Siku ya jana wapenzi wa simu za mkononi za Samsung walipata kile walichokua wakikisubiri kwa muda mrefu, Samsung Galaxy S7 simu hiyo ilizinduliwa jana uko Barcelona mida ya saa mbili na nusu za usiku kwa saa za afrika mashariki pia sherehe hizo ziliambatana na uzinduzi wa “Samsung Gear” mpya, Samsung walitangaza vifaa vyao vipya vya Samsung Gear jana ambavyo ndo vilionekana kufurahisha wapenzi wa Samsung kuliko simu yenyewe.
Gear hizo ni Pamoja na “Samsung Gear 360” ambayo ni camera yenye uwezo wa kuzunguka nyuzi 360, pamoja na “Gear VR” hii ikiwa ni kifaa chakuwezesha kuvaa simu yako usoni yani kama vile unaangalia Televisheni. Vifaa hivyo vya Samsung vilivyo vutia sana kwenye uzinduzi huo vitatolewa bure kwa nchi zitakazo wahi kununua simu hizo kwenye website ya Samsung.
Kifaa cha “Samung Gear 360” kina uwezo wa kamera zenye “MP 30” kila moja kamera hizo ziko pende mbili za kifaa hicho, kifaa hicho kidogo kinauwezo wa kuonyesha video live kutoka kwa watumiaji karibia 4 kwa kila mtumiaji wa samsung, kifaa hicho cha Samsung kinauwezo wa kuchukua video live kwenye simu yako bila kusubiri ukitegemea “Samung Galaxy S7” inatumia technolojia ya sasa ya 4G inayotolewa na mtandao wa TIGO kwa nchni Tanzania, kifaa hicho cha Gear 360 kinauzwa kuanzia dollar $100 mpaka $130 kwenye masoko ya mitando mbalimbali Duniani.
Hata hivyo kifaa cha “Samung Gear VR” kimeonekana kupewa support kubwa na facebook ambapo kwenye miezi inayokuja facebook wamepanga kukiboresha kifaa icho kwa hali ya juu na kuwezesha facebook kutumiaka kwa urahisi zaidi kupitia kwenye kifaa hicho cha “Samsung Gear VR” hayo yalidhibitishwa jana na “Founder” wa Facebook “Mark Zuckerberg”.
Kama jana ulikosa kutizama uzinduzi huo wa Samsung Galaxy s7 bonyeza link hapo chini kuangalia video hiyo ya uzinduzi huo uko Barcelona.
BONYEZA HAPA