Baada ya tetesi za ujio wa sehemu ya Regram, Hivi karibuni mtandao wa Instagram umetangaza ujio wa sehemu hiyo mpya ambayo itaitwa Reshare. Sehemu hiyo itawaruhusu watumiaji wa mtandao wa Instagram kuweza kushiriki au kushare picha ya mtu yoyote kwenda kwenye sehemu ya Stories.
Sehemu hiyo mpya itakuwezesha kushare post kutoka kwenye akaunti yoyote kwenda kwenye sehemu yako ya stories ndani ya mtandao wa Instagram, hata hivyo pale unapo share post au picha kutoka kwenye akaunti fulani, kutakuwa na jina la akaunti hiyo chini ya picha hiyo uliyo share kwenye sehemu yako ya Stories.
Utaweza kushare picha yoyote kwa kubofya kitufe cha kutuma au (paper plane) kilichopo pembeni ya kitufe cha maoni au (Comments), kisha baada ya kubofya hapo utaona sehemu mpya ikiwa imeandikwa Add Post to Your Story bofya hapo ili kushiriki post hiyo kwenye sehemu yako ya Stories.
Hata hivyo Instagram imesema kuwa, utaweza kushiriki picha au post kutoka kwenye akaunti ambazo ziko wazi au (public) na endapo akaunti hiyo ni akaunti binafsi au (private), basi hutoweza kuona sehemu ya Add Post to Your Story mara baada ya kubofya kitufe cha kutuma kilichopo pembeni ya kitufe cha maoni. Pia kama akaunti yako ni ya wazi au (public) na hutaki mtu yoyote kushare au kushiriki picha zako kwenye sehemu yake ya Stories, unaweza kuzima sehemu hiyo kupitia settings kwenye sehemu iliyoandikwa Allow Others to Reshare.
Kwa sasa sehemu hii inapatikana kwa watumiaji wa simu za Android, kwa watumiaji wa simu za iOS sehemu hii inatarajiwa kuja kwenye mfumo huo siku za karibuni. Kama unatumia simu ya Android na bado hujaona sehemu hiyo, hakikisha unaupdate kwanza programu ya instagram kupitia Play Store.