Hizi Hapa Sifa na Bei ya Tecno Camon 11 na Camon 11 Pro

Yaliyomo kwenye simu mpya za Camon 11 na Camon 11 Pro
hizi ndio sifa na bei ya tecno camon 11 na Camon 11 pro hizi ndio sifa na bei ya tecno camon 11 na Camon 11 pro

Habari njema kwa wapenzi wa simu za Tecno hatimaye hivi leo kampuni ya Tecno imezindua simu zake mpya za Tecno Camon 11 na Camon 11 Pro, Kama taarifa zilivyosema hapo awali, simu hizi mpya zimezinduliwa hivi leo huko nchini Kenya na ukweli simu hizi zinakuja na muonekano mzuri na sifa nzuri kuliko toleo la simu za Tecno Camon X.

Advertisement

Kwa kuanza labda tuanze kuangalia sifa za Tecno Camon 11 Pro, Simu hii mpya ya Camon 11 Pro inakuja na kioo cha inch 6.2 chenye ukingo wa juu maarufu kama notch, kioo hicho kimetengenezwa kwa teknolojia ya LCD pamoja na resolution ya 720 x 1500 pixel na uwiano wa 19:9. Kwenye ukingo huo wa juu maarufu kama notch kuna kamera moja ya selfie yenye Megapixel 24 pamoja na sensor maalum kwaajili ya kusaidia sehemu ya AR emoji kufanya kazi vizuri. Sehemu hiyo ni kama ile ya kwenye iPhone X inayoitwa Animoji.

Hizi Hapa Sifa na Bei ya Tecno Camon 11 na Camon 11 Pro

Tukiwa bado tuko kwa mbele, Kamera hiyo ya selfie pia inakuja na tekolojia ya AI ambayo inafanya uweze kupiga picha zenye mwanga bora na muonekano mzuri zaidi. Tukiamia kwa nyuma Camon 11 Pro inakuja na kamera mbili moja ikiwa ina Megapixel 16 na nyingine inakuja na Megapixel 5, kamera hizi nazo zinakuja na mfumo wa AI ambao unafanya uweze kupiga picha makini zaidi. Mbali na hayo kamera hizo mbili za nyuma zinakuja na mfumo wa kubadilisha maandishi kutoka kwenye karatasi na kuweka kwenye mfumo wa Softcopy moja kwa moja bila kutumia programu yoyote.

Simu hii inaendeshwa na mfumo wa Android 8.1 Oreo pamoja na mfumo mpya wa HiOS (4.1) ambao unakuja na maboresho zaidi. Tofauti na tulivyo zoea, hivi sasa simu hizi za Tecno Camon 11 zinakuja na RAM kubwa zaidi huku toleo hili la Camon 11 Pro likiwa na RAM ya GB 6. Mbali na hayo sifa nyingine za Tecno Camon 11 Pro ni kama zifuatavyo.

Sifa za Tecno Camon 11 Pro

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.2 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1500 pixels, na uwiano wa 19:9 ratio (~269 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo) na HiOS 4.1
  • Uwezo wa Processor – Octa-Core 2.0GHz.
  • Aina ya Processor (Chipset) – MediaTek Helio P22 Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Mali-G71 MP2.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 64 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 128.
  • Ukubwa wa RAM – GB 6.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 24 yenye teknolojia ya AI pamoja na LED Flash
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili moja ikiwa na Megapixel 16 na nyingine inakuja na Megapixel 5 zenye AI, Autofocus na Flash ya Dual-LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po 3750 mAh battery.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.0, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS. USB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Black na Blue
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM,), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Light Sensor, Compass, Proximity Sensor, Face ID Sensor na Fingerprint.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma), na Ulinzi wa kutambua uso (Face ID).

Bei ya Tecno Camon 11 Pro

Kwa upande wa bei Tecno Camon 11 Pro inakuja ikiwa inauzwa kwa shilingi za Kenya Ksh 24,000 ambayo hii ni sawa na makadirio ya hadi Tsh 536,000 bila kodi. Kwa hapa Tanzania tegemea kupata simu hii kuanzia Tsh 550,000 au zaidi.

Baada ya kuangalia sifa za Camon 11 Pro hebu sasa tuangalie sifa na bei ya Camon 11. Kwa upande wa Camon 11 nayo inakuja na kioo cha Inch 6.2 chenye ukingo wa juu, pia kioo hicho kimetengenezwa kwa LCD uku kikiwa na resolution ya 720 x 1500 pixel na uwiano wa 19:9.

Kwa mbele Camon 11 inakuja na kamera ya Megapixel 16 huku ikiwa na Flash ya LED, Kwa nyuma simu hii inakuja na kamera mbili huku kamera moja ikiwa na Megapixel 13 na nyingine ikiwa na Megapixel 2. Camon 11 yenyewe pia inaendeshwa na Android Oreo 8.1 ambayo juu kuna mfumo wa Tecno wa HiOS 4.1, utofauti mwingine kwenye simu hii ni GPU ambapo GPU ya Camon 11 ni PowerVR GE8320 na RAM ambayo inakuja na ukubwa wa GB 3 pamoja na ukubwa wa ndani ambao ni GB 32. Sifa kamili za Tecno Camon 11 ni kama zifuatazo.

Sifa za Tecno Camon 11

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.2 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1500 pixels, na uwiano wa 19:9 ratio (~269 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo) na HiOS 4.1
  • Uwezo wa Processor – Octa-Core 2.0GHz.
  • Aina ya Processor (Chipset) – MediaTek Helio P22 Chipset.
  • Uwezo wa GPU – PowerVR GE8320.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 32 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 128.
  • Ukubwa wa RAM – GB 3.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 16 yenye teknolojia ya AI pamoja na LED Flash
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili moja ikiwa na Megapixel 13 na nyingine inakuja na Megapixel 2 zenye AI, Autofocus na Flash ya Dual-LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po 3750 mAh battery.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.0, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS. USB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Red, Black na Blue
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM,), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Light Sensor, Compass, Proximity Sensor, Face ID Sensor na Fingerprint.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma), na Ulinzi wa kutambua uso (Face ID).

Bei ya Tecno Camon 11

Kwa upande wa bei, Tecno Camon 11 yenyewe itauzwa kwa shilingi ya Kenya Ksh 15,000 sawa na Tsh 336,000. Kwa hapa Tanzania tegemea kuipata simu hii kuanzia Tsh 350,000 na kuendelea.

Kwa sasa simu hizi bado hazijapatikana rasmi hapa Tanzania, ila pengine ndani ya wiki mbili ama tatu tegemea kuzipata simu hizi kupitia maduka mbalimbali ya Tecno pia kupitia mtandao wa Jumia. Kwa habari zaidi za simu hii pamoja na video ya mapitio ya simu hii hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

14 comments
  1. Ninayo hiyo Tecno camon 11pro…Daaah! Aisee ni hatari sanaa, hongereni aiseee ila msitutolee toleo jipya fasta fasta mtatushushia hadhi huku mtaani.. Kwasasa hivi yaani sisi ndo wanaumee tunaotembea kifua mbele mtaani….Hahahahahaaaa, nani anateseka na camon 11pro wapendwaa???????

  2. Mimi niwakala wa usajili Lani.
    Nauliza Tecno CAMON 11. zinaweza kusapoti kifaa cha usajili (biometric)?

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use