Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Samsung Yasogeza Mazuri ya Galaxy S23 Kupitia Wahamasishaji

Samsung imeangazia namna gani wahamasishaji (influencers) hawa wamezipokea simu mpya za Galaxy S23
Samsung Yasogeza Mazuri ya Galaxy S23 Kupitia Wahamasishaji Samsung Yasogeza Mazuri ya Galaxy S23 Kupitia Wahamasishaji

Matoleo mapya ya simu za Samsung aina ya Series: Galaxy S23 Ultra, Galaxy S23+, na Galaxy S23 zimeendelea kuwa gumzo mjini huku wahamasishaji maarufu sasa wakielezea namna gani simu hizi zenye hadhi ya premium ni bora na suluhisho la kudumu kwa wateja.

Samsung imeangazia namna gani wahamasishaji (influencers) hawa wamezipokea simu mpya za Galaxy S23 ili wateja waelewe na wapate shauku ya kutumia simu hizi mpya ambazo zimepandisha hadhi teknolojia ya simu nchini kutokana na uwezo mkubwa wa matoleo haya mapya.

Advertisement

Samsung Yasogeza Mazuri ya Galaxy S23 Kupitia Wahamasishaji

Simu hizi za Galaxy S23 zina camera bora zaidi inayofahamika kama 200mega pixel yenye uwezo mkubwa wa kupiga picha nzuri na kurekodi video hata wakati wa usiku. Simu hizi zinaendana vizuri na mazingira husika kutokana na umakini uliotumika katika uengenezaji wake.

Mpiga picha yeyote anaweza kutumia simu hizi za Galaxy S23 kupiga picha za aina tofauti kutokana na ubora mkubwa unaowezesha matumizi ya camera hii katika aina yoyote ya mwanga na kutoa picha zilizo bora kabisa.

Fahad Fuad, ambaye ni muandaaji wa maudhui kuhusu safari za kitalii nchini anasema, “Simu hii mpya ya Galaxy S23 imefanya kazi yangu iwe nyepesi kwani napata picha nzuri za maeneo mapya ya kuzuru na picha hizi naweza kuzipiga wakati wowote iwe usiku au mchana bila kuwa na wasiwasi kuwa simu itazima kutokana na battery yake kuwa na uwezo wa kudumu kwa siku mbili mfulululizo.

Huu ni uzoefu wa aina yake ambao Watanzania wanatakiwa kushuhudia kwani ni mfano mzuri wa teknolojia ya hali ya juu. Nilikubali kuwa mmoja wa wahamasishaji kwa sababu najihusisha sana na masuala ya utunzaji wa mazingira, jambo ambalo Samsung pia inatilia maanani na kutoa kipaumbele. Hili ni jambo jema na la kuigwa.”

Simu hizi za Galaxy S23 Series (S23 Ultra, S23 and S23 Plus) zina muonekano mzuri na rangi zenye mvuto mkubwa ambazo ni pamoja na nyeusi (phantom black), kijani, lavender na rangi ya maziwa (cream). Simu hizi pia zina kalamu maalumu (S pen) ambayo watumiaji wanaweza kutumia kuandika vitu mbalimbali na kufanya michoro.

Samsung Yasogeza Mazuri ya Galaxy S23 Kupitia Wahamasishaji

“Kama mchekeshaji, nahitaji kutuma kwenye mitandao ya kijamii maudhui yenye kusisimua kwa wanaonifuatilia. Galaxy S23 ndio simu halisi kwa kazi yangu kwani naweza kupiga picha na kurekodi video bora ambazo zina sauti ya hali ya juu jambo ambalo linazidi kuzipaisha simu hizi ikilinganishwa na simu zingine.

Huwa nafurahia sana kucheza michezo mbalimbali inayopatikana kwenye Galaxy S23 nikiwa na rafiki zangu. Inabidi utumie simu hii ili upate uzoefu huu ili usije ukadhani naongea tu kinadharia,” alisema Idris Sultan mmoja wa wachekeshaji maarufu Tanzania na ni mmoja wa wahamasishaji wakuu wa Simu za Samsung Tanzania wenye wafuasi wengi mtandaoni.

Idris pia anasema uwezo wa camera hiyo kuvuta vitu kutoka mbali ni jambo la kipekee. “Naweza kuvuta kitu kilichopo mjini kabisa huku nikiwa Kigamboni ambayo ipo ng’ambo ya pili ya bahari.”

Watumiaji, katika hali ya kupata hadhi ya premium, wanaweza kuchukua matukio katika hali ya uhalisia na matukio yote hasa ya kimichezo yanapatikana bila kuchelewa.

Simu zote za Galaxy S23 series zimetengezwa kwa namna ya aina yake na zenye muonekano mzuri kwani zimetengenezwa kutokana na malighafi bora ambayo yamechakatwa hivi kuifanya simu inayoongoza kwa sasa katika matumizi ya malighafi iliyochakatwa ambayo ni bora katika utunzaji wa mazingira.

Mmoja wa wajasiriamali wa teknolojia na pia mhamasishaji maarufu, Irene Kiwia, anasema uzoefu wa simu hii mpya ya Galaxy S23 ndio alikuwa anahitaji kwa muda mrefu. “Hii ni teknolojia ya hali ya juu ambayo imefanya kazi yangu iwe rahisi mno kwani sasa naweza kutuma maudhui yenye ubora wa juu kabisa kwenye kurasa zangu za mitandao ya kijamii. Siwezi hata kufikiria simu nyingine yenye uwezo wa kufanya maajabu haya,” alisema.

Aliwakumbusha watumiaji kuwa simu hiyo ya Galaxy S23 series ina warranty ya miezi 24 ambayo inamuondolea mtumiaji hofu endapo chochote kitatokea huku vigezo na masharti yakizingatiwa. Samsung itahakikisha hupati hasara

Galaxy S23 pia ina usalama na usiri wa kutosha ambao unahakikisha mtumiaji ana uwezo wa kujua endapo anadukuliwa kwa namna yoyote ikiwemo matumizi ya data.

MWISHO

Kuhusu Samsung Electronics Co. Ltd

Samsung inatoa hamasa duniani na kuonesha njia katika masuala ya mawazo chanya na teknolojia yenye kuleta mabadiliko. Kampuni hii inaongoza katika ulimwengu wa TV, simu za smart, mitandao, memory, LSI na LED.

Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea chumba cha habari cha Samsung kupitia news.samsung.com.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use