Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kushare kwa Haraka Document Yoyote Kupitia Link

Tuma document zote za doc, docx, pdf na nyingine kupitia link moja kwa moja
Jinsi ya Kushare kwa Haraka Document Yoyote Kupitia Link Jinsi ya Kushare kwa Haraka Document Yoyote Kupitia Link

Kama wewe ni kama mimi na mara nyingi umekuwa ukijihusisha na kutuma na kupokea document mbalimbali basi huwenda njia hii ikwa bora kwako. Kupitia hapa nitakuonyesha njia rahisi ya kushare document kwa mtu yoyote kupitia link moja kwa moja.

Njia hii ni bora sana kwa sababu inarahisisha na mtu ataweza kuedit file moja kwa moja kwa kutumia link hiyo au kudownload document hiyo kwa haraka. Basi bila kupoteza muda twende moja kwa moja kwenye njia hii rahisi.

Advertisement

Kwa kuanza pakua app ya Microsoft Office, app hizi zipo nyingi hivyo hakikisha unapakuwa app hii kupitia link hapo chini.

Download App Hapa

Jinsi ya Kushare kwa Haraka Document Yoyote Kupitia Link

Baada ya kudownlod moja kwa moja fungua app hiyo kisha tengeneza akaunti kama hauna akaunti, hii itakusaidia sana baada hivyo ningekushauri kutengeneza akaunti, kama unayo kompyuta unaweza kutumia data zako ambazo unatumia kwenye kompyuta yako.

Baada ya kuingia kwenye app moja kwa moja fungua document unayotaka kushare na watu kupitia link, bofya document hiyo kuweza kufungua. Baada ya hapo utaweza kuona kitufe cha kushare kilichopo chini upande wa kulia.

Jinsi ya Kushare kwa Haraka Document Yoyote Kupitia Link

Baada ya hapo chagua sehemu ya link, hakikisha unakuwa na internet kwenye simu yako pia hakikisha umeingia kwenye akaunti yako ya microsoft kupitia app hii.

Jinsi ya Kushare kwa Haraka Document Yoyote Kupitia Link

Baada ya hapo moja kwa moja chagua kama unataka mtu aweze kuedit document unayo mtumia au awe na uwezo wa kuangalia tu documnet na kudownload. Chagua sehemu ya Edit link kama unataka mtu aweze kuedit au chagua View-only link kama unataka mtu aweze kuangalia tu.

Jinsi ya Kushare kwa Haraka Document Yoyote Kupitia Link

Baada ya hapo moja kwa moja utaweza kupata link ambayo unawea kushare na mtu au watu moja kwa moja na hii itakupa urahisi wa kuweza kushiriki na watu wangi zaidi kuliko ambavyo ungeshare na watu document yenyewe kupitia programu mbalimbali kama WhatsApp au kwa kutumia email.

Jinsi ya Kushare kwa Haraka Document Yoyote Kupitia Link

Na hiyo ndio njia rahisi ambayo unaweza kutumia kushare document kwa haraka na urahisi kupitia link, kumbuka njia hii inahitaji kuwa na app ambayo nimekutajia hapo juu hivyo hakikisha unapakua app hiyo kwanza kabla ya kuendelea kwenye hatua hizi.

Kama unataka kujifunza zaidi unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kupata mfumo wa Windows Office Pro 2019 bure kabisa. Kwa maujanja zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania tech kila siku.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use