Hivi leo kampuni ya Samsung imetangaza kuja kwa headphone zake mpya za kisasa za U Flex, headphone hizi zime tengenezwa maalumu kwaajili ya Samsung Galaxy S8, lakini pia unaweza kutumia kwenye vifaa vingine vya Samsung.
Headphone hizo mpya ambazo ni wireless zinakuja na uwezo wa kipekee wa kutumia sehemu mpya ya Bixby ambayo inapatikana kwenye simu za Samsung Galaxy S8.
Headphone hizo pia zina kuja na vibonyezo vya sauti kwenye kamba yake ya plastiki ya kuvaa shingoni iliyotengenezwa kwa teknolojia ya kisasa huku spika zake zenye urefu wa mm 11 zikiwa na uwezo wa bass na mm 8 kwa nyuma zikiwana uwezo wa tweeter.
Headphone hizi za Samsung U Flex zinafanya kazi kwenye kifaa chochote chenye uwezo wa Android Nougat 7.0 huku ikitumia Bluetooth na WiFi kuleta sauti kutoka kwenye kifaa chako. Hata hivyo haedphone hizo zinatarajiwa kuja na rangi tatu yaani Blue, Black na Ivory, kuhusu bei bado samsung haija weka wazi kuhusu hilo.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video.
Chanzo : GSM Arena