Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Fahamu Kuhusu Sehemu ya ‘Encrypt’ Kwenye Simu za Android

Haya ndio unayotakiwa kujua kuhusu sehemu ya Encrypt kwenye Android
Fahamu Kuhusu Sehemu ya 'Encrypt' Kwenye Simu za Android Fahamu Kuhusu Sehemu ya 'Encrypt' Kwenye Simu za Android

Kama wewe ni mmoja wa watumiaji wazuri wa simu ya Android basi lazima utakuwa umeshawahi kuona sehemu ya Encrypt kwenye simu yako. Sehemu hii imejificha sana na inawezekana kwa namna moja ama nyingine hujawahi kuona sehemu hiyo kabisa kwenye simu yako ya Android.

Kama hujawahi kuona sehemu hiyo usijali, kwani kupitia makala hii nitakuelezea yote ambayo unatakiwa kujua kuhusu sehemu hii ya Encrypt ambayo inapatikana kwenye simu zote za Android. Basi bila kuendelea kupoteza muda zaidi twende tuka jifunze kuhusu sehemu hiyo.

Advertisement

Maneno Yaliyotumika Zaidi

Kwajili ya kufanya uweze kuelewa kuwa urahisi na haraka, hapo chini ni baadhi ya maneno ambayo yametumika sana kwenye makala hii. Ni vyema kujua maneno hayo kabla ya kuendelea kwani yanatumika sana kuelezea mada hii kwa urahisi na kwa lugha bora ya kiswahili.

  • Kusimbua – Hichi ni kitendo cha kufanya decryption au kutoa data kutoka kwenye mfumo wa kuwa encrypted na kuwa decrypted.
  • Usimbuaji – Hichi ni kitendo cha kufanya encryption yaana kubadilisha data kutoka kwenye uwezekano wa kusomeka na mtu au programu na kuwekwa kwenye mfumo ambao ni maalum ambao hausomeki na programu au mtu yoyote hadi pale anapokuwa na password maalum au ufunguo wa usimbuaji.
  • Ufunguo wa usimbuaji – Hii maana yake ni password maalum ambayo inaweza kuondoa data za mtumiaji kutoka kwenye hali ya kuwa encrypted na kuwa decrypted. Password hiyo inaweza kuwa kifaa au namba maalum.

Fahamu Kuhusu Sehemu ya 'Encrypt' Kwenye Simu za Android

Nini Maana ya Encrypt Kwenye Android

Google ilianzisha sehemu ya Encrypt kwenye mfumo wa Android Gingerbread (2.3.x) na kuendelea, hata hivyo kuanzia kipindi hicho sehemu hiyo imekuwa ikipitia mabadiliko mbalimbali kama vile, inasemekana kuwa sehemu hii ya Encrypt huwa inakuja ikiwa imewashwa moja kwa moja kwenye baadhi ya simu za Android zenye mfumo kuanzia Android Lollipop (5.x) na kuendelea.

Sehemu ya Encrypt ni sehemu ambayo inasaidia kuhifadhi data za muhimu za mtumiaji wa simu ya Android na kuzifanya ziwe kwenye usalama zaidi dhidi ya wadukuaji au Hacker. Sehemu hii hufanya kazi ya usimbuaji wa data au kuziweka data ziwe kwenye mtindo ambao hauwezi kusomeka na mtu au programu hadi hapo mtumiaji anapokuwa na password maalum kwaajili ya kusimbua data hizo.

Sehemu ya Encrypt hulinda data nyeti kwenye simu yako. Kwa mfano, mashirika yenye data nyeti za biashara kwenye simu za kampuni zinaitajika kutumia sehemu hii ya Encrypt ili kusaidia kulinda data hizo. Kwa mtumiaji wa kawaida pia unaweza kutumia sehemu ya Encrypt ila ni vyema kendelea kusoma makala hii.

Mambo ya Kuzingatia Kabla ya Kutumia Sehemu ya Encrypt

Fahamu Kuhusu Sehemu ya 'Encrypt' Kwenye Simu za Android

Kama nilivyo kwambia hapo kujuu, simu nyingi za Android zinakuja na sehemu hii ya Encrypt ikiwa imewashwa moja kwa moja, lakini kama unatumia simu ya Android ambayo sehemu hii ya Encrypt haijawashwa basi ni muhimu kufahamu mambo haya machache kuhusu sehemu hiyo.

  • Mara Chache Hufanya Simu Kuwa Slow – Kama kwa namna yoyote ukiwasha sehemu hii unaweza kuona simu yako imekuwa slow hasa pale unapokuwa unawasha simu yako. Hii husababishwa na hatua za kufanya decrypted ambazo hufanywa pale unapowasha simu yako kila mara.
  • Ukiwasha Sehemu Hii Hakuna Njia ya Kuzima – Pale unapo washa sehemu hii ya Encrypt kwenye simu yako ya Android ni vyema kujua kuwa hakuna njia yoyote ya kuzima zaidi ya kufanya Factor reset ambayo inaweza kupoteza data zako zote zilizopo kwenye simu yako.
  • Kama Simu Yako Ipo Rooted ni Lazima Ku-Unroot Kabla ya Kuwasha Sehemu Hiyo – Kama simu yako ipo rooted hutoweza kuwasha sehemu ya Encrypt hadi hapo utakapo ondoa root kwenye simu yako ndipo utaweza kuwasha sehemu hiyo. Baada ya kuwasha kikamilifu sehemu hiyo sasa unaweza kuroot simu yako kwa awamu nyingine.

Hayo ndio mambo ya muhimu ambayo unatakiwa kujua kabla ya kuwasha sehemu ya Encrypt kupitia simu yako ya Android. Kama mambo hayo kwa namna yoyote yatakua hayakusumbui basi unaweza kuendelea kusoma makala hii ili kujua jinsi ya kuwasha sehemu hii ya Encrypt.

Jinsi ya Kuwasha Sehemu ya Encrypt

Kwa mara nyingine, kama unatumia simu zilizotoka hivi karibuni sehemu hii huja ikiwa imewashwa lakini kama unataka kuwasha sehemu hii kwenye simu yako basi unaweza kufuata hatua hizi. Kumbuka kuwa sehemu hizi zinaweza kutofautiana kwa kila simu hivyo unaweza kutumia sehemu ya kutafuta kwenye simu yako kupata ili kupata sehemu hii ya Encrypt.

Fahamu Kuhusu Sehemu ya 'Encrypt' Kwenye Simu za Android

Ingia kwenye Settings, kisha ingia kwenye Security kisha tafuta sehemu iliyo andikwa Encrypt Phone baada ya kubofya hapo soma maelezo yaliyopo, pia hakikisha simu yako ina chaji angalau asilimia 80 au hakikisha simu yako imechomekwa kwenye chaji wakati hatua zote hizi zinafanyaika. Hii ni muhimu kwa kuwa hatua zote hufanyika kwa muda mrefu hivyo ni muhimu kuhakikisha simu yako haizimi katika ya hatua hizo.

Bila shaka hadi hapo utakuwa umepata uelewa kuhusu sehemu ya Encrypt kupitia simu yako ya Android. Kama unataka kujua zaidi kuhusu sehemu nyingine mbalimbali unaweza kusoma hapa kujua maana ya sehemu ya Fast Charing kupitia simu yako. Kwa makala nyingine kama hizi hakikisha unaendelea kutembelea tovuti ya Tanzania Tech kila siku.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use