Hivi karibuni Facebook Messenger ilijiunga na kampuni ya usafirishaji kwa njia ya anga ya KLM Royal Dutch ambapo muungano huo utawawezesha watumiaji wa Facebook Messenger kuangalia taarifa za ndege ikiwa pamoja na kuwasiliana na watoa huduma wa ndege hiyo ya KLM.
Hii ni mara ya kwanza kwa kampuni ya facebook kujiunga na kampuni ya usafirishaji kwa njia ya anga, hii inafanya kampuni ya KLM kuwa ya kwanza kutoa huduma zake kwa njia ya Facebook Messenger. Facebook Messenger imeonekana kupanuka sana kwa sasa hivi karibuni pia application hiyo ya facebook messenger iliingia ubia na makampuni mbalimbali ya biashara ili kuwezesha kulipia bidhaa mbalimbali moja kwa moja kwa kutumia application hiyo ya Facebook Messenger.