 19:9 ratio (~270 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core 1.6 GHz Cortex-A53
  • Aina ya Processor (Chipset) – Exynos 7870 Octa (14 nm).
  • Uwezo wa GPU – Mali-T830 MP1.
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili moja inayo GB 32 na nyingine inayo GB 16 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 512.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko simu mbili moja ikiwa na RAM ya GB 3 na nyingine ikiwa na GB 2
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 5
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 13 yenye f/1.9, 1/3.1″, 1.12µm, PDAF na nyingine ikiwa na Megapixel 5 yenye f/2.2, 1/5″, 1.12µm, depth sensor. Huku zote zikiwa zinasadiwa na Flash ya LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3400 mAh battery.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS. USB ya microUSB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Ocean Blue na Charcoal Black.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za accelerometer, proximity na compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Haina Fingerprint.

Bei ya Samsung Galaxy M10

Kwa upande wa bei Samsung Galaxy M10 kwa sasa inapatikana kwa nchini India na inapatikana kwa rupee ya India INR 8,000 ambayo ni sawa na takribani Shilingi za Tanzania TSh 260,000 bila kodi kwa toleo lenye RAM ya GB 2, na Rupee ya India INR 13,000 sawa na Tsh 423,000 bila kodi kwa toleo lenye RAM ya GB 3.

Samsung Galaxy M20

Kwa upande wa simu ya Samsung Galaxy M20, Simu hii inakuja na sifa nzuri zaidi ya Galaxy M10, Simu hii inakuja na kioo cha Inch 6.3 chenye resolution ya 2340 x 1080px ambacho pia kime tengenezwa kwa teknolojia ya IPS LCD Display. Kama ilivyo M10, Galaxy M20 nayo inakuja na ukingo wa juu maarufu kama Infinity-V Notch.

Kwenye ukingo huo kuna kamera ya mbele yenye uwezo wa Megapixel 8, kamera ambayo pia inatumika kufanya kazi kama Face unlock scanner. Kwa nyuma simu hii inakuja na kamera mbili moja ikiwa na Megapixel 13 na nyingine ikiwa na Megapixel 5. Galaxy M20 inaendeshwa na processor ya Exynos 7904 (14nm, 4x Cortex-A73 @ 1.8GHz and 4x Cortex-A53 @ 1.8GHz) ambayo inasaidiwa na RAM kati ya GB 3 au GB 5, Sifa nyingine za Samsung Galaxy M20 ni kama zifuatazo.

Sifa za Samsung Galaxy M20

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.3 chenye teknolojia ya PLS TFT (FHD) capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1520 pixels, pamoja na uwiano wa 19:9 ratio (~490 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×1.8 GHz Kryo 260 Gold & 4×1.8 GHz Kryo 260 Silver)
  • Aina ya Processor (Chipset) – Exynos 7870 Octa (14 nm).
  • Uwezo wa GPU – Exynos 7904 Octa (14 nm).
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili moja inayo GB 64 na nyingine inayo GB 32 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 512.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko simu mbili moja ikiwa na RAM ya GB 4 na nyingine ikiwa na GB 3
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 13 yenye f/1.9, 1/3.1″, 1.12µm, PDAF na nyingine ikiwa na Megapixel 5 yenye f/2.2, 1/5″, 1.12µm, depth sensor. Huku zote zikiwa zinasadiwa na Flash ya LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 5000 mAh battery.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS. USB ya Type-C 1.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Ocean Blue na Charcoal Black.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity na compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).

Bei ya Samsung Galaxy M20

Kwa upande wa bei Galaxy M20 kwa sasa inapatikana kwa nchini india huku ikiwa inauzwa ka Rupee ya India INR 13,000 sawa na Tsh 423,000 bila kodi kwa toleo lenye RAM ya GB 64, na Rupee INR 11,000 sawa na Tsh 360,000 bila kodi kwa toleo lenye RAM ya GB 32.

Kwa mujibu wa tovuti ya GSMArena, sasa unaweza kutoa oda ya Simu zote hizi kupitia tovuti ya Amazon ya nchini India, na upatikanaji wa simu hizi utaanza rasmi tarehe 5 ya mwezi wa pili mwaka huu 2019.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use