Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy F62

Simu hii inakuja uwezo mkubwa wa battery yenye 7000 mAh
Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy F62 Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy F62

Baada ya Samsung kuzindua toleo jipya la simu za Galaxy F Series, hatimaye kampuni hiyo hivi leo imeongeza ingizo jipya la Galaxy F62. Simu hii ni ya pili mara baada ya Galaxy F41 ambayo ni ya kwanza kwenye mfululizo wa simu za Galaxy F Series.

Galaxy F62 ni simu mpya kutoka Samsung ambayo inakuja na sifa bora pengine kuliko simu nyingi sana za daraja la kati. Kitu kikubwa na cha tofauti kwenye simu hii ni uwezo wake wa battery ambapo sasa simu hii inakuja na uwezo wa battery ya hadi 7000 mAh.

Advertisement

Kwa sasa ni simu mbili tu kutoka kampuni ya Samsung ambazo zinakuja na uwezo huu wa battery, simu ya kwanza ikiwa Galaxy M51 iliyotoka mwezi wa nane mwaka jana 2020. Simu ya pili ndio Galaxy F62 ambayo inakuja na sifa ambazo pengine karibia zinafanana na Galaxy M51.

Kwa upande wa kioo Galaxy F62 inakuja na kioo cha Super AMOLED chenye inch 6.7, kioo ambacho kinakuja na resolution ya hadi pixel 1080 kwa 2400.

Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy F62

Simu hii pia inakuja na kamera nne kwa nyuma, huku ikiwa na kamera kuu ya Megapixel 64, na nyingine zikiwa na Megapixel 12, MP 5 pamoja na MP 5. Kwa mbele Galaxy F62 inakuja na kamera ya selfie ya Megapixel 32.

Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy F62

Kwa upande wa sifa za ndani Galaxy F62 inakuja na RAM ya kuchagua kati ya GB 6 na 8, pamoja na uhifadhi wa ndani au ROM ya GB 128. Simu hii pia inakuja na mfumo wa uendeshaji wa Android 11 pamoja na mfumo wa Samsung wa One UI 3.1.

Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy F62

Kwa upande wa upatikanaji, Samsung Galaxy F62 inategemewa kuanza kupataikana nchini India na baadae kusambaa duniani kote. Kwa sasa inasemekana kuwa kuna matoleo mawili ya simu hizi yani Galaxy F62 4G pamoja na Galaxy F62 5G. Bila shaka hapa Tanzania tutapata toleo la Galaxy F62 4G. Kujua zaidi kuhusu simu hii unaweza kusoma zaidi hapa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use