Kama wewe ni mmoja wa watu ambao kwa muda ulikuwa unataka kushare screen ya simu yako kwenye Smart TV yako basi makala hii ni kwa ajili yako.
Kupitia makala hii nitakuonyesha njia rahisi ambayo unaweza kutumia kuweza kushare screen ya simu yako au kioo cha simu yako kwenye Smart TV. Njia hii ni rahisi lakini inahitaji kufuata maelekezo haya hatua kwa hatua.
Basi bila kupoteza muda moja kwa moja twende kwenye hatua hizi ambazo ni rahisi, kumbuka ni muhimu kufuata hatua zote kwa usahihi.
Share Screen Kwenye Smart TV
Kwa kuanza unatakiwa kuhakikisha kama Smart TV yako inakuja na teknolojia ya chromecast built in. Kama box la TV yako lime andikwa chromecast built in, basi TV yako inakuja na teknolojia hiyo, kama haina teknolojia hii pia usijali.
Kama TV yako haina teknolojia hiyo unaweza kudowonload app ya Chromecast built-in kwenye Smart TV yako kupitia link hapo chini.
Kama TV yako inayo teknolojia ya chromecast built in, moja kwa moja endelea kwa kudownload app ya Google Home kupitia simu yako ya Android au iOS.
Baada ya kuinstall app hii, moja kwa moja endelea kwenye app hii kwa kuingia kwenye app hiyo kwa kutumia akaunti ambayo umetumia kwenye Smart TV yako ya Android.
Kumbuka Smart TV yako inatakiwa kuwa imeunganishwa kwenye internet au WiFi pamoja na simu yako, yaani Internet inayo tumiwa na simu na inayo tumiwa na Smart TV yako ziwe ni chanzo kimoja. Pia akaunti ya Google unayo tumia kwenye Smart TV yako na unayo tumia kwenye simu yako iwe ni akaunti moja.
Fungua app ya Google Home, kisha fuata maelekezo yalipo kwenye app. Hakikisha unafanya kila kitu ambacho app ina kutaka.
Baada ya kufuata hatua zote na kuhakikisha kuwa TV yako ime onekana kwenye app ya Google Home basi moja kwa moja utaona screen ya simu yako ya Android au iOS kwenye TV yako ya Smart TV yenye mfumo wa Android.
Kama unataka maelezo zaidi unaweza kusoma hapa, pia kama kuna mahali umekwama unaweza kuuliza swali lako kupitia sehemu ya maoni hapo chini.
Kitu cha msingi hakikisha simu yako na Smart TV yako zote zimeunganishwa kwenye Wifi moja, bila kufanya hivyo hutoweza kufanikiwa kufanya hatua hizi.
Kama unataka kujifunza zaidi unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kuzima Bluetooth kwenye Smart TV yoyote yenye kutumia mfumo wa Android.