Mtandao wa Facebook umekua ni msaada mkubwa hasa kwa nchi za Afrika, Facebook imeweza kusaidi sekta mbalimbali za teknolojia ikiwa ni pamoja na kuboresha na kurahisisha mawasiliano kati ya ndugu jamaa na wengine wote tunao wapenda, yote haya yanafanyika kupitia programu pamoja na nyezo mbalimbali zinazotolewa na mtandao huo maarufu wa kijamii.
Katika kuelekea kwenye mkutano wake wa Facebook Developer Conference al maarufu kama F8, Facebook kupitia mtandao wa Facebook Developer imeanza shindao lake linalo kwenda kwa jina la Bots for Messenger Challenge, shindano hili linawahusu waafrika wanaoishi Afrika Mashariki ya Kati, Afrika Kaskazini pamoja na Afrika kusini mwa Sahara. Shindano hilo kama ilivyo jina lake mtu au kikundi cha watu wanatakiwa kutengeneza Bots au roboti maalum ambazo zitakua zinafanya kazi kwenye programu ya Facebook Messenger.
Washiriki wanatakiwa kutengeneza roboti hizo kupitia Facebook kwa kufuata makundi maalum ya Gaming, Entertainment, Productivity, Utility pamoja na Social Good, makundi haya pekee ndiyo yatakupa nafasi ya kutengeneza bots hizo na kutuma kwaajili ya ushiriki kuanzia tarehe 15 mwezi March mwaka huu 2017. Washiriki watakao pendalea kushiriki kama kikundi facebook inaruhusu hadi watu watatu kuungana ili kutengeneza bots hizo, Kuna zawadi nyingi sana zitatolewa ikiwepo simu Gear VR pamoja na pesa taslimu mpaka kiasi cha dollar za marekani $40,000 ikiwa ni pamoja na Facebook mentorship tofauti kwa kila mshindi wa shindano hilo.
Kama unataka kujua zaidi jinsi ya kushiriki tembelea kwenye tovuti yao ya Messenger Challenge kwani hapo ndipo utakapo pata habari zote pamoja na vigezo na masharti ya kushiriki. Pia kama unataka kuona mfano wa Facebook Messenger Bots bofya hapa kisha chagua bots na ujaribu kupitia programu yako ya Facebook Messenger, bots hizo zinafanya kazi vizuri kwenye programu zote za facebook messenger hata ile ya kwenye kompyuta.