Android ni moja kati ya mfumo wa uendeshaji wenye mambo mengi sana, hii inapelekea watu wengi kushindwa kutumia kikamilifu baadhi ya sehemu ambazo kawaida zinaweza kuwa na faida mbalimbali kwenye matumizi ya simu za Android ya kila siku.
Kuliona hili siku ya leo tumekuletea Settings za muhimu kwenye simu yako ya Android ambazo unatakiwa kuwasha au kuzima sasa hivi. Kuzuri ni kuwa nitakwambia ni kwanini uzime au uwashe sehemu hizo kupitia settings kwenye simu yako ya Android, basi moja kwa moja twende kwenye makala hii.
TABLE OF CONTENTS
Zima Background Data Baadhi ya App
Background data ni sehemu ambayo hutumia kiasi kikubwa cha data na kufanya data kuisha kwa haraka kwenye simu yako, lakini pia sehemu hii hufanya battery ya simu ya kuisha haraka hivyo unaweza kuzima background data kwenye baadhi ya apps kwa kufanya hivi.
Ingia kwenye Settings, kisha bofya Data usage, kisha chagua Background data na moja kwa moja utaona apps mbalimbali, bofya kuzima kwa apps ambazo hutumi mara kwa mara.
Hakikisha unazima kwenye apps ambazo hutumii kwani ukizima kwenye apps ambazo unatumia mara kwa mara kama ilivyo WhatsApp au Instagram hutoweza kupata Notification yoyote.
Zima Data Sync
Sehemu ya Google Sync ni muhimu lakini sio kila wakati, mara nyingi sehemu hii inakuwa imewashwa moja kwa moja unapo nunua simu ila unaweza kuizima ili kusaidia bando lako lisiweze kuisha kwa haraka na pia kusaidia simu yako kudumu na chaji. Unaweza kuzima sehemu hii kwa kufanya hivi.
Vuta sehemu ya Notification iliyopo juu kwenye simu yako, kisha moja kwa moja tafuta sehemu yenye mishale kama inavyo onekana kwenye picha hapo juu na hakikisha umezima sehemu hiyo. Mara nyingi sehemu hii huwa na majina tofauti lakini lazima utakuta ina neno Sync.
Kumbuka kama unataka kupokea email au vitu vingine mara tuu vinapotumwa basi unaweza kufuata hatua hizo hapo juu kuweza kuwasha tena sehemu hiyo.
Washa Find My Mobile
Find my Mobile ni settings inayopatikana kwenye kila simu, sehemu hii inakusaidia sana kuweza kupata simu yako pale inapo potea au pale ambapo unakuwa hujui umeweka wapi simu yako. Sehemu hii inapatikana kwa kufanya hatua zifuatazo.
Ingia kwenye Settings ya simu yako, kisha chagua Lock screen and Security, baada ya hapo chagua sehemu ya Find My Mobile baada ya hapo hakikisha sehemu zote zimewashwa. Pia sehemu hii inaweza kuwa inapatikana kwa jina tofauti hivyo unaweza kutumia sehemu ya kusearch ndani ya simu yako kuweza kuipata unaweza kutafuta “Find my phone” au “Phone Finder”.
Pia kama sehemu hii haipo kabisa kwenye simu yako basi download app hapo chini kisha install kwenye simu yako na hakikisha sehemu zote hizo zimewashwa, app hiyo ni app kutoka Google na itakusadia sana pale utakapo kuwa umepoteza simu yako utaweza kuona simu yako ilipo.
Washa Device Manager
Kama umewasha settings hapo juu basi ni muhimu kuwasha sehemu ya Device manager, sehemu hii ni muhimu na itakusaidia sana pale ambapo utataka kutumia sehemu ya Find my phone au find my mobile. Bila kuwasha sehemu hii hutoweza kutumia sehemu hiyo hapo juu. Ili kuwasha sehemu hii unaweza kufuata hatua hizi.
Ingia kwenye Settings, kisha chagua Security, alafu chagua Device adminstrators kisha hakikisha sehemu ya device manager imewashwa. Kumbukua sehemu hii inaweza kuwa tofauti kwenye kila simu hivyo kwa urahisi unaweza kuipata kwa kutafuta kwa kutumia sehemu ya kutafuta kwenye menu ya simu yako andika “device manager” kwenye sehemu ya kusearch kupata sehemu hiyo.
Zima Location
Mara nyingi sio watumiaji wote ambao wanahitaji sehemu ya location iwe imewashwa muda wote, kwani sehemu hii kufanya simu yako kuisha chaji kwa haraka na pia hufanya baadhi ya apps kuweza kujua mahali ulipo kwa haraka, ajapo kuwa zipo njia nyingine za kujua hulipo lakini njia hii ya location ni moja kati ya njia ambayo inatumiwa na apps nyingi.
Ingia kwenye Settings kisha bofya Securty au location kisha moja kwa moja tafuta location kisha hakikisha sehemu hiyo imezimwa kwenye simu yako. Pia unaweza kutumia sehemu ya kutafuta kwa kuandika “location” na moja kwa moja zima sehemu hiyo.
Hakikisha unatumia sehemu hiyo kwa ukitumia sehemu ya location iliyopo juu kabisa kwenye sehemu ya Notification unaweza ukakuta sehemu hiyo imejiwasha kwani apps nyingi zina uwezo wa kuwasha sehemu hiyo bila hata wewe kujua.
Zima Sehemu ya Auto Update
Sehemu ya Auto update hii hufanya simu yako ku-update app zote mara moja pale update zinapokwepo kwenye apps mbalimbali kupitia soko la play store. Japo kuwa sehemu hii ni nzuri lakini inafanya bando lako liweze kuisha kwa haraka. Unaweza kuzima sehemu hii kwa kufuata hatia hizi chache hapa.
Na hizo ndio baadhi ya sehemu ambazo unaweza kuzima na kuwasha kwenye simu yako ya Android, hakikisha unaendelea kupitia makala hii kila siku kwani tuendelea kuongeza sehemu nyingine nyingi kadri muda unavyozidi kwenda.
Kama unataka kujifunza zaidi unaweza kusoma hapa kujua baadhi ya Menu za siri ambazo ulikuwa huzijui zinazo patikana kwenye simu yako ya Android. Kwa maujanja zaidi endelea kutembelea tovuti ya Tanzania tech kila siku.