Hivi karibuni mtandao wa twitter umekua ukifanya maboresho kadhaa, moja ya kati ya maboresho hayo ni pamoja na kuongeza idadi ya maneno kwenye tweet moja yaani kutoka idadi ya maneno 140 mpaka maneno 280.
Lakini kama haitoshi hivi karibuni Twitter imetangaza kupitia ukurasa wake kuwa sasa utaweza kutumia jina lenye idadi ya maneno 50 tofauti na awali ulikuwa unatakiwa kutumia jina lisilozidi idadi ya maneno 20 pekee.
Starting today, your Twitter display name can be up to 50 characters in length! Go ahead, add that middle name or even a few more emojis. https://t.co/QBxx9Hnn1j
— Twitter Support (@TwitterSupport) November 10, 2017
Hii ina maanisha sasa unaweza kutumia jina lako kamili kama limezindi herufi 20 na kuendelea. Hata hivyo hii sio kwenye upande wa username yaani hapa na maanisha lile jina unalotumia linalo anza na @, hapa na maanisha jina lako kamili. Sehemu ya @username itabaki kuwa na idadi yake ya kawaida ya maneno 15 tu.
Twitter imeleta mabadiliko makubwa kipindi hichi cha nusu ya mwisho wa mwaka, hivi karibuni tuliona mtandao huo ukibadilisha muonekano wake pamoja na icon zake pamoja na kuongeza baadhi ya sehemu kama “night mode” sehemu ambayo inapatikana kwenye kompyuta pamoja na programu za mtandao huo.
Kuelekea mwisho wa mwaka tunategemea kuona mabadiliko mengine makubwa ya mtandao huo kwa mwaka 2018, je ungependa kuona kitu gani kikibadilika kwenye mtandao wa Twitter kwa mwaka unaofuata wa 2018..? tuambie kwenye maoni hapo chini.
Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App ya Tanzania Tech kupitia Play Store pia usasahau kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kupata habari zote za teknolojia kwa njia ya Video.