Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Samsung Yazindua Simu Mpya ya Samsung Galaxy J2 Pro (2018)

Simu hii inakuja na kioo bora cha inch 5 chenye teknolojia ya Super AMOLED
Samsung Yazindua Simu Mpya ya Samsung Galaxy J2 Pro (2018) Samsung Yazindua Simu Mpya ya Samsung Galaxy J2 Pro (2018)

Hivi karibuni kampuni ya Samsung nchini Vietnam imezindua simu mpya ya Samsung Galaxy J2 Pro, simu hii inakuja ikiwa na sifa na uwezo bora pamoja na kusemekana kuuzwa kwa bei nafuu zaidi.

Kwa mwaka huu simu hii inakuja na kioo cha inch 5 chenye teknolojia ya Super AMOLED display chenye qHD resolution (540 x 960 pixels), vilevile simu hii ya bei nafuu inakuja na processor yenye uwezo wa 1.4 GHz huku ikiwa inasaidiwa na RAM ya GB 1.5 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 16.

Advertisement

Simu hii pia inakuja ikiwa na uwezo wa Line mbili ambazo zinapatika nyuma kwenye sehemu ya kuweka battery, kwa upande wa kamera Galaxy J2 Pro inakuja na flash zenye teknolojia ya LED kwa mbele na nyuma huku kwa nyuma ikiwa na kamera ya Megapixel 8 na mbele ikiwa na kamera ya Megapixel 5.

Kuhusu mfumo wa uendeshaji simu hii inakuja na mfumo wa Android 7.0 Nougat huku ikiwa na sensor za  Accelerometer pamoja na proximity pekee, Galaxy J2 Pro inatumia battery yenye uwezo wa 2,600 mAh inayoweza kudumu siku moja nzima kama ikichajiwa vizuri. Simu hii inakuja ikiwa ina uzwa bei ya dollar za marekani $144 sawa shilingi za kitanzania Tsh 330,000 kumbuka bei inaweza kubadilika kwa Tanzania.

Simu hii inakuja kwa rangi tatu za Black, Blue pamoja na Gold, simu hii mpya ya Galaxy J2 Pro ina tegemewa kuingia sokoni mapema january na itanza kuuzwa kwa nchi za Asia Mashariki.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use