Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Samsung Yazindua Simu Mpya ya Samsung Galaxy J5 Pro

Samsung wametoka simu mpya ya samsung galaxy j5 lakini hii ni Pro
Samsung Galaxy J5 Pro Samsung Galaxy J5 Pro

Samsung ni moja ya kampuni yenye utaratibu wa kutoa simu nyingi sana kwa mwaka mzima, tumesha sikia hivi karibuni samsung ilizindua samsung galaxy J7 na leo pia nakuletea taarifa hii kuhusu samsung kuzindua tena simu yake mpya ambayo ni toleo la mwaka huu 2017 la Samsung Galaxy J5 Pro.

Simu ya Samsung Galaxy J5 ni simu ambayo ilizinduliwa mwaka jana 2017 lakini toleo jipya la Samsung Galaxy J5 Pro ndio toleo jipya ambalo linakuja na sifa za zaidi. Simu hii iliyozinduliwa huko nchini Thailand inakuja na sifa za RAM ya GB 3 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 32, lakini sifa zingine zinabaki kama sifa za simu ya zamani yaani Samsung Galaxy J5 ya mwaka jana.

Advertisement

Kama utakua hujui sifa zake kwa undani simu hii ya Galaxy J5 pro ina sifa zifuatazo, simu hii ina kioo cha inch 5.20 pamoja na Processor ya 1.6GHz octa-core ikiwa na kamera ya mbele na nyuma zenye uwezo wa megapixel 13 huku ikiendeshwa na mfumo wa Android 7.0 hivi vyote vikiwa vinaendeshwa na Battery yenye ukubwa wa 3000mAh yenye uwezo wa kudumu na chaji kwa siku moja yaani masaa 24.

Kwa upande wa bei simu hii inauzwa uko Thailand kwa pesa ya thailand THB 9,990 ambayo ni sawa na dollar za marekani za $295 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 660,210.00 kutokana na viwango vya pesa vya siku ya leo. Bado haijajulikana lini simu hii itafika huku Afrika kaa na Tanzania Tech ili kupata habari za simu hii itakapo kuja Tanzania au Afrika kwa ujumla.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use