Hizi Hapa Sifa na Bei za Samsung Galaxy J4 na Galaxy J6

Hizi hapa sifa kamili na bei za simu mpya za Samsung Galaxy J Series
Galaxy J4 na Galaxy J6 Galaxy J4 na Galaxy J6

Inawezekana kabisa kwa siku ya leo Samsung inaongoza kwa kuzindua simu nyingi kwa siku moja, kwani baada ya kuzinduliwa simu mpya Galaxy S Light Luxury huko nchini china, Sasa Samsung imezindua rasmi zimu mpya za Galaxy J Series ambazo ni Galaxy J4 pamoja na Galaxy J6.

Kwa sababu tulisha weza kuona muonekano wa simu hizi kwenye makala zilizopita sasa twende moja kwa moja tukaangalie sifa za simu hizi mpya, Kama ukusoma makala zilizo pita unaweza kusoma makala hizo kwanza kisha njoo soma sifa za simu hizo hapa.

Advertisement

Samsung Galaxy J6

Sifa za Samsung Galaxy J6

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 5.6 chenye teknolojia ya Super AMOLED display, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1480 pixels, 18.5:9 ratio (~294 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.0 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core 1.6 GHz Cortex-A53, Exynos 7870 Octa Chipest.
  • Uwezo wa GPU – Mali-T830 MP1
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili moja itakuwa na GB 32 na nyingine itakuwa na uwezo wa GB 64 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 256.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko simu za aina mbili moja itakuwa na GB 3 na nyingine itakuwa na GB 4
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8 yenye (f/1.9), LED flash, phase detection autofocus, pamoja na LED flash.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 13 yenye uwezo wa (f/1.9, 28mm), autofocus, pamoja na LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery inayotoka ya Li-Ion 3000 mAh battery
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bletuooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, Tyep C USB.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Black, Gold na Blue
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Micro-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint. (Kwa Nyuma)

Kama utakuwa makini, utaona kuwa simu hii imefanana sana sifa na simu mpya ya Galaxy A6 ambayo nayo pia leo imezinduliwa kwa nchi za Europe. Tofauti iliyoko kati ya Galaxy J6 na Galaxy A6 ni kamera, ambayo Galaxy A6 yenyewe inayo kamera kubwa zaidi.

Samsung Galaxy J4

Sifa za Samsung Galaxy J4

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 5.5 chenye teknolojia ya Super AMOLED display, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1280 pixels, 16:9 ratio (~267 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.0 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core 1.4 GHz Cortex-A53, Exynos 7570 Quad Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Mali-T720 MP2
  • Ukubwa wa Ndani – GB 16 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 256.
  • Ukubwa wa RAM – GB 2
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 5 yenye f/2.2, LED flash.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 13 yenye uwezo wa (f/1.9, 28mm), Geo-tagging, touch focus, face detection, panorama, HDR, autofocus, pamoja na LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3000 mAh battery
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, Type C USB.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Black, Gold na Orchid Gray
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Micro-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Haina Fingerprint.

Bei ya Galaxy J4 na Galaxy J6

Simu hizi mpya za Galaxy J4 pamoja na Galaxy J6 kuna uwezekano mkubwa wa simu hizi kuja Afrika na endapo zikija hapa Tanzania unaweza kuipata kwa Tsh 550,000 kwa Samsung Galaxy J6 yenye GB 64 na RAM ya GB 4 na Galaxy J6 yenye GB 32 na RAM ya GB 3 itauzwa kwa Tsh 450,000. Bei ya Galaxy J4 bado haija tangazwa endelea kutembelea Tanzania Tech tutakujulisha pindi tutakapo pata bei halisi ya simu hiyo. Kumbuka bei inaweza kubadilika kwa Tanzania kwa sababu ya Kodi.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use