Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Sasa WhatsApp Inaruhusu Kufuta Meseji za Hadi Lisaa Limoja

Kama umekosea kutuma meseji kwa mtu utaweza kuifuta baada ya lisaa
WhatsApp WhatsApp

Mwezi wa kumi mwaka 2017 WhatsApp ilileta sehemu mpya ya Delete For Everyone, sehemu hii inakuruhusu kuweza kufuta meseji ulizo kosea kutumia mtu na kumzuia mtu uliye mtumia asiweze kuzisoma.

Lakini sehemu hii kipindi cha nyuma ilikuwa ikiruhusu watumiaji wa programu ya WhatsApp kufuta meseji ambazo umezituma kwa muda usiozidi dakika saba pekee, Sasa hivi karibuni kupitia App ya majaribio ya WhatsApp Beta sehemu hiyo inaonekana kuongezewa muda na sasa utaweza kufuta meseji ulizo tuma kwa makosa kwa muda usiozidi lisaa limoja.

Advertisement

Yaani kama ulimtumia mtu meseji kimakosa lisaa limoja lililo pita utaweza kuifuta meseji hiyo na inaweza kufutika pia kwa yule mtu uliye mtumia. Sehemu hii haijaishia kwenye meseji moja pekee bali unaweza kufuta meseji zote ulizokuwa unachati na mtu kwa lisaa limoja lililopita. Sasa kama bado hujui jinsi ya kufuta meseji za WhatsApp na zifutike kwa ulio watumia unaweza kusoma makala Hii Hapa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use