Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Fahamu Sehemu Zote Mtu Alizopita kwa Kutumia Android

Kupitia njia hii utaweza kujua sehemu zote ulizopita kwa siku nzima kupitia simu yako
Fahamu Sehemu Zote Mtu Alizopita kwa Kutumia Android Fahamu Sehemu Zote Mtu Alizopita kwa Kutumia Android

Ni wazi kuwa kuna wakati unatokea mtu unataka kujua sehemu zote mtu alizopitwa kwa siku nzima, iwe ulipoteza kitu kwenye safari yako ya siku hiyo au unatafuta sehemu ambayo ulipita mara moja na umesahau jinsi ya kufikia sehemu hiyo.

Matatizo hayo na mengine mengi unaweza kuyatatua kwa kutumia njia hii rahisi ambayo itakusaidia sana kujua sehemu zote ambazo wewe au mtu mwingine alipita kwa siku nzima. Basi baada ya kusema hayo moja kwa moja twende kwenye njia hii rahisi.

Advertisement

Kwa kuanza hakikisha unakuwa na simu ya Android, simu yako hiyo inatakiwa kuwa na mfumo wa Android kuanzia Android 7 na kuendelea, hii ni muhimu kwani kuna baadhi ya vitu vinaweza visifanye kazi kwenye simu yako kama simu yako haina Android 7 na kuendelea.

Baada ya kuhakikisha simu yako inayo mfumo huo wa Android, sasa moja kwa moja endelea kwenye hatua inayofuata ambapo unatakiwa kupakua App ya Trackbook, app hii inapatikana kupitia Play store na unaweza kupakua hapo juu au unaweza kupakua app hii kupitia link hapo chini.

Download App Hapa

Baada ya kuinstall app na kuifungua hakikisha unawasha location kwenye simu yako na moja kwa moja endelea kwenye hatua zinazo fuata, kumbuka unatakiwa kuwasha location na kufanya hatua hizi kabla ya kuanza safari yako.

Fahamu Sehemu Zote Mtu Alizopita kwa Kutumia Android

Baada ya kuwasha location sasa fungua app hii na bofya kitufe kilichopo upande wa kushoto chini, kitufe hichi kinasaidia kuweza kujua uko wapi kwa muda huo, hivyo ni muhimu sana kubonyeza kitufe hicho kabla ya kuanza kutumia app hii au kuendelea kwenye hatua nyingine.

Fahamu Sehemu Zote Mtu Alizopita kwa Kutumia Android

Baada ya hapo subiri app hii itaku onyeshe ulipo na utaweza kuona kutufe cha blue kikionyesha alama ambapo ndio eneo unalo patikana kwa muda huo, kama umehakikisha kuwa ndipo ulipo moja kwa moja bofya kutufe cha blue upande wa kulia chini kwaajili ya kuanza kurekodi sehemu unazopita.

Fahamu Sehemu Zote Mtu Alizopita kwa Kutumia Android

Sasa unaweza kuendelea na safari yako na simu yako itaendelea kurekodi kila unapopita kila mtaa na kila eneo ambalo ulipita kwa siku nzima. Mara baada ya kukamilisha safari yako basi moja kwa moja unaweza kubofya sehemu hiyo hiyo na moja kwa moja data hizo zita hifadhiwa kwenye simu yako.

Sasa ili kusoma data hizo, moja kwa moja bofya sehemu ya Tracks iliyopo chini katikati na moja kwa moja utabofya sehemu rekodi mpya kabisa kwenye ukurasa huo.

Fahamu Sehemu Zote Mtu Alizopita kwa Kutumia Android

Bofya kufungua rekodi hiyo ambayo itakuwa na tarehe na muda. Baada ya hapo utaweza kuona data zenye kuonyesha vidoti vya blue ambavyo vina maanisha kila mtaa uliopita kwa siku nzima au kwa muda ambao ulikuwa unarekodi maeneo hayo kupitia app hii.

Fahamu Sehemu Zote Mtu Alizopita kwa Kutumia Android

Kama unavyoweza kuona hapo juu kutokana na kuwa mimi binafsi sikutembea wakati najaribu app hii basi utaona imeonyesha kuwa nilikuwa sehemu moja tu!. Kuona mfano halisi unaweza kuangalia picha hapo chini ambayo ndio inaonyesha vidoti vya blue ambavyo vina ashiria ndio sehemu zote mtu huyo alipo pita wakati anarekodi kwa kutumia app hii.

Fahamu Sehemu Zote Mtu Alizopita kwa Kutumia Android

That’s it! hiyo ndio njia ambayo unaweza kutumia kujua sehemu yoyote ambazo ulipita, unaweza kutumia njia hii kutafuta kitu ulicho kipoteza na unaweza kujua njia zote ulizopita na sehemu ulipo simama hivyo natumaini njia hii inaweza kumsaidia mtu siku moja!.

Kama unataka kujifunza zaidi, unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya ku forward SMS kutoka namba moja kwenda namba nyingine kwa urahisi, pia unaweza kujifunza kwa vitendo hapa jinsi ya kujua mtu anae soma SMS zako bila wewe kujua.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use