Kampuni ya TCL Yazindua Simu Mpya ya Alcatel 5V

Kampuni ya Alcatel sasa imeanza kuja na simu za kisasa zenye muonekano bora
Simu mpya ya Alcatel 5V Simu mpya ya Alcatel 5V

Alcatel ni simu ambazo ziliwahi kutumiwa sana hapa Tanzania, hivi karibuni simu hizo zimepotea kidogo hapa Tanzania, lakini sio kwamba simu hizo hazipo sokoni kabisa kwani siku ya jana kampuni ya TCL ambayo sasa ndio inamiliki kampuni ya Alcatel, imezindua simu mpya ya Alcatel 5V simu inayokuja na muonekano mzuri pamoja na ukingo wa juu maarufu kama top notch.

Alcatel 5V inakuja na kioo cha inch 6.2 chenye uwiano wa 19.9 pamoja na resulution ya 720 x 1500, muonekano wa simu hii ni tofauti na ambavyo ungedhani, kwani kipindi cha nyuma simu kutoka kampuni Alcatel zilikuwa zinamuonekano wa kawaida sana.

Advertisement

Sifa nyingine za Alcatel V5 ni pamoja na kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 12 na nyingine ikiwa na Megapixel 2, kwa mbele simu hii inakuja na kamera yenye uwezo wa Megapixel 8 huku ikiwa na uwezo wa 1.12μm pixels. Sifa nyingine ni kama zifuatazo.

Sifa za Alcatel V5

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.2 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1500 pixels, 19:9 ratio.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android One 8.1 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core 2.0 GHz Cortex-A53, MediaTek’s Helio P22 (MT6762) Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Adreno 504
  • Ukubwa wa Ndani – GB 32 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 256.
  • Ukubwa wa RAM – GB 3
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele –  Megapixel 6.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili moja ikiwa na Megapixel 12 na nyingine ikiwa na Megapixel 2. Kamera zote mbili zinasaidiwa na flash ya LED Flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 4000 mAh battery.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, microUSB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Blue na Black
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Ulinzi kwa Fingerprint (Kwa Nyuma).

Bei ya Alcatel 5V

Kwa upande wa bei ya simu, Alcatel V5 itakuwa inapatikana kwa baadhi ya nchi na itakuwa ikipatikana kwa dollar za marekani $200 sawa na shilingi za Tanzania TSh 456,000. Kumbuka bei hii inaweza kubadilika kwa hapa Tanzania kutokana na kupanda na kushuka kwa viwango vya kubadilisha fedha pamoja na kodi.

Na hiyo ndio simu mpya kutoka kampuni ya Alcatel ambayo mwaka huu imesha zindua simu nyingi za kisasa ikiwemo simu ya Alcatel 1X simu ya bei rahisi yenye kutumia mfumo wa Android Go.

3 comments
    1. Ni kampuni ya kutengeneza eletroniki ambayo inamiliki kampuni za simu kama Blackberry na Alcatel.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use