Mkutano wa CES 2019 bado unaendelea huko Las Vegas nchini marekani, Hivi karibuni kampuni ya Alcatel imeonyesha simu zake mpya za Alcatel 1x (2019), Simu ambazo ni toleo jipya la simu ya Alcatel 1x (2018) moja kati ya simu za kwanza kabisa kuwa na mfumo wa Android Go.
Alcatel 1x (2019) inakuja na kioo kikubwa zaidi cha IPS display chenye inch 5.5 pamoja na resolution ya 720p. Kwa mbele simu hii inakuja na kamera ya Megapixel 5 ambayo inasaidiwa na Flash ya LED, kwa nyuma Alcatel 1x (2019) inakuja na kamera mbili moja ikiwa na Megapixel 13 na nyingine ikiwa na Megapixel 2 ambayo hii ni depth sensor kwa ajili ya sehemu ya bokeh effects.
Alcatel 1x (2019) inaendeshwa na processor ya MediaTek MT6739 (quad Cortex-A53) ambayo inakuja na uwezo wa 1.5GHz au 1.3GHz. Processor hiyo inasaidiwa na RAM ya GB 2 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 16. Tofauti na toleo la mwaka jana la Android Go, simu hii mpya sasa inatumia mfumo wa kawaida wa Android Oreo 8.1. Sifa nyingine za simu hii mpya ya Alcatel 1x (2019) ni kama zifuatazo.
TABLE OF CONTENTS
Sifa za Alcatel 1x (2019)
- Ukubwa wa Kioo – Inch 5.5 chenye teknolojia ya IPS LCD, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resoluti ya 720 x 1440 pixels, 18:9 ratio (~293 ppi density)
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
- Uwezo wa Processor – Quad-core 1.5 GHz Cortex-A53
- Aina ya Processor – Mediatek MT6739 (28 nm)
- Uwezo wa GPU – PowerVR GE8100
- Ukubwa wa Ndani – GB 16 yenye uwezo wa kuongezewa na memory card hadi GB 128.
- Ukubwa wa RAM – GB 2
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 5 yenye LED Flash.
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko mbili moja ikiwa na Megapixel 13 na Kamera nyingine inayo Megapixel 2 ambayo hii ni depth sensor. Kamera zote zinasaidiwa na Flash ya LED.
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Non-removable Li-Po 3000 mAh.
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, microUSB 2.0, USB On-The-Go.
- Rangi – Inakuja kwa rangi Mbili za Pebble Blue, Pebble Black.
- Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
- Aina za Sensor – Fingerprint, accelerometer, proximity na compass
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
- Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa nyuma).
Bei ya Alcatel 1x (2019)
Kwa upande wa bei Alcatel 1x (2019) inategemewa kuuzwa Asia, Amerika ya Kusini, Mashariki ya Kati, Afrika pamoja na Ulaya. Simu hii inatarajiwa kupatikana kwa bei ya dollar za marekani $120 ambayo ni sawa na Shilingi za Tanzania Tsh 277,000 bila kodi.
Kwa habari zaidi kuhusu mkutano wa CES 2019 hakikisha unatembelea Tanzania Tech kila siku hasa kipengele cha CES 2019.
Nahitaji hiyo cm Alcatel 1x naipateje?