Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Sifa na Bei ya Galaxy Fold Simu Inayojikunja Kutoka Samsung

Sifa na bei ya simu inayojikunja kutoka Samsung
Sifa na bei ya Galaxy Fold Sifa na bei ya Galaxy Fold

Kampuni ya Samsung Hapo jana ilizindua simu mpya za Galaxy S10 na Galaxy S10 Plus, katika uzinduzi huo Samsung ili tangaza rasmi ujio wa simu yake mpya inayojikunja iliyopewa jina la Samsung Galaxy Fold.

Kama ambavyo ilikuwa kwenye simu za Galaxy S10 na S10 Plus, Galaxy Fold nayo pia ilifanikiwa kuvuja kwenye tetesi ambazo pia zikuwa hapa kwenye tovuti ya Tanzania Tech. Kama wewe ni msomaji wa tovuti ya Tanzania Tech basi lazima utakuwa unajua kidogo kuhusu simu, kama hujui basi hizi ndio sifa za Galaxy Fold.

Advertisement

Kwa mujibu wa Samsung, Galaxy Fold inakuja na kioo cha inch 4.6 ikiwa imefungwa, na Inch 7.3 ikiwa imefunguliwa, Kioo cha mbele cha Galaxy Fold kimetengenezwa kwa teknolojia ya Super  AMOLED, wakati kioo cha ndani cha simu hii kimetengenezwa kwa teknolojia ya Dynamic AMOLED ambayo hii ni teknolojia ya juu ya Super AMOLED.

Galaxy Fold inaendeshwa na processor ya Qualcomm SDM855 Snapdragon 855 (7 nm) ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 12 pamoja na ukubwa wa ndani au ROM ya GB 512. Simu hii haina sehemu ya Memory Card hivyo hutoweza kuongeza ukubwa huo.

Kwa upande wa Kamera Galaxy Fold inakuja na kamera tatu kwa nyuma kama ilivyo simu za Galaxy S10, kamera mbili zina Megapixel 12 na moja inakuja na Megapixel 16, kamera zote hizo zikisaidiwa na Flash ya LED Flash. Vilevile simu hii ikiwa imefunguliwa inakuja na kamera mbili za Selfie, moja ikiwa na Megapixel 10 na nyingine ikiwa na Megapixel 8, pia simu hiyo ikiwa imefungwa inakuja na kamera moja ambayo ina Megapixel 10.

Simu hii inakuja na Battery ya Li-Po yenye uwezo wa 4380 mAh yenye uwezo wa kudumu na chaji siku mbili kulingana na matumizi yako. Battery ya simu hii inakuja na teknolojia ya Fast charging ambayo inasaidia simu hii kujaa chaji kwa haraka zaidi. Sifa nyingine za Galaxy Fold zinafanana kabisa na Simu za Galaxy S10 na Galaxy S10 Plus.

Samsung-Galaxy-Fold_ Samsung-Galaxy-Fold_ Samsung-Galaxy-Fold_

Sifa za Samsung Galaxy Fold

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 7.3 (Ikiwa imefunguliwa) chenye teknolojia ya Dynamic AMOLED capacitive touchscreen, Inch 4.6 inches HD+ Super AMOLED (21:9) ikiwa imefunguliwa vyote vikiwa na uwezo wa kuonyesha rangi Milioni 16.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie) yenye mfumo wa OneUI
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (1×2.84 GHz Kryo 485 & 3×2.42 GHz Kryo 485 & 4×1.8 GHz Kryo 485).
  • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM855 Snapdragon 855 (7 nm).
  • Uwezo wa GPU – Adreno 640.
  • Ukubwa wa Ndani –  GB 512.
  • Ukubwa wa RAM – RAM GB 12.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Ikiwa imefulinguliwa ziko kamera mbili Megapixel 10 yenye f/2.2, PDAF na nyingine Megapixel 8, yenye f/1.9, depth sensor na ikiwa imefungwa inakuja na kamera moja ya Megapixel 10. Huku ikisaidiwa na teknolojia ya HDR.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu moja inakuja na Megapixel 12, yenye uwezo wa f/1.5-2.4, 26mm (wide), 1/2.55″, 1.4µm, Dual Pixel PDAF, OIS, nyingine inakuja na Megapixel 12 yenye f/2.4, 52mm (telephoto), 1/3.6″, 1.0µm, AF, OIS, 2x optical zoom na kamera nyingine inakuja na Megapixel 16 yenye f/2.2, 12mm (ultrawide). Huku zote zikiwa na uwezo wa kurekodi video za 2160p@60fps, 1080p@240fps, 720p@960fps, HDR, dual-video rec.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po 4380 mAh yenye teknolojia ya Fast Charging.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE
    na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS, GALILEO na USB ya 3.1, Type-C 1.0 reversible connector; magnetic connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi moja ya Black
  • Mengineyo – Haina Radio FM, inatumia laini mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint (side-mounted), accelerometer, gyro, proximity, compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa pembeni).

Bei ya Samsung Galaxy Fold

Kwa upande wa bei, Galaxy Fold inatarajiwa kutoka baadae mwaka huu na itakuwa sio simu ya bei rahisi kwani inategemewa kuuzwa kwa dollar za marekani $1,980 ambayo hii ni sawa na Shilingi za Tanzania Tsh 4,634,000 bila kodi. Bei ya simu hii inawezekana kupanda kutokana na kodi na kubadilika kwa viwango vya kubadilisha fedha.

Na hizo ndio sifa za Galax Fold ambayo imezinduliwa hapo jana, Je nini maoni yako kuhusu simu hii..? Je hii ni moja kati ya simu ambayo ungependa kuwa nayo mwaka huu na sio Toyota Vitz..?

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use