Mtandao wa instagram bado unaendelea kuboreshwa zaidi, hivi karibuni mtandao huo umetangaza kuleta sehemu mpya mbili ambapo sasa picha na video zilizopo kwenye seheumu ya stories zitaweza kudumu zaidi ya masaa 24.
Sehemu ya kwanza ni “Stories Archive” ambapo sehemu hiyo itakusaidia kuhifadhi picha na video zako za stories, yaani kama kwenye Galler ya simu yako. Utofauti ni kuwa mara baada ya kuhifadhi picha hizo na video kupitia sehemu ya “Stories Archive” wewe pekee ndio utaweza kuziona,
Lakini haijaishia hapo instagram imeleta sehemu ya pili ambayo inaitwa “Stories Highlights,” hii ina-kuwezesha kushiriki na wengine mlolongo wa stories (stories zaidi ya moja) unazo zipenda na zitatokea mbele ya profile yako na mtu akitembelea profile yako ataweza kuziona.
Naposema mlolongo wa Stories ina maana, utaweza kupanga stories zinazo onekana mbele ya profile yako kupitia ma-faili mbalimbali yani kwa mfano, unaweza kuweka mlolongo wa video au picha za stories kama 5 ndani ya faili na kulipa jina labda “muziki,” mara baada hapo moja kwa moja faili hili litatokea mbele ya profile yako na pale mtu atakapo tembelea profile yako na kufungua faili hilo ataweza kuona mlolongo wa video zote tano zilizopo humo kwa pamoja.
Lakini hata hivyo utaweza kuwasha au kuzima sehemu hiyo kupitia Settings endapo unataka picha na video zilizopo kwenye stories zipotee ndani ya masaa 24 kama ilivyo kuwa kawaida. Kwa sasa sehemu hizi zimesha anza kutoka kwenye programu za Instagram za mifumo ya Android pamoja na iOS, hivyo kama bado hujaona sehemu hizo update programu yako ya instagram.
Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.